Bila
shaka mu wazima wa afya wasomaji wa safi hii. Ni siku nyingine tena
Mungu ametujalia tunakutana katika safu yetu na kujuzana mawili matatu
yahusuyo maisha yetu ya uhusiano. Muhimu kupeana darasa maana ni moja ya
kujifunza vitu vipya au kukumbushana vile ambavyo tayari tunavifahamu.
Hakika
hakuna asiyejua mchepuko katika kizazi cha leo. Watu wanachepuka kwenye
ndoa na hata kwenye uchumba. Anayechepuka huwa akilini mwake ana dhima
moja tu, “nachepuka ili kukidhi haja yangu lakini namuheshimu mke
wangu.”
Anayechepuka anaamini kwamba anafanya tendo la siri. Anaamini ni siri
yake hivyo si rahisi kwa mwenzake kuweza kushtukia mchezo. Tatizo hilo
liko katika pande zote mbili japo ukubwa na athari zake zinatofautiana.
Uchepukaji wa mwanamke ni tofauti na ule wa mwanaume. Mwanamke ili
achepuke anahitaji muda mrefu kujishauri kabla hajachepuka. Hakurupuki
kuchukua uamuzi wa kuchepuka ndiyo maana anahitaji mtu wa kumshawishi
sana ili aweze kuchepuka.
Tofauti na mwanamke, mwanaume yeye huligeuza suala la kuchepuka kama
ni halali yake. Mara nyingi wanaume huwa wanaamini kuchepuka ni halali
yao. Hawachukui muda mrefu sana kujishauri kuingia kwenye mchepuko.
Anamuona mwanamke, haraka tu anachepuka.
Wanaume wanaamini kwamba wanapochepuka hawawezi kushtukiwa haraka.
Wanaamini kitendo kile watakifanya kwa siri na umakini mkubwa ili wake
zao wasiweze kugundua janja yao. Kutokana na kujiamini na kujipa taito
ya kuwa mwanaume ndiyo kichwa cha familia, ndiyo maana wengi
wanahalalisha tendo hilo na kulifanya eti liwe la kawaida kwa wanaume.
Ukifanya
tathimini ya wanaume wengi, utagundua kwamba wanajipa uhalali kwamba
bora wachepuke wao na si wanawake. Wanasema wanawake wanapaswa kuheshimu
ndoa zao kama wao wanavyoheshimu lakini katika kipengele cha kuchepuka,
wanawake ndiyo wakiheshimu zaidi lakini wao kipengele hicho
wanakilainisha kidogo.
Wanakilainisha kwa maana kwamba wanaweza kuchepuka, wao ndiyo wenye
majukumu ya kulea familia. Wanaongozwa na tamaa ya miili hususan kwa
vibinti vidogovidogo ambavyo vinahamasisha kwa mavazi, shepu na
muonekano wao kwa jumla.
Wanachepuka kwa madai kwamba wapate ladha tofauti. Eti anapokutana na
kibinti kidogodogo kinamfanya aweze kuinjoi zaidi kwa sababu anakutana
na vionjo vipya. Leo ataanza na huyu, kesho atakutana na mwingine
ataonja ladha mpya kesho tena atahamia kwa mwingine.
Tabia inazidi kukua, haimchukui muda suala la kuchepuka kwake
linakuwa ni mazoea. Haridhiki kabisa na uwepo wa mkewe peke yake. Hawezi
tena kubaki njia kuu, kila siku ataendelea kuchepuka tena akiamini kwa
kuwa mkewe hashtukii basi kwa upande wake ni halali lakini si kwa mkewe.
Hoja ya msingi ya kujiuliza hapa ni moja, kama mwanaume ameamua
kuchepuka, siku mwanamke naye akichepuka itakuwaje? Kwa nini uamini
kwamba mchepuko ni wa upande mmoja na si wa pande zote mbili? Utamu
anaoupata mwanaume katika mchepuko ndiyo huohuo unaoweza kumpoza.
No comments:
Post a Comment