KLABU ya Arsenal imepata pigo baada ya kiungo wake,
Mesut Ozil kuumia na anatakiwa nje kwa kipidi chote kilichobaki kumaliza
mwaka 2014.
Kiungo huyo alikwenda kufanyiwa vipimo vya MRI katika
goti lake na Chama cha Soka Ujerumani kimethibitisha atakuwa nje kwa
miezi mitatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hakufanya
mazoezi na timu yake ya taifa ya Ujerumani mjini Frankfurt baada ya
kuanza kulalamika juu ya hali yake.
Mesut Ozil atakuwa
nje kwa kipindi chote kilichobaki mwaka 2014 baada ya Chama cha Soka
Ujerumani kuthibitisha kuumia kwake goti
Ozil hajaonyesha dalili kubwa za maumivu katika miezi
ya karibuni na amecheza mechi tisa msimu huu, akifunga bao moja.
Taarifa ya Arsenal imesema: "Ozil alilalamika kuwa na
maumivu ya goti la kushoto baada ya mechi na klabu ikakishauri Chama
cha Soka Ujerumani kumfanyia uchunguzi atakapojiunga na kikosi cha timu
ya taifa.
"Klabu itamfanyia uchunguzi wa kina na ni mapema sana
kusema Ozil atakuwa nje kwa muda mrefu kiasi gani".
Ozil, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 42.5 mwaka
jana, amekuwa akikandiwa kwa kucheza chini ya kiwango akiwa na jezi ya
Arsenal.
Habari za kuumia kwake zinazokuja mwezi wa pili ndani
ya msimu mpya, ni pigo kwa kochaa Arsene Wenger ambaye sasa idadi ya
majeruhi inaongezeka katika timu yake, Ozil akkungana na Aaron Ramsey, Mathieu Debuchy, Olivier Giroud pamoja
na Mikel Arteta.
No comments:
Post a Comment