Tuesday 12 August 2014

BIASHARA INAYOLIPA TANZANIA NI SIASA...Hutaki kajinyonge na buibui.

Bunge kutumia zaidi ya Tsh milioni 142 kukodi vipaza sauti.

mic
Wakati kukiwa na malalamiko kwamba Bunge la maalumu la Katiba linagharimu fedha nyingi za walipakodi, uongozi wa taasisi hiyo umetumia Sh142.56 milioni kukodi vipaza sauti kutoka kituo cha mikutano cha kimataifa Arusha (AICC).
Katibu wa Bunge maalumu Yahya Khamis Hamad alithibitisha kukodiwa kwa vipaza sauti hivyo kwa ajili kamati zote 12 na kwamba kila gharama ya chumba kimoja kwa siku ni Dola 450 za Marekani (Dola moja ni wastani wa Sh1,650).
Kwa maana hiyo Bunge hilo linatumia Dola 5,400 sawa na Sh8.91 milioni kwa siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12 vinavyotumiwa na kamati hizo na kwa siku 16  ambazo kamati zitakutana, jumla gharama hizo zitafikia Sh142.56.
“Vifaa vya sauti tulivyokuwa navyo vinalalamikiwa vilikuwa siyo standard (viwango) hasa vya mazungumzo, tumekodi kutoka ukumbi wa mikutano wa AICC na tumekuwa nao usiku mzima kuvifunga,” alisema katibu wa bunge.
Source : Mwananchi