Tuesday 28 October 2014

Unafahamu kilichomfanya Mnigeria kuruka ukuta wa Ikulu ya Marekani? Kisome hapa.

Adesanya 
Moja ya taarifa zilizochukua headline wiki iliyopita ni kuhusiana na tukio la mtu mmoja kuruka ukuta wa ikulu ya Marekani, na baadaye kukamatwa baada ya kushambuliwa na mbwa kabla ya kutiwa nguvuni na walinzi wa ikulu hiyo, Secret Service.
Habari zinasema hii si mara ya kwanza kwa Mnigeria Dominica Adesanya (23) kuruka ukuta wa White House, na safari hii baada ya kumfikisha mahakamani imebainika kuwa ana tatizo la akili hivyo hawezi kushitakiwa akiwa na hali hiyo.
Daily Mail imeripoti kuwa baada ya mahakama kuthibitisha vipimo kutoka hospitali kuwa ana tatizo hilo, mahakama iliamuru awekwe chini ya ulinzi huku akipata matibabu ya ugonjwa huo mpaka Desemba 22 kesi yake itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Adesanya ametolewa mahakamani hapo akipiga kelele za kuomba msaada huku akilaumu kitendo cha kukamatwa kwake.
Hii ni mara ya pili kwa jamaa huyo kuruka ukuta wa White House, ambapo mara ya kwanza Adesanya ambaye ana asili ya Nigeria kufanya hivyo ilikuwa Julai 27 majira ya saa 4 usiku mwaka huu, na kurudia tena Oktoba 23 majira ya saa 1 jioni.
White-House-jumper-jpg

No comments:

Post a Comment