Shabiki
mwanamke aliyekuwa akiishabikia timu ya soka ya Saudia katika eneo la
milki za kiarabu amewakasirisha wanaume wengi katika mtandao wa kijamii
nchini humo.
Kanda ya video iliyowekwa katika mtandao wa You tube
ikionyesha alivyokasirishwa baada ya mchezaji wa Saudia kuchezewa rafu,
imetizamwa na watu 400,000 na kupata maoni 1000.Wengi waliotoa maoni yao ni wanaume waliokasirishwa na hatua ya mwanamke huyo kuwa ndani ya uwanja uliojaa maelfu ya wanaume.
Timu yake ilishindwa ndio maana akakasirika.
Nchini Saudi Arabia,wanawake wamepigwa marufuku kuhudhuria mechi za soka,lakini kwa kuwa mechi hiyo ilikuwa ikichezwa katika miliki za kiarabu,shabiki huyo pamoja na wanawake kadhaa waliokuwa wakiishabikia Saudi Arabia waliweza kujiunga na mashabiki wengine wa kiume katika uwanja huo.
No comments:
Post a Comment