Gazeti la Cadenas Ser limetoa taarifa kwamba Rosell amemwambia Jaji wa kesi yake wiki hii kwamba klabu yake ililipa kiasi cha €300,000 kuwasafirisha marafiki wa Neymar kutoka Brazil mpaka Barcelona kwa kutumia ndege binafsi katika utambulisho wa Neymar.
Kundi la marafiki wa Neymar maarufu kama ‘The ‘Toiss’ wamekuwa na Neymar tangu utotoni katika mitaa ya jiji la Sao Paulo, na wamekuwa wakimtembelea Neymar jijini Barcelona, lakini sasa ni mchezaji mwenyewe anayewalipia washkaji zake.
No comments:
Post a Comment