Wednesday 15 October 2014

MBEYA::MWANAMKE AUAWA KWA KUSHINDWA KULIPA T.SH,3,000/=



Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,Ahmed Msangi.
 
WAKATI wajumbe maalum wa katiba wakiwa wamependekeza suala la haki za binadamu na mgawanyo sawa wa madaraka kati ya mwanamke na mwanaume, vitendo vya ukatili na mauaji kwa wanawake vimezidi kushika kasi mkoani Mbeya.

Katika tukio la hivi karibuni, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa kwa jina la Rutina Ng’ekele(75), mkazi wa kijiji cha Mabondeni, kata ya Bulyaga, tarafa ya Tukuyu mjini wilayani Rungwe, amefariki dunia katika hospitali ya Makandana wilayani Rungwe, akiwa anapatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa mateke na ngumi.

Taarifa zinasema kuwa, Bibi huyo alishambuliwa vikali sehemu mbalimbali za mwili wake na mtu aliyefahamika kwa jina la Nicolous Afyasisye.

Tukio hilo limeelezwa kutokea Octoba 4, mwaka huu, majira ya saa moja usiku na kupelekea marehemu kulazwa hospitalini hapo mpka mauti yalipomfika jana Octoba 14, mwaka huu, saa sita mchana.

Chanzo cha tukio hilo, kimeelezwa kuwa ni marehemu kumlipa mtuhumiwa Tsh.7,000/= badala ya Tsh.10,000/= aliyokuwa akidaiwa na mtuhumiwa, jambo ambalo lilisababisha mtuhumiwa aanze kumshambulia marehemu.

Baada ya kitendo hicho, mtuhumiwa alikimbilia kusikojulikana na Jeshi la polisi limethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.

Kamanda wa polisimkoani Mbeya, Ahmed Msangi, alisema kuwa anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahala alipo mtuhumiwa wa tukio hilo, azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
 

No comments:

Post a Comment