Tuesday, 26 August 2014

KAULI YA MO::UTAJIRI HAUJI KIRAHISI RAHISI...

MO azindua jarida la IRIS Executive na kusema utajiri hauji “kirahisi rahisi”

DSC_0281
Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP Mh. Mohammed Dewji (Mb) ambao ndio wadhamini wakuu wa sherehe za uzinduzi wa jarida la IRIS Executive (katikati), Ofisa Mtendaji Mkuu wa IRIS Executive Development Centre, Phylisiah Mcheni (kulia) na Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Bw. Vipul Kakad wakiwa meza kuu kwenye hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa jarida IRS Executive ambalo tolea la jipya ukurasa wa mbele limepambwa na picha ya Mh. Mohammed Dewji “MO”. (Picha na Zainul Mzige wa MOblog)
Na Mwandishi wetu
OFISA Mtendaji Mkuu wa  MeTL GROUP na Mbunge wa Singida Mjini kupitia tiketi ya CCM, Mohammed Dewji, amesema kazi ya kutengeneza utajiri sio rahisi, inahitaji mipangilio madhubuti na uvumilivu ili kufanikisha lengo hilo.
Mbunge huyo ambaye kampuni zake zimeajiri watu 24,000 sawa na asilimia 5 ya ajira rasmi nchini, amesema kutengeneza utajiri hakufanyiki kwa njia ya kupanda lifti bali ni ujenzi wa tofali kwa tofali hadi nyumba kukamilika.
Akiwa anaendesha kampuni ambayo pato lake hadi mwishoni mwa mwaka huu litakuwa ni za Marekani bilioni 1.5 amesema uwezo huo haukupatikana  mara moja bali umetokana na nia pamoja na kutrumia vyema fursa zinazopatikana nchini.
Amesema katika uzinduzi wa Jarida la IRIS Executive linalomilikiwa na Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambacho kina ofisi Tanzania, Kenya na wawakilishi nchini Uganda na Rwanda Vijana wa Tanzania wapo katika nchi inayofaa na wakati muafaka na hivyo wanauwezo mkubwa wa kutoka kiuuchumi.
Alisema wakati uchumi wa afrika unakua kwa asilimia 5 na wa dunia kwa asilimia 8 uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 7 hali inayotoa nafasi kubwa kwa vijana kusonga mbele ili mradi wachapekazi kwa bidii na maarifa.
DSC_0326
Mhariri Mtendaji wa jarida la IRIS Executive, Mike Mina akielezea historia fupi ya gazeti hilo kwa wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa jarida hilo ulifanyika usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Dar Es Salaam Serena. Kushoto ni Meneja Masoko wa jarida la IRIS Executive, Alinda Henry.
Katika uzinduzi wa jarida hilo lenye nakala 40,000 mtaani katika nchi zote za Afrika Mashariki na likizingatia mahitaji ya ukuaji wa uchumi Afrika Mashariki, Dewji maarufu kama Mo amewataka vijana kuhakikisha kwamba wanatoa habari kwa haraka na kwa muda muafaka kwani ndio kichochea cha uwekezaji na uendeshaji.
Alikubaliana na Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo Mike Mina kwamba habari ni kitu muhimu katika kufanikisha uwekezaji na biashara, lakini akasisitiza habari zinaoztolewa katika muda muafaka.
IRIS Executive ambalo katika toleo lake la pili limeandika habari kumhusu Mo ambaye kwa miaka 15 amefanikiwa kuiondoa MeTL kutoka pato la dola milioni 30 hadi dola bilioni 1.5,huandika na kufuatilia masuala ya maendeleo hasa katika sekta zinazogusa uchumi moja kwa moja kama fedha na benki, uzalishaji viwandani, mafuta na gesi, kilimo na uwekezaji.
Toleo lake la kwanza lilimgusa Ofisa Mtendaji wa IPP, Dk Reginald Mengi.
Akizungumza historia yake kabla ya kuzindua jarida hilo alisema kwamba yeye alizaliwa nyumbani na mkunga wa kienyeji 1975 kama walivyo watanzania wengi na kwamba amefikia hapo kwa bidii kubwa akitaka vijana kuiga safari hiyo kwa kutumia vyema fursa zilizopo.
DSC_0349
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni akizungumza na wageni waalikuwa kwenye uzinduzi huo.
Kampuni ya MeTL inafanya shughuli anuai kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo na viwanda, lojistiki, huduma za fedha,majumba ya biashara, petroli,vinu vya kusindika nafaka,vifaa vya plastiki, usambazaji na masuala ya simu.
Aidha kampuni hiyo inajivunia kufanya biashara katika nchi za Ethiopia, Malawi, Msumbiji, Zambia, Dubai, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Sudan Kusini na Kenya huku ikiwa na viwanda zaidi ya 31 nchini Tanzania pekee.
Dewji amepata elimu ya juu kutoka Chuo Kikuu cha Georgetown nchini Marekani ambacho katika baadhi ya maelezo yake anasema ndio iliyomfumbua macho na kuona umuhimu wa kutumia fursa za ushindani wa kibiashara duniani.
Mara nyingi MO amekuwa akisema,Falsafa yake kama mfanyabiashara sio kuridhika na mafanikio aliyonayo bali kuendelea kufanyakazi kwa bidii na kufanikiwa zaidi. Alisema.
DSC_0392
