Monday 15 September 2014

CHOVYA CHOVYA::Sikio la Kufa Halisikii Dawa, Aunty Ezekiel Akutwa Tena na Yule Mume wa Mtu




Stori: Imelda Mtema
Mahaba niue! Baada ya penzi la staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Moses Iyobo ‘Moze’ kushamiri kwa kasi ya umeme, wawili hao wamenaswa wakisindikizana kimalovee kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar.

Tukio hilo lililopigwa chabo na mwanahabari wetu mwanzo mwisho, lilijiri Ijumaa iliyopita ambapo wawili hao walionekana wakiingia pamoja kimahaba eneo hilo.

Aunt ambaye ni mke halali wa Sunday Demonte anayedaiwa kufungwa Uarabuni kwa msala wa madawa ya kulevya, alionekana na Iyobo ambaye pia ni mume wa mtu (Mwengy) wakishikana mikono katika sehemu ya kukagulia mizigo kisha wakaagana kwa mabusu motomoto.

Mwanahabari wetu alipomuuliza Aunt kulikoni, alifunguka: “Nakwenda Marekani lakini wengine wote unaowaona wananisindikiza kama desturi ya watu kusindikizana.”Kweli? 
GPL

No comments:

Post a Comment