Tuesday 19 August 2014

HABARI NJEMA KWA JAMII YA WANA MBEYA; AGA KHAN KUANZA KUTOA HUDUMA ZA WANAWAKE KUJIFUNGUA

HABARI NJEMA KWA JAMII YA WANA MBEYA; AGA KHAN KUANZA KUTOA HUDUMA ZA WANAWAKE KUJIFUNGUA


HOSPITALI ya Aga Khna Primary Medical Center, Mbeya, inatarajia kuanza kutoa huduma za kisasa za wanawake kujifungua.
Habari za uhakika kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari, zimesema kuwa, Hospitali hiyo, ambayo ipo katikati ya Jiji la Mbeya, tayari imepata vifaa vyote vya kisasa na vimefungwa ndani ya hospitali hiyo.

Huduma hiyo inaanza kutolewa mwezi Septemba mwaka huu na wanawake wa kwanza watapewa huduma hiyo bure, bali wengine watakuwa wanajifungua kwa fedha zisizozidi Laki mbili.

wanawake wote wajawazito ambao zimefika siku zao za kujifungua, imeelezwa kuwa watatakiwa kufika katika hospitali hiyo bila kitu chochote kama zifanyavyo hospitali zingine, na wakishajifungua kila mmkoja atapewa taulo(Baby show) la mtoto.