Tukio hilo limetokea mapema asubuhi ya leo na hivyo kulazimika kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa Nape ambae alikuwa amefungwa mkono wake alisema amepatwa na tatizo hilo leo asubuhi baada ya kuanguka uwanjani japo mbali ya kuanguka alisema hajaweza kuacha kupanda jukwaani kuwaeleza wananchi wa Iringa mjini juu ya mbunge wao mchungaji Peter Msigwa( Chadema)
Kwani alisema ni lazima mbunge Msigwa aondoke katika jimbo hilo baada ya kushindwa kuwatumikia vema wananchi wa jimbo hilo na kuendelea kuwaletea mabalaa mbali mbali .
Nape pia ametymia nafasi hiyo kutaja ahadi lukuki za mbunge Msigwa ambazo alipata kuwaahidi wananchi pasipo kuzitekeleza katika jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment