Monday 15 September 2014

UBARIKIWE::MISS ILALA NO 2 AWAPATIA ZAWADI WATOTO YATIMA, WAMUOMBEA DUA MAALUM

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Moshi akitoa mkono wa heri kwa Miss Nasreem Abdul.
Miss Nasreem Abdul akiwa pamoja na wasichana waliofanyiwa ukatili na kutelekezwa na sasa wanalelewa na Taasisi ya wanawake katikaa Jitihada Kimaendele 'WAJIKI' Kilichopo Mwananyamala Kinondoni Jijini Dar.
Miss Nasreem Abdul akiwa na watoto yatima wa kituo cha AL- HIDAYA ORPHANS CENTER cha buguruni.
Miss Ilala namba mbili Nasreem Adbul ameonesha mfano wa kuigwa kwa warembo wengine baada ya kuwapatia zawadi watoto yatima wenye uhitaji na wanaoishi mazingira magumu.

Kwa mujibu wa meneja wa mrembo huyo Livingstone Mkoi alisema kuwa" Katika kile kinachoonekana kuguswa na matatizo  ya kijamii na ni siku chache tu tangu achukukue ushindi wa pili katika kinyang'anyilo cha kumtafuta Miss Ilala mrembo wetu ametembelea vituo kadhaa vya watoto yatima pamoja na TAASISI YA WANAWAKE KATIKA JITIHADA KIMAENDELEO "WAJIKI" Iliyopo Mwananyamala Jijini Dar na kutoa kile alichokuwa nacho" Alisema Mkoi
Aidha kituo kingine alichotembelea  mrembo huyo ni cha AL- HIDAYA ORPHANS CENTER Kilichopo Buguruni ambacho kina watoto zaidi ya 70 huku kila siku wanaongezeka.
Hata hivyo kwa upande wa mrembo huyo alisema" Namshukuru Mungu kwa kunisaidia kuwa mshindi wa pili na wiki hii tunaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya shindano la Taifa la Urembo hivyo nimeguswa na matatizo wanayoyapata watoto yatima na ndiyo maana nimetoa zawadi yako kwako kama msaada na Mungu akinijalia baadae tena nikishinda taji la Taifa nitaendelea mikoani kwani watoto wako wengi wanaoitaji msaada" Alisema Nasreen

No comments:

Post a Comment