Sunday 14 September 2014

SAMBAZA UPENDO::SERENGETI FIESTA YAFUNIKA NDANI YA GEITA

Mkali kutoka pande za Mwanza, Young Killer akichana mistari stejini.Ommy Dimpoz akiimba kwa pamoja na mrembo kutoka pande za Geita nyimbo ya ME & YOU. Niki wa Pili akiwakilisha Crew ya Weusi. Mkongwe wa Hip Hop, Fid Q akitiririsha 'vesi' ndani ya Ukumbi wa Desire Park.Chege na Temba wakipagawisha mashabiki stejini. Mzee wa Kula Ujana, 'Nay wa Mitego' akiimba sambamba na mashabiki wake Geita.  
Linah akifanya vitu vyake stejini.
Msanii kutoka pande za Bukoba ajulikanaye kama BK Sande akifungua burudani ndani ya Ukumbi wa Desire Park mkoani GeitaDirector Shaibu akiachia vimbwanga jukwaani.Mr Blue akienda Sanjari na mashabiki waliofurika ndani ya Ukumbi wa Desire Park mkoani Geita.
TAMASHA la Serengeti Fiesta 2014 usiku wa kuamkia leo limeonyesha hali ya kukubalika vilivyo kwa wakazi wa Geita baada ya uongozi wa Tamasha hilo kuamua kuwapa burudani hizo kwa mara ya kwanza na wakazi hao kuonyesha hali ya kuitikia vilivyo kwa kufurika ndani ya Ukumbi wa Desire Park mkoani humo.
(PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GEITA)

No comments:

Post a Comment