Wednesday 29 October 2014

SAMAHANI KWA PICHA HIZI::MBWA WAKUTWA WAKITAFUNA MWILI WA BINADAMU HUKO SONGEA


Fuvu la kichwa likiwa linazolewa 

 Mabaki ya mwili yaliyokutwa katika eneo la kijiji cha Lupapila wilaya ya songea mkoani Ruvuma yakikusanywa na wataalamu kutoka hospital ya mkoa wa Ruvuma.

 MIFUPA ya masalia ya binadamu wa jinsia ya kiume ambaye hakuweza kufahamika jina na kukadiriwa kuwa na miaka (30) yamegundulika na Zaujia Pilly (70) mkazi wa kijiji cha Lupapila wilaya ya songea mkoani Ruvuma

Ruvuma wakati akienda kuchimba dawa za kienyeji baada ya kuwaona mbwa wakishambulia sehemu za mabaki hayo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea oktoba 26 mwaka huu majira ya saa 9:45 alasiri huko katika kijiji cha Lupapilamtaa wa Mahinya kata ya Subira nje kidogo ya manispaa ya Songea.
 
Alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio kwenye msitu wa uwanja wandege ilikutwa mifupa ya binadamu wa jinsia ya kiume ikiwemo fuvu la Kichwa, Mbavu, Mikono na Miguu wakati sehemu ya kiuno na mapaja ikiwa imeharibika vibaya.
 
Alifafanua kuwa mabaki ya mwili huo yaligunduliwa na Zaujia Pilly wakati akienda kuchimba dawa za kienyeji kwenye msitu huo ghafla aliwaona Mbwa wakifukuzana kugombania mabaki ya mwili wa binadamu.
 
Alieleza zaidi kuwa Zaujia baada ya kugundua tukio hilo alitoa taarifa katika uongozi wa serikali ya Mtaa na kisha taarifa zilipelekwa katika kituo kikuu cha polisi cha songea mjini ambako baadaye polisi walifika eneo la tukio wakiwa wameongozana na Daktari kutoka hospitgali ya Mkoa wa Ruvuma ambaye aliyafanyia uchunguzi mabaki ya mwili huo na kubaini kuwa marehemu alikuwa amepigwa na kitu kizito kichwani kwenye eneo la kisogo kilichopelekea kifo chake.

Kamanda Msikhela alisema kuwa kufuatia tukio hilo hakuna mtu yeyote anayehusishwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma linaendelea kufanya chunguzi wa kina juu ya kifo hicho.

 Na Amon Mtega -Songea

No comments:

Post a Comment