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji “MO” (Mb) ambao ndio wadhamini wakuu wa sherehe za uzinduzi wa jarida la IRIS Executive akitoa nasaha zake kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa jarida hilo usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Dar es Salaam Serena.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu- IRIS Executive Development Center, Phylisiah Mcheni akimkaribisha MO kuzindua jarida hilo, pamoja na kumshukuru kwa kudhamini uzinduzi huo pia alisema, IRIS Executive ni jarida pekee lenye makazi yake nchini Tanzania kuweza kufika nchi zote za Afrika Mashariki kwa idadi za nakala na taarifa zilizomo ndani zinazolenga uwekezaji na biashara kwa watendaji ni matumaini yetu kwamba wasomaji watakuwa siku zote wanajua nini kinachoendelea kwa manufaa yao, makampuni na sekta mbalimbali zinazochangia katika kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa.
Aidha pamoja na kulipata jarida hilo la IRIS Executive katika nakala halisi pia hupatikana katika mtandao kwa anuani ya www.irisexecutive.com
Uzinduzi huo ulihudhuria na maofisa watendaji wa ngazi mbalimbali kutoka makampuni yanayojishughulisha na uwekezaji,biashara, habari na utamaduni.
DSC_0368
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni (kulia) akiitambulisha timu yake ya vijana na jarida hilo kwa wageni waalikwa.
DSC_0399
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji “MO” (Mb) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni wakijiandaa kuzindua rasmi jarida hilo.
DSC_0419
Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji “MO” (Mb) akizindua rasmi jarida hilo huku ukurasa wa mbele ukiwa umepambwa na picha yake sambamba na mahojiano maalum aliyoelezea mafanikio na changamoto mbalimbali alizopitia katika biashara hadi hapo alipofika. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni akishuhudia tukio hilo.
DSC_0425
DSC_0428
|It’s now official launched”…..Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji “MO” (Mb) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni wakifurahi pamoja baada ya uzinduzi rasmi wa jarida hilo.
DSC_0445
Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji “MO” (Mb) akikata keki maalum iliyoandaliwa kusindikiza uzinduzi huo.
DSC_0447
Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji “MO” (Mb) akimlisha kipande cha keki Mhariri Mtendaji wa jarida la IRIS Executive, Mike Mina.
DSC_0451
Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji “MO” (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa jarida la IRIS Executive. Kutoka kushoto ni Ofisa uhusiano na raslimaliwatu wa IRS Exexcutive, Beatrice Silayo, Jokha Sadiki, Ofisa Mtendaji Mkuu waKituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni, Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji “MO” (Mb),Mhariri Mtendaji wa jarida la IRIS Executive, Mike Mina, Meneja Masoko wa jarida la IRIS Executive, Alinda Henry na  Ofisa anayeshughulikia masuala ya Fedha wa jarida la IRIS Executive Bw. George Saltai.
DSC_0299
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) na Katibu wa Mbunge wa Singida mjini, Hassan Mazala (kulia) naye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa. Katikati ni Ofisa anayeshughulikia masuala ya Fedha wa jarida la IRIS Executive Bw. George Saltai.
DSC_0300
Picha juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa jarida la IRIS Executive na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
DSC_0317
DSC_0356
DSC_0303
Meneja Mkazi wa Shirika la Ndege la Rwanda,  Hafeez Balogun (kushoto) na Meneja Mauzo wa Shirika la Ndege la Rwanda, Dhruv Parmar (katikati) pamoja na Meneja Mkuu wa African Life Assurance, Bw. Wilson Mnzava (kulia) wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri kwenye halfa hiyo.
DSC_0394
Msaidiz wa Mh. Mohammed Dewji “MO” Nicole Cherry akipiga picha matukio mbalimbali kupitia simu yake ya kiganjani wakati wa hafla hiyo.
DSC_0461
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni akibadilishana mawazo na Meneja Mkazi wa Shirika la Ndege la Rwanda,  Hafeez Balogun (katikati) na Meneja Mauzo wa Shirika la Ndege la Rwanda, Dhruv Parmar (kushoto) kwenye sherehe za uzinduzi wa jarida hilo.
DSC_0482
Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (kulia) akibadilishana mawazo na Mhariri Mtendaji wa jarida la IRIS Executive, Mike Muna wakati wa uzinduzi wa jarida hilo.
DSC_0492
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni (wa pili kulia) katika picha na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa jarida la IRIS Executive ambalo kwa sasa liko mitaani na unaweza kujipatia nakala yako.
DSC_0464
Mbunifu wa Mavazi nchini Tanzania, Sheria Ngowi akisalimiana na Meneja Mkuu wa African Life Assurance, Bw. Wilson Mnzava wakati wa uzinduzi wa jarida hilo.
DSC_0452
Mkurugenzi Mtendaji wa Mikono Business Consult Deogratius Kilawe (kulia) akisalimiana na Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania, Sheria Ngowi kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa jarida la IRIS Executive uliofanyika usiku wa kuamkia leo.
DSC_0489
Mbunifu wa Mavazi nchini anayefanya vizuri katika soko la kimaifa Sheria Ngowi (kulia) akiwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko cha Sheria Ngowi Brand, Deogracious Kessy wakati wa uzinduzi wa jarida la IRIS Executive.

KAMA MADAWATI HATUNA::ONA NYUMBA ZILIZOJENGWA KWA MBAO FINLAND.....

Badhi ya nyumba za ghorofa zilizojengwa kutumia mbao katika jiji la LAHTI nchini Finland ambazo zilitembelewa na madiwani wa majiji sita ya Tanzania waliokuwa katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoratibiwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania.
Finland ni miongoni mwa nchi zenye maeneo makubwa ya misitu ya kupandwa dunaini, zaidi ya asilimia 80 ya eneo la nchi hiyo ni misitu na wenyewe wanasema nyumba zinazojengwa kwa kutumia mbao zina gharama nafuu kuliko kujenga kwa matofali au mawe.
Mkurugenzi wa jiji la LAHTI, Kari Porra akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa nyumba hizo za mbao kwa mratibu wa ziara hiyo Godfrey Nyamrunda kutoka taasisi ya Uongozi ya Tanzania, nyuma yao ni Meya wa jiji la Dar Esa Salaam Dk Didas Masabur

Upaja Wangu Ndio Silaha Yangu, Nikivaa Nguo Ndefu Sijiamini Kabisa Nakosa Confidence

Upaja Wangu Ndio Silaha Yangu, Nikivaa Nguo Ndefu Sijiamini Kabisa Nakosa Confidence

August 26, 2014
Admin 
Nimeona Nikuandikie Watu Wanipe Ushauri , Mimi ni Msichana Bado Mbichi Sana ila Tatizo langu ni Mavazi yaani Sijui inakuwaje kila nikitoka out ama Kwenda kazini nikivaa nguo ndefu sijiamini hata kidogo nakosa amani na hata furaha , ila siku nikiwa nimevaa nguo fupi basi najiamini si mchezo naweza kumface mtu yoyote , alafu napenda vile Kila mtu anavyoniangalia nikitembea with my High Heels..Je Nitakuwa nimeathirika kisaikologia kimavazi ama ni Kawaida hata wadada wengine inawakuta hivyo?

Monday, 25 August 2014

ONA KIM KARDASHIAN ALIVYOMTEGA USHER...


HUYU NDO MTU ALIONEKANA MREFU KULIKO WOTE DAR.....

NGONGOTI ADUWAZA WATU AKIKATIZA MITAA YA MWENGE, DAR

August 25, 2014
Ngongoti akikatiza mitaa akiwa katanguliwa na ‘mshikaji’ wake.
…Akipishana na jamaa aliyebeba viti.
…Akiwa katikati ya magari madogo.
....Akipita karibu na paa la nyumba.
KAMERA yetu imefanikiwa kumnasa Ngongoti aliyekuwa akikatisha maeneo ya Mwenge, jijini Dar na kuwakumbusha baadhi ya watu enzi za utoto wao ambapo wengi walionekana kuduwaa.

HII NDO SAIKOLOJIA YA WANAWAKE ILI KUMPATA MCHUMBA...

Saikolojia ya Wanawake Kuchagua Mwenza (Mchumba) Inachekesha Sana

  Monday, August 25, 2014 
Wanasaikolojia wakiongozwa na mwanasaikolojia Benedict Jones wamegundua kwamba, mwanamke akitaka kupima uzuri wa mwanaume ambaye angependa kuwa rafiki au mpenzi wake, hupenda kujua kama hata wanawake wenzie wanampenda kama yeye anavyompenda……..

Anavyozidi kuwaona wanawake wenzie wakitabasamu au kumchekea mwanaume huyo anapopita mbele yao ndivyo atakavyojua kwamba, huyo mwanaume ni mzuri.

Hali hii inafahamika kama copycat reflex na ni matokeo ya nadharia ya Darwin ya mambo ya mabadiliko ya maumbile ya viumbe, kwa mujibu wa wataalamu hao, yaweza kutumika pale ambapo mwanamke anakumbana na wanaume wengi wanaomtaka lakini anapata matatizo ya kumchagua yupi na kumwacha yupi.

Au akiona uchaguzi wa mwanaume bora utamchukulia muda wake mwingi na nguvu zake hujirahisishia kwa kuchukua uamuzi wa kuwaangalia wanawake wenzie wanavyomwona mchumba wake mtarajiwa. 

Uchunguzi huu hufanyika bila wanawake wenzie kujua kwa hiyo mwanaume anayeonekana kuchangamkiwa sana na wanawake wenzake kwa lengo la kumvuta ili awe mpenzi wake ndiye ambaye atapata uwezekano mkubwa wa kukubaliwa na mwanamke huyo.

PICHA YA LEO:kantanka group WANATENGENEZA NA NDEGE itaanza kuruka desemba





Hapo ikiwa katika hatua za awali za utengenezwaji ndege

samaki mkunje angali mbichi

PICHA ZINGINE ZA MAGARI KUTOKA GHANA YAKIWA TAYARI KWA KUUZWA...

PICHA NYINGINE ZA MAGARI YANAYOTENGENEZWA GHANA




TAZAMA PICHA YA MAGARI YANATENGENEZWA AFRIKA HUKO GHANA

HII NDO GARI ILIYOTENGENEZWA GHANA.....

Hii ni karakana/kiwanda cha magari ya huko ghana

Hapo gari likiunganishwa vitu.

kazi inaendelea



Gari ikiwa katika hatua za mwisho kutengenezwa

KARIBU MLIMA KILIMANJARO::WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO

WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO
 August 25, 2014
Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza mara baada ya kuwasili kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akigawa fulana maalum zenye nembo ya TANAPA na Real Madrid kwa mmoja wa wachezaji kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Erastus Lufungulo akitoa neno la ukaribisho kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid walipowasili kwa ziara fupi.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro
Wakongwe wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro.
Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakongwe wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro.
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

SIASA SI HASA:::USICHEZE VIBAYA NA SIASA....MAKONDA ROHO JUU JUU

Hali Ndani ya CCM ni Mbaya, Roho ya Makonda Inatafutwa Usiku na Mchana

Udaku Specially on Monday, August 25, 2014
Kwa mujibu wa nzi wetu anayecheza viunga vya Lumumba akitutiririshia habari zote mpaka mapigo ya mioyo ya akina Kinana, Nape na wana CCM wote walio juu ya maharamia wote, anatujuza kuwa huko CCM moto wake sio wa kitoto,

Makonda anatuhumiwa kumtusi Lowassa hadharani tena akivaa mwavuli wa UVCCM ilihali hana cheo chochote ndani ya Chama,

Baada ya matusi yale ya nguoni ambayo aliyaporomosha huyu dogo nikuwa mashitaka rasmi yalifikishwa kwenye kamati ya maadili na Lowassa,

Sheria ya CCM inasema kama mtu hayupo kwenye kikao husika cha mashitaka ni mwiko kujadiliwa,

Sasa siku ambayo tayari kamati kuu ilijipanga kumwajibisha (kumvua uanachama) kwenye kikao chake cha mwezi jana, Makonda alikimbilia Ufaransa akitoroshwa na Ridhiwan Kikwete na Bernard Membe kwa madai kuwa anakwenda kwenye semina ya masuala ya katiba,

Baada ya kutokuwepo kwenye kikao husika huvyo iliamuliwa suala hilo lisogezwe kwenye kikao kitakachofuata hasa hiki cha dharula juzi,

Kikao cha juzi tena wakati akiwa tayari kajulishwa kwa barua toka kwa katibu mkuu, Makonda tena alisafiri kwenda Ujerumani kwa madai ya kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake, safari hii Membe akihusika kuratibu na taarifa za kuaminika nikuwa hakwenda Ujerumani bali aliongozana na Membe kwenye ziara yake huko Mashariki ya Mbali ambako aliendelea kubaki huko hata baada ya Membe kurudi mpaka cc ilipomaliza kikao chake juzi,


Upande wa Lowasa wanaoonekana ndio wenye nguvu wameapa kuwa ni lazima waikate "roho" ya kisiasa ya Makonda kwa kuhakikisha anafukuzwa uanachama.

TATHIMINI YAKO:KUOLEWA NA MZUNGU NI SIFA KUBWA.

 
Lucy Komba akiwa na mpenzi wake wa mamtoni.