August 29, 2014
WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA NA MAJERUHI SABA KATIKA AJALI MBAYA
Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita
Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga
Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo
Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo
Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka
Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea
Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo Haribika Baada ya ajali hiyo
Mashuhuda wakiwa wamelizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea
Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea , Askari wa usalama wa barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo
Ilikuwa ni Ajali mbaya
Mashuhuda
Baadhi ya Majeruhi wakiwa wanatolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya
WATU
kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba
wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.
Ajali
hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya
abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota
Hiace na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo
ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea
Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.
Walisema
inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka
mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso
ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Muuguzi
Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako
Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7
ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
Alisema
kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa
Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea
kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.
Hata
hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja
kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara
baada ya tukio.
na fredy mgunda
No comments:
Post a Comment