KIMBEMBE CHA MADAKTARI
August 28, 2014IMEBUMA kwao! Madaktari wawili, Hamis Chacha na Shengena wa zahanati moja iliyopo Yombo Buza jijini Dar wamejikuta katika wakati mgumu baada ya polisi kuwaibukia na kuwaweka chini ya ulinzi kwa madai ya kufanya jaribio la kumchoropoa mimba msichana mmoja aliyedaiwa kuwa ni denti wa chuo f’lani cha digrii za juu, Dar.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Agostii
25, mwaka huu katika zahanati hiyo ambayo jina tunalihifadhi kwa
sasa.Awali, Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ikiwa
katika pitapita zake ilinasa tukio hilo ambapo polisi walikuwa ndani ya
zahanati hiyo wakiwaweka chini ya ulinzi madaktari hao.
OFM ilifanikiwa kuzama ndani ya zahanati hiyo na kuingia kwenye chumba cha kilichodaiwa hutumika katika zoezi hilo.
OFM ilifanikiwa kuzama ndani ya zahanati hiyo na kuingia kwenye chumba cha kilichodaiwa hutumika katika zoezi hilo.
Daktari Shengena alipoona kamera ya OFM
alitaka kukimbia licha ya kuwepo kwa askari ndani ambapo walitumia nguvu
za ziada kuwadhibiti vyema na kuingizwa ndani ya chumba alichokuwemo
mwenzake ambaye naye alinaswa akiwa na vifaa vilivyodaiwa ni vya
kuchomolea mimba akiwa amevificha kwenye mfuko wa rambo.
Baada ya maafande kuwaweka chini ya ulinzi,
madaktari hao walizua kituko kufuatia kuzitupa chini shilingi 40,000
walizopewa na denti huyo kama malipo ya kazi hiyo wakidhani ni za
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘Takukuru’.
kiasi cha fedha cha Shillingi arobaini elfu walicholipwa madaktari kwa ajili ya kufanikisha zoezi la utoji mimba.
Wakizungumza na waandishi wetu baada ya
kuulizwa nini kilikuwa kikiendelea chumbani humo, Dokta Chacha alidai
kuwa mgonjwa huyo ana tatizo kwenye kizazi hivyo alikuwa akitaka
kusafishwa na si kutoa mimba maelezo yalikosolewa na denti huyo aliyedai
kuwa alikwendwa kwa mapatano ya kumchoma mimba ili akaendelee na masomo
chuoni.
Akijibu kuhusu kwa nini alivificha vifaa va kutolea mimba kwenye
mfuko, Dokta Chacha alijiumauma na kusema denti huyo alifuata taratibu
zote kama wagonjwa wengine, lakini alishindwa kuonesha risiti au cheti
cha kumsajili mgonjwa huyo kwa ajili ya matibabu.Kichekesho kingine kilikuwa wakati OFM na wanausalama wakitoka nje ya zahanati hiyo na watuhumiwa na kukuta kwenye maeneo mengine kukiwa kweupe na kusemekana kuwa, madaktari na manesi walioshuhudia wenzao wakitaitiwa walitoka nduki kwa kuogopa ushahidi.
Mwishowe watuhumiwa hao walifikishwa katika Kituo cha Kidogo cha Polisi Buza na kufunguliwa jalada lenye Kumbukumbu Na. BUZ/RB/32/2014 kabla ya baadaye kufikishwa Kituo cha Polisi Chang’ombe, Dar kwa ajili ya mahojiano ya kina kuhusiana na sakata hilo.
No comments:
Post a Comment