Mwanaume Mmoja Ameua Watu Sita Baada ya Mkewe Kuchepuka na Wanaume Hao Kingono
Wednesday, August 13, 2014
Mwanaume mmoja ameua watu 6 baada ya
mkewe kujihusisha na wanaume hao kingono,kutokana na tukio hilo
mwanamume huyo amehukumiwa adhabu ya kifo nchini China.
Shao Zongqi, mwenye umri wa miaka 38 alikutwa na hatia baada ya kutekeleza mauaji hayo mwezi January mwaka huu.
Kwa muujibu wa mahakama, Shao alipanga
kulipiza kisasi baada ya kugundua kua mkewe alikua na mahusiano na
wanaume wawili tofauti,shirika la habari la Xinhua limeeleza hayo.
Wakati wa sherehe za mwaka mpya wa
kichina,Shao alijeruhi wanaume tisa, na kumuua mmoja pamoja na familia
yake na wanaume wengine wawili wa jirani,wakati mwanamume mmoja akiwa na
mkewe na mtoto wao wa kiume walinusurika katika tukio hilo.
Wakati hukumu hiyo ikitolewa siku ya
jumatatu, iliamuriwa Shao alipe kiasi cha yuani 604,000/- sawa na dola
za kimarekani 98,000/- kwa familia walio hai ambao waliondokewa na jamaa
zao kutokana na shambulio hilo.
Pamoja na kulipa faini hiyo Shao ameapa kukata rufaa kutokana na hukumu hiyo ya kifo inayomkabili.