Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la
Mufindi Kusini Mh. Menrad Kigola wakati alipowasili katika mashamba ya
chai ya Ngwazi yanayomilikiwa na kampuni ya Uniliver wilayani Mufindi
ambapo pia alishiriki kuchuma chai akishirikiana na Nape Nnauye Katibu
wa NEC Siasa ,Ittikadi na Uenezi wakati wa ziara yake katika jimbo hilo,
Kinana yuko katika ziara ya siku 30 ya mikoa ya Pwani, Tanga na Iringa
akikagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na
kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na uhai wa
Chama cha Mapinduzi ambapo leo anahitimisha ziara hiyo kwa kufanya
mkutano mkubwa wa hadhara mjini Iringa.
Katika mkutano uliofanyika kijiji cha Nyololo aliyekuwa
Katibu wa CHADEMA Kijiji cha Igowole Bw. Josephat Sibadi Soda amerejea
CCM baada ya uongozi wa chama hicho kutomlipa madeni ya vifaa
mbalimbali alivyochukua madukani wakati wa ujenzi wa mnara wa marehemu
Daud Mwangosi aliyeuwawa wakati wa mapambano ya jeshi la polisi na
wafuasi wa CHADEMA mwaka jana uliojengwa katika kijiji cha Nyololo yeye
akiwa mkandarasi na mbunfu wa mnara huo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mkuu wa mkoa wa
Iringa Dr Christine Ishengoma mara baada ya kuwasili katika mashamba ya
chai ya Ngwazi wilayani Mufindi kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana kulia na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa ,Ittikadi na Uenezi wakishiriki kuchuma chai katika shamba la chai la Ngwazi wilayani Mufindi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
kazi ya kumwagilia maji katika bustani ya miche ya miti ya mbao katika
vitalu vya kuotesha miti vya Umoja wa Vikundi vya Kijamii vya Kigamboni
mjini Mafinga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Nyololo Njiapanda kata ya Nyololo wilayani Mufindi.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akimkaribisha Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ili aongee na wananchi wa kata ya
Nyololo.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa ,Ittikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi wa kata ya Nyololo wilayani Mufindi katika mkutano uliofanyika uwanja wa Nyololo Njiapanda.
No comments:
Post a Comment