WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO
August 25, 2014
August 25, 2014
Wakongwe
wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi
cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa
Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Kikundi
cha ngoma kikitumbuiza mara baada ya kuwasili kwa wachezaji wastaafu wa
Klabu ya Real Madrid kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Meneja
Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akigawa fulana maalum zenye
nembo ya TANAPA na Real Madrid kwa mmoja wa wachezaji kabla ya kuelekea
Mlima Kilimanjaro.
Mkuu
wa Hifadhi ya Kilimanjaro Erastus Lufungulo akitoa neno la ukaribisho
kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid walipowasili kwa ziara
fupi.
Meneja
Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani)
akiongoza msafara wa wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro
Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakongwe wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro.
Waziri
wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa
cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid
mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima
Kilimanjaro.
Wachezaji
wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na
watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya
kupanda Mlima Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment