Wananchi wa Kijiji cha Luvuyo Kata ya Madope wakimpokea Mbunge wao, Deo Filikunjombe kwa maandamano.
Wanachama
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi wa Kijiji cha Luvuyo
kata ya Madope wakishirikiana jana na Deo Filikunjombe (kushoto)
kuchimba mifereji ya maji katika barabara ya Luvuyo - Njombe yenye urefu
wa Kilomita 6 ambayo inajengwa kwa ufadhili wa mbunge huyo kwa kiasi
cha zaidi ya shilingi milioni 50.
Mbunge
wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa Luvuyo
mara baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya Luvuyo - Njombe.
Deo
Filikunjombe akisafirishwa katika mkokoteni wa kukokotwa na ng'ombe
baada ya wananchi wa Luvuyo ambao awali walitishia kuhama wilaya ya
Ludewa kuhamia Njombe kusikilizwa kilio chao cha ubovu wa miundombinu
kwa kuanza kujengewa barabara na mbunge huyo
No comments:
Post a Comment