Saturday 16 August 2014

TANGAZO LA AJIRA JESHI LA POLISI - 2014/2015

TANGAZO LA AJIRA JESHI LA POLISI - 2014/2015






Katika mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi Tanzania linatarajia kuajiri wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Juu wa mwaka 2013/2014. Ili kutekeleza azma hii waombaji watajaza kikamilifu na wataambatanisha vivuli vya vyeti vyao na kutuma Makao Makuu ya Polisi kwa njia ya Posta kabla ya tarehe 31.08.2014 kwa anuani ifuatayo:

Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S. L. P. 9141,
DAR ES SALAAM
WAOMBAJI WAWE NA TAALUMA ZIFUATAZO:
Shahada: Menejimenti ya Rasilimali Watu, Utawala katika Utumishi wa Umma, Uchumi, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji[BaLE], Sheria, Ualimu, Maendeleo ya Jamii, Uandishi wa Habari, Uandishi wa Habari za Michezo, Mawasiliano ya Umma, TV & Redio Production, Michezo, Ugavi[BA in Procurement & Supplies], Mawasiliano ya Redio[Bsc in Radio Communication], Mazingira[BA in Environmental Disaster Mgt], Uhandisi Mitambo, Uhandisi Madini[Mining Engineering], Uchoraji[BA in Fine Arts], Fedha na Benki[Finance & Banking], Daktari[Medical Doctor] na Daktari wa Meno[Dental Surgeon], Mkemia, Bailojia[Molecular Biology].
Stashahada: Utunzaji Kumbukumbu, Katibu Muhutasi[Personal Secretaries], Mawasiliano ya Redio, Matengenezo ya Kompyuta, Fax na Photocopy Machines, Mafundi Mitambo wa Meli, Mafundi Umeme wa Magari, Ugavi[Procurement & Supplies], TV na Video Production, Manahodha, Tabibu[Clinical Officer], Tabibu wa Meno[Dental Therapist], Mzoeza Viungo[Psysiotherapist/Occupational Therapist], Fundi Sanifu Mionzi[Radiographer] na Fundi Sanifu Macho[Optometrist].
Astashahada: Uzamiaji, Mpishi, Fundi Pikipiki, Fundi Ushonaji na Muuguzi Msaidizi[Enrolled Nurse].
MASHARTI KWA MWOMBAJI
1. Mwombaji atajaza fomu ya maombi kikamilifu na atabandika
picha yake “Ppt Size” kwenye fomu.
2. Mwombaji aambatanishe katika fomu vivuli vya vyeti vyote
yaani cheti cha kuzaliwa, kuhitimu elimu ya sekondari[Leaving
& Academic], cheti/vyeti vya taaluma[Academic Transcript].
3. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
SIFA ZA MWOMBAJI
1. Awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
2. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
3. Awe amehitimu chuo mwaka wa masomo 2013/2014 tu.
4. Awe na tabia njema.
5. Asiwe na kumbukumbu za kutenda uhalifu.
6. Awe na afya njema[kimwili na kiakili]
7. Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.
8. Asiwe na alama za kuchora mwilini[tatuu].
9. Awe na urefu usiopungua sentimita 155.
10. Asiwe mtumiaji wa madawa ya kulevya.
11. Awe hajaajiriwa na idara nyingine Serikalini.
12. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Polisi.
13. Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje ya Tanzania.
Fomu:- Fomu ya Ajira Elimu ya Juu 2013/2014 zinapatikana kwenye tovuti www.policeforce.go.tz au kwa wakazi wa Mbeya wafike ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.

USAILI WA JESHI LA POLISI TANZANIA KWA WAKAZI WA MBEYA.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,  BARAKAEL .N. MASAKI – ACP anawatangazia Wananchi wote ya kuwa orodha ya majina ya vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi inapatikana kwenye tovuti ya Polisi: www.policeforce.go.tz au wafike ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya iliyopo Forest jirani na Mahakama kuangalia majina yao.
Muhimu:


·         Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo  juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.
·         Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
·         Mwombaji  awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..
·         Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.
Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.

TAREHE YA USAILI KWA MKOA WA MBEYA NI 28.09.2014 HADI 01.10.2014. SAA 08:00 ASUBUHI HADI 10:00 JIONI.