RAIS YOWERI MUSEVENI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MOJA
Rais
wa Uganda Yoweri Museveni akiteremka katika ndege iliyomleta leo jijini
dar es Salaam kwa ajili ya ziara yake ya siku moja nchini Tanzania .
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua
Gwaride la Maaskari pamoja na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni
baada ya kuwasili leo jijini katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya siku moja. Rais
wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (Kulia) pamoja na
mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) wakiangalia ngoma za
utamaduni baada ya kuwasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
Mwalimu Julius Nyerere Leo jijini Dar es Salaam ,kwa ajili ya ziara ya
siku moja hapa nchini. Rais
wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (Katikati)akipata
maelekezo kutoka kwa mwongoza msafara na kushoto ni Rais wa Uganda
Yoweri Museveni ambaye amewasili nchini leo kwa ajili ya ziara ya siku
moja . ( Picha na Lorietha Laurence-Maelezo). Ndege
iliyomleta Rais wa Uganda Yoweri Museveni ikiwa imetua katika Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa ziara yake
ya kikazi ya siku moja ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment