Saturday, 13 September 2014

Familia ya Steenkamp yapinga uamuzi

Familia ya Marehemu Reeva Steenkamp
Familia ya Reeva Steenkamp ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius imekasirishwa na uamuzi wa jaji wa kesi hiyo baada ya kumpata na hatia ya mauaji ya kutokusudia na kumuondoalea mashtaka ya mauaji.
June Steenkamp amesema kuwa mwanawe ambaye alikufa vibaya hakufanyiwa haki.
Amesema kuwa hakuamini kwamba jaji wa kesi hiyo alikubali ushahidi wa Oscar Pistorius kwamba alidhani bi Reeva Steenkamp alikuwa mtu ambaye alikuwa amevamia nyumba yao.
Hatahivyo mjombaake Pistorius alimshukuru jaji huyo kwa kumuondolea mashtaka ya mauaji mwanariadha huyo.
Oscar Pistorius ataendelea kuwa nje kwa dhamana hadi hukumu yake itakapotolewa mnamo mwezi ujao.

MPAMBANAJI:::HALIMA MDEE AWA MWENYEKITI MPYA BAWACHA

Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa (Bawacha),wakifungua shampeni kusherehekea ushindi wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (kushoto) baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo. (Picha na Francis Dande)
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bara), Hawa Mwaifunga akilia kwa furaha baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika juzi.
Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema wakiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (kulia) akipongezwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bara), Hawa Mwaifunga.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wake (Bara), Hawa Mwaifunga (kushoto) na  Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Hamida Abdallah.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema, Halima Mdee akizungumza baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Baraza hilo.

WATAHISIWA WENGI SANA::Mama Mzazi Wa Msanii Nay wa Mitego Ana Wasiwasi na Mwanae Kuwa Keli ni Freemason


Mama mzazi wa mkali wa bongofleva Nay wa Mitego ameongea kwa mara ya kwanza na millardayo.com na kusema ana wasiwasi na mwanae ambae hivi karibuni ametoa video mpya aliyoifanya nchini Kenya.
Amekiri kweli kwamba siku kadhaa zilizopita ilibidi amwite na kumuweka chini Nay wa Mitego akitaka amueleze kama ni kweli amejiunga na ‘freemason’ ambayo wengi wanaitafsiri kwamba ni dini ya kumwabudu shetani kitu ambacho kiliwahi kukanushwa na aliyewahi kuwa mmoja wa viongozi wa freemasons Tanzania.
Mama anasema alimketisha Nay chini baada ya video ya ‘Mr. Nay’ kutoka ambapo baadhi ya picha sio za kawaida mfano damu pamoja na alama zilizotumika ndani yake.

Amesema ‘Naitwa Matilda Mwaipopo ni mama mzazi wa Nay, kwakweli mwanangu namchukulia lakini sifa tu zinazokuja kama Nay kwenye magazeti, Nay freemason, watu wanakuja wananisimamisha…. mwanao Nay kweli? mbona tunasikia freemason? basi kichwa changu kinapagawa…. ‘
‘Nikiangalia miziki anayoifanya kama hii aliyoitoa juzi, jamani mwanangu anaambiwa freemason usikute kweli freemason, Nay wa Mitego nimemuita…. mwanangu vipi? ninayoambiwa ni ya kweli? Freemason wewe? mbona wimbo wako huu siuelewielewi?  ananiambia mama mimi sio freemason, namwambia hapana mwanangu hapana….. nasikia freemason watu wanatoaga hata wazazi sadaka’

‘Mimi ndio mama niliebakia baba yenu alifariki aliniacha ukiwa na miaka mitatu nimejitahidi kukulea mpaka leo…… unitoe sadaka mama yako kweli?????!!! Nay wa Mitego sana ni kucheka…… anaona tu mama kama anapagawa, lakini kwakweli mwanangu simuaminiamini miziki yake hii anayoifanya’

Friday, 12 September 2014

JINSI YA KUJITIBU UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Tumeangalia mfumo wa uzazi wa mwanaume kwa wakati uliopita lakini leo itapendeza zaidi kujua ni jinsi gani mwanaume anaweza kujitibu tatizo hilo hapohapo nyumbani.
Lakini kabla ya kujua jinsi ya kujitibu hapohapo nyumbani ni vizuri tukayatambua madhara ya upungufu wa nguvu za kiume.
MADHARA MAKUBWA NI YAPI?
Madhara makubwa ni kushindwa kushiriki vizuri tendo la ndoa
Kuwahi sana kufika kileleni
Kushindwa kuinuka kabisa
Kuinuka kwa muda mfupi sana
Kuinuka na kushiriki tendo lakini wakati wako kwenye tendo wanalegea na kushindwa kuendelea.
Kuathirika kisaikolojia
Ongezeko kubwa sana la usaliti ndani ya ndoa
Kushindwa kusababisha ujauzito (kwa sababu ya kushindwa kushiriki tendo vizuri).

VISABABISHI
Na ni vitu gani ambavyo husababisha upungufu wa nguvu za kiume kwa mwanaume, ni vizuri sana kuvijua ili uweze kuepukana navyo kwa haraka. Navyo ni;
Umri mkubwa kuanzia miaka 45 na kuendelea, uwezo hupungua taratibu.
Kujichua kwa muda mrefu
Kuugua kisukari (Diabetes)
Kuugua presha (High Blood Preasure)
Utumiaji ulevi. Wengi hudhani utumiaji wa vinywaji vikali sana ni dawa lakini hivyo vinywaji vinakufanya uwe tegemezi (addicted) na bila ya hivyo basi unakua huwezi tendo.
Uvutaji sigara kwani sigara ina sumu ambazo si rafiki kwa mfumo wa uzazi wa mwanaume.
Lishe  mbovu nayo huchangia sana tatizo hili.
VYAKULA RAFIKI
Kwa mwanaume vipo vyakula ambavyo ni rafiki sana kwa mfumo wake wa uzazi na vyakula hivyo au mimea hiyo ni kama;
Matumizi ya asali na tangawizi kwa wingi,
Matunda yenye njano nyingi, mfano, maembe
Matikiti maji na mbegu zake
Mbegu za maboga
 Matumizi ya samaki, mfano, pweza.
Kwa matibabu zaidi wasiliana nasi kwa hizo namba hapo juu ili kutatua tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na kujenga familia zilizo bora kwa Watanzania.

HIKI NDO KITUKO KINGINE ALICHOKIFANYA BALOTELI BAADA YA KUTUA LIVERPOOL

Mshambuliaji Mario Balotelli mwenye umri wa
miaka 24, aliyehamia Anfield kutoka AC Milan kwa
Pauni milioni 16 mwezi uliopita, jana alitolewa nje
katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Wolves baada ya
kuzozana na refa, Chris Foy.
Balotelli akielekea nje baada ya mzozo huo
Bahati nzuri, alizuiwa na mchezaji mwenzake, Kolo
Toure wakati Foy akizungumza naye kwenye
mchezo huo.
Chanzo cha mzozo huo ni baada ya Mtaliano huyo
kugongana na mchezaji wa Wolves. Baada ya
mzozo huo tu, Balotelli alitolewa nje mara moja.
Kolo Toure (kushoto) akimzuia Balotelli asiendelee
na mzozo

ELIMU YA MAHUSIANO::MMEGOMBANA? FUATA MBINU HIZI KURUDISHA MAPENZI

Kugombana ni jambo ambalo halikwepeki katika uhusiano wa kimapenzi. Upo ugomvi ambao ni wa kawaida na huisha kirahisi lakini upo ugomvi ambao huwa mkubwa na kama ukitokea na ukashindwa kujua nini cha kufanya kuweka mambo sawa, husababisha ufa kwenye penzi lenu.Leo tutazungumzia mambo muhimu ya kufanya inapotokea wewe na mpenzi wako mmeingia katika ugomvi mkubwa, mmetoleana maneno machafu au hata kupigana.
1. TAFAKARI CHANZO CHA TATIZO
Kuna usemi kwamba ukitaka kulitatua vizuri tatizo ni lazima kwanza ujue chanzo cha tatizo lenyewe. Ukishindwa kugundua chanzo cha tatizo, basi na wewe unakuwa sehemu ya tatizo.
Utashangaa kwamba wapenzi wengi hugombana na mambo kuwa makubwa kabisa kwa sababu ya vyanzo vidogo ambavyo walishindwa kuvigundua mapema na matokeo yake vikazaa matatizo mengine.
Mfano rahisi, chanzo kinaweza kuwa mpenzi wako amekupigia simu lakini ukashindwa kuipokea kwa muda muafaka. Atakapopiga kwa mara nyingine au mkikutana, usitegemee atakufurahia kwa sababu atahisi umemdharau kwa kutopokea simu yake.Endapo ukifanya makosa ya kushindwa kuliona kosa lako mapema na kushindwa kuomba radhi au kutoa maelezo yanayoeleweka kwa nini hukupokea simu, matokeo yake utamjibu vibaya, naye atakujibu vibaya na mwisho mtaishia kupigana au kuachana kabisa mkiwa mmeshatoka kabisa kwenye kosa la msingi.
Bila shaka msomaji wangu umeona jinsi chanzo kidogo kinavyoweza kusababisha tatizo kuwa kubwa. Ndoa nyingi au uhusiano unaofika mwisho huwa umesababishwa na mambo madogo ambayo yalishindwa kutafutiwa suluhu mapema.
Katika kila ugomvi unaotokea, jambo la kwanza jipe muda wa kutafakari chanzo kilichosababisha mkagombana. Wakati mwingine wewe ndiyo unaweza kuwa chanzo cha tatizo lakini kama ukiyajua makosa yako mapema na kukiri kisha kuomba radhi kwa mwenzio, utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kurudisha mapenzi kwa haraka.
2. MPE MUDA HASIRA ZIISHE
Kila binadamu ameumbwa akiwa na hasira na kwa bahati mbaya ni wachache wanaoweza kuzidhibiti hasira zao. Ni rahisi mtu kutukana, kupiga au kuharibu vitu akiwa na hasira.Baada ya kugombana, kila mmoja lazima atakuwa na hasira na njia pekee inayoweza kuepusha matatizo zaidi, ni kujipa muda na kumpa muda mwenzako ili hasira zipungue.
Kama mpo sebuleni na umetokea ugomvi, ni busara kwenda chumbani au nje mpaka hasira zako zikiisha. Ni makosa kulazimisha suluhu wakati kila mmoja akiwa na jazba kwani mtaishia pabaya zaidi.
Ukishaona hasira zako zimetulia na mwenzako naye ametulia, unaweza kuanzisha mada juu ya kilichosababisha mkagombana. Tumia lugha ya upole kwani endapo utakuwa ukifoka au kuzungumza kwa sauti ya juu, matokeo yake mtarudia tena kugombana.
3. MPE NAFASI YA KUZUNGUMZA
Huwezi kumuelewa mtu kabla hujampa nafasi ya kuzungumza na kumaliza kile alichokusudia kukisema. Endapo tatizo limetokea na upo kwenye hatua za kusaka suluhu, mpe mwenzako nafasi ya kueleza dukuduku lililopo ndani ya moyo wake.
Usimkatishe wala kumbishia chochote, muache aongee ulichomuudhi mpaka dukuduku lake liishe kisha na wewe jieleze kwa upole na sauti tulivu.
4. OMBA MSAMAHA
Hakuna silaha nzuri inayoweza kukusaidia kuushinda ugomvi wowote na kutuliza mambo kabla hayajawa mabaya kama kuomba msamaha. Neno ‘samahani’ ni dogo lakini lina maana kubwa kwa yule mtu anayelitoa na anayelipokea.
Hata kama unaona dhahiri kwamba kosa siyo lako, omba msamaha kwanza kisha baada ya hapo anza kumuelewesha mpenzi wako kwa upole. Lazima mwisho na yeye atayaona makosa yake na kukuomba msamaha, mtaweza kuepuka kuukuza ugomvi huo na kurudisha hisia za mapenzi.
5. USIWEKE KINYONGO
Endapo umeamua kuomba msamaha kwa mpenzi wako, au yeye amekuomba msamaha, samehe kwa dhati kutoka ndani ya moyo wako na sahau kile kilichotokea. Ni kosa kubwa kuweka kinyongo rohoni, yaani unamwambia kwamba umemsamehe wakati moyo wako bado una hasira naye. Ukisamehe kwa dhati, jifunze na kusahau kwani kusamehe kunaenda sambamba na kusahau.
Wazungu wanasema forgive and forget. Elewa kwamba mpenzi wako ni binadamu ambaye hajakamilika, wala si malaika.
Lazima atakuwa akikosea mara kwa mara, endapo utakuwa ukilimbikiza vinyongo, unafuga matatizo makubwa kwani siku nyingine akikukosea hata jambo dogo, utakumbushia na ya jana na juzi na mwisho ugomvi utakuwa mkubwa sana.

JITAMBUE:::SOMA SABABU TANO ZINAZOKUFANYA USIFANIKIWE KATIKA KAZI ZAKO


Leo katika JITAMBUE KWANZAtumeangazia katika sababu maalum zinazowakwamisha watu wengi wasifikie vilele vya mafanikio yao, sababu hizo ni;

(i)  KUKOSA MOTISHA.
      Mafanikio huja kwa kupenda kile unachofanya.Je, kazi unayofanya inakupa mateso? Kama umeshawahi kuwachunguza watu wenyemafanikio, basi utaona angalau wanakitu kimoja muhimu wanachokipenda na kukithamini katika kazi zao: wanapenda wanachokifanya na wanafanya wanachokipenda.Je, hili ni tatizo kwako? Kama jibu ni hapana, unaweza kuanza leo kutambua mateso uyapatayo kutokana na kazi yako. Hii takuwa ni njia sahihi ya kupata motisha wa mafanikio katika kazi yako.

(ii)  UKOSEFU WA IMANI.
        Imani ni uimara wa kujiamini mwenyewe, Mungu na wengine unaoweza kuwaamini. Jenga maono imara kwa kila jambo unalotaka kulikamilisha.Kufanya hivyo itakupa moyo wa kufanya kazi bila kurudishwa nyuma na mtu yeyote, kwani binadamu tupo wakati mwingine ili kurudishana nyuma kwa kuona wivu na chuki katika mafanikio ya wenzetu.

(iii)  HOFU YA KUSHINDWA.
         Hofu ya kushindwa haipo, wala hofu ya mafanikio haina nafasi.Hofu husimama kama shahidi wa uongo, ukionekana kama ukweli. Hofu ni udanganyifu unaojitokeza unapotaka kufanya jambo fulani, kweli nivigumu kupambana na hofu.Lakini njia sahihi ya kuikabili hofu ni kuwasoma watu waliokwisha jambo fulani linaloendana na jambo unalohitaji kulifanya. Binadamu tumeumbwa sawa, ukiamini kuwa unauwezo hakika utaweza.

(iv)  KUTOKUWA NA MIKAKATI.
        Unapotaka kufanya biashara yenyekuleta mafanikio makubwa, ni lazima uwe na washauri wazuri.Huhitaji kupoteza muda, pesa na nguvu zako, washauri ni watu watakao kupatia mikakati madhubuti itakayokupatia moyo katika kuanzisha biashara yako.Chagua mtu yeyote anayekuvutia katika biashara, jaribu kuchunguza anafanyavipi kazi, alianzeje, hakika utafika katika biashara yako.

(v)  VIKWAZO VYA KIIMANI.
       Mara nyingi tumekuwa na vikwazo vya kiimani kuhusu kile tunachohitaji kukipata.Kwa mfano utakuwa unahitaji kufikia malengo yako lakini lakini kitu kinakwambia "hapana, siikwaajili yako, huwezi kufanya hivi" haya mawazo huchafua malengo yetu na maisha yetu.Njia pekee ya kushinda hali hii ni kusema neno "HAPANA!" mara hali hii inapotokea. Weka akilini kuwa wewe ni mtu kama watu wengine wanaofanikiwa maishani, na tambua kabisha kuwa kusudi la Mungu kukuweka wewe hai ni makusudi makuwa ya kukufanya ujiamini na umuombe kwa kila jambo.

Hivyo ni baadhi ya vitu muhimu ambavyo watu wengi wanasahau kuzingatia katika shughuli zao za kila siku.Hakika ukifuata vitu hivyo, utafanikiwa kwani wewe ni mtu muhimu sana katika jamii inayokuzunguka.

UWAJIBIKAJI:::STEVE NYERERE AJIUZULU URAIS BONGO MOVIE UNITY

NAYE ALIKUWA RAIS...

Aliyekuwa Rais wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steve Nyerere.
Rais wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' ametangaza kujiuzulu cheo hicho kupitia ukurasa wake wa instagram. Amedai kuna mpango mbaya dhidi yake hivyo akaona bora ajiengue pasipo kufafanua zaidi.

HABARI NA PICHA:::HITILAFU YA UMEME ILIVYOSABABISHA MOTO MTAMBANI

Wananchi wakisaidiana kuokoa mali za Msikiti wa Mtambani mara baada ya kushika moto uliowahi kuzimwa.
Kikosi cha zimamoto kikiwa eneo la tukio kutoa msaada.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa eneo hilo la tukio.
(PICHA ZOTE NA DAR ES SALAAM YETU BLOG)

(Picha hii ni wakati msikiti huo ulipoungua mara ya kwanza Agosti 13, mwaka huu)
MSIKITI wa Mtambani uliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam umeungua tena kwa moto leo mchana. Hii ni mara ya pili msikiti huo kuungua kwa moto baada ya ile ya awali ya Agosti 13 mwaka huu. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.

VIVUTIO::hawa ndio mastaa wengine wa Marekani walioitembelea Tanzania.

Screen Shot 2014-09-12 at 1.56.17 AM 
Siku hizi stori za mastaa wa dunia kuja kuitembelea Tanzania sio moja wala mbili manake wamekua wakija wengi tu na hawaachi kuipa nchi hii matangazo ya bure kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Screen Shot 2014-09-12 at 1.32.18 AM 
Mastaa wengine waliotua kwenye ardhi ya Jakaya time hii ni mwigizaji staa wa Marekani Gabrielle Union na mumewe Dwyane Wade mcheza kikapu wa Miami heat ambapo wameifanya Serengeti Tanzania kuwa sehemu nyingine waliyoitembelea duniani wakiwa kwenye honeymoon yao.
Screen Shot 2014-09-12 at 1.32.25 AM 
Gabrielle ana wafuasi zaidi ya milioni mbili na laki tatu kwenye page yake ya insta alikopost hizi picha za Tanzania.

MIMI MGENI:::WATANZANIA WATAKIWA KUTODANYWA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA



jumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vyama vya Siasa vinavyounda TCD, Mhe. John Cheyo.
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.

 MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD Mhe. John Cheyo amewataka Watanzania kutodanganywa kuhusiana na mchakato mzima wa kusaka Katiba Mpya.
 
Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe. Cheyo wakati alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha asubuhi cha Jambo kinachorushwa na Televisheni ya Shirika la Habari Tanzania (TBC).
 
Mhe. Cheyo amesema kuwa ni vema viongozi kuacha kusema uwogo na kuwa waungwana katika mchakato wa kutafuta Katiba Mpya kwani si vema kuitakia Tanzania mabaya bali ni kutaka mchakato huo wa Katiba uendelee kwa amani.
 
Ameongeza kuwa Taifa la Tanzania linahitaji kuwa Taifa lenye nguvu kwani amani haiwezu kuwekewa thamani kwa vurugu, hivyo ametaka amani iliyopo nchini ilindwe na kuepuka kudanganywa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na nchi.
 
Mhe. Cheyo ameshangazwa kwa kitendo cha viongozi wa UKAWA kutoweka ajenda ya kurudi ndani ya Bunge hilo wala kuzungumzia kuhusu suala hilo la kurudi ndani, bali wamekuwa wakitaka wajumbe wengine walioko ndani watoke kwa kusema kuwa bunge hilo sio halali.
 
“Nawashangaa UKAWA kwa kutoweka ajenda ya kurudi ndani ya Bunge hili Maalum la Katiba na badala yake wao wanaweka ajenda ya kutoka ndani ya bunge hili tena kwa nguvu”, alisema Mhe. Cheyo.
 
Aidha, Mhe. Cheyo amewataka vijana nchini wawe na mshikamano na kuepuka kudanganywa na viongozi kwa kuambiwa mambo yenye uwongo huku akisisitiza kuwa Rais aliyeko sasa hivi ana nia njema ya kuipatia nchi Katiba iliyo bora na yenye kumfaa kila Mtanzania.
 
“Vijana achene kuvunjika miguu yenu bure, achene kukimbia kimbia barabarani huku mkilishwa maneno yenye uongo kuhusiana na mchakato huu wa Katiba, vunjikeni miguu kwa kufanya kazi kwa bidiii na sio kusikiliza uwongo”, alisema Mhe. Cheyo.
Akizungumzia kuhusu TCD, Mhe. Cheyo amefafanua kuwa TCD ni Jukwaa la majadiliano kwa ajili ya maridhiano na mapatano pale panapokuwa na tofauti kati ya vyama vya siasa.
 
“TCD ni Jukwaa kwa ajili ya kufanya majadiliano na si vinginevyo, hii ni meza ya maridhiano na nawaambia kuwa huko mnapokwenda ni kuchepuka, rudini ndani kwenye njia kuu”, alisisitiza Mhe. Cheyo.
 
Naye mjumbe wa Kamati namba Sita ya Bunge Malaam la Katiba Mhe. Steven Wasira amewaasa Watanzania kwa kusema kuwa, watu wanaosema kuwa Bunge limenyofoa baadhi ya mambo muhimu yanayohusu wananchi ni waongo na wenye nia ya kupotosha Umma wa Tanzania.
 
“Kuna watu wanasema kuwa Bunge Maalum la Katiba limenyofoa baadhi ya mambo muhimu yanayohusu wananchi huo ni uwongo, ni mambo gani hayo yaliyonyofolewa? kwasababu kuna mambo mengi yameongezwa na kuboreshwa katika mapendekezo kwa ajili ya makundi mbalimbali ndani ya hiyo Rasimu”, alisema Mhe. Wasira.
 
Mhe. Wasira ameongeza kuwa katika Bunge hilo kuna Ibara ya Rasimu ya Katiba na sio ibara za CCM, amewataka Watanzania nchini wafanya uchunguzi na kusikiliza kwa kuchambua ili kupata ukweli wa hayo.
 
“Sisi tuko tayari kuvaana na viopngozi wowote kwani tunataka Watanzania wote waamini shughuli zifanywazo ndani ya bunge hili na waepuke kudanganywa”, alisema Mhe. Wasira.
 
-MWISHO-

IGA UFE::Hawa Ndio Watu 10 walioshindwa chuo na kuleta mabadiliko makubwa duniani


Image result for Steve jobs
1. STEVE JOBS
Inawezekana komputa za Mac na bidhaa nyinginezo kama iPhone zisingekuwepo kama Steve Jobs angebakia chuo.
2. Bill Gates
bill-gates-jpg
Moja wa watu walioacha chuo Harvard na wamefanikiwa na ni tajiri mkubwa duniani. Mwanzilishi wa Microsoft. Kauli aliyoitoa kwenye mahafali pale Harvard mwaka 2007 alisema ” Mimi ni mshawishi mbaya ndio maana mmeniita niongee wakati wa mahafali. Ningeongea wakati wa kuanza masomo yenu ni wachache sana mngekuwepo hapa.”
3.Frank Lloyd Wright
Mbunifu mkubwa wa vyuo vingi marekani lakini hajawahi kuhudhuRia hata kimoja. Ingawa Frank Lloyd Wright alichaguliwa kwenda chuo cha  Wisconsin-Madison mwaka 1886, lakini aliacha baada ya mwaka mmoja.
4. Buckminster Fuller
Bwana Huyu alifukuzwa Harvard mara mbili lakini ni mtu ambaye amefanikiwa sana na kuleta mawazo mapya katika ulimwengu huu. “He was expelled from Harvard twice: first for spending all his money partying with a vaudeville troupe, and then, after having been readmitted, for his “irresponsibility and lack of interest.”
5. James Cameron
Muongozaji maarufu wa filamu za Hollywood aliyetengeneza filamu nyingi za kubuni na za kisayansi na zenye gharama kubwa zikiwemo Titanic na Avatar.
6. Mark Zuckerberg
Mark Zuckerberg
Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook na aliyekuwa mwanafunzi wa Harvard. Baada ya Facebook kuanza kupata umaarufu aliamua kuacha chuo.
7. Tom Hanks
Mwigizaji maarufu aliyeamua kuacha chuo Sacramento State na kujiunga na Great Lakes Theater Festival kule Cleveland, Ohio. Huko akajifunza vitu vingi kumfikisha kuwa moja ya waigizaji na watengeneza filamu maarufu huko Hollywood.
8. Harrison Ford
Jamaa hut=yu aliacha chuo pale Ripon College siku chache kabla ya kumaliza. Ni moja ya watu waliofanya vitu vikubwa kwenye filamu za Star wars miaka 1977.
9. Lady Gaga
Lady-Gaga-HD-Pics-3
Kabla ya kuwa  Gaga, alikuwa anaitwa  Germanotta. alizaliwa na  Stefani Joanne Angelina Germanotta, msanii ambaye kwa sasa anaitwa   Lady Gaga alianza kusoma New York University’s Tisch,  Shule ya Usanii na baada ya hapo aliacha chuo baada ya mwaka mmoja na kuanza uimbaji wake pale  New York club na kuweza kusaini mkataba wake na Interscope Records akiwa na miaka hiyo hiyo 20.
10. Tiger Woods
tiger-woods
Mtu maarufu katika mchezo wa golf, baada ya miaka miwili aliacha kusomea uchumi pale Chuo cha  Stanfold, kwa sasa analipwa zaidi ya dola milioni 100 kwa mwaka.
Chanzo cha habari (Time)
Kwa wasomaji wetu sijasema uache chuo ila fikiria kwa kina utaleta tofauti gani kwa kile unachofanya, na je mafanikio yako umelenga kwenye nini? Je unaweza KUjifunza kitu gani kutoka kwa hawa watu?

HAKUNA FOLENI HUKO::WEMA, DIAMOND, AUNT WANATAJWA KWENYE MICHEPUKO HATARI!

Stori: Shakoor Jongo
Ni tamaa ya ngono au ni nini? Hivyo ndivyo unavyoweza kujiuliza baada ya kubainika kwamba mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel Grayson wanatajwa kwenye mchepuko hatari wa kuzungukana kimalovee, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.
Mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel wakiwa katika picha ya pamoja.
KILA KUKICHA
Ishu hiyo imebumburuka baada ya hivi karibuni mastaa kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha kuhusiana na mambo yao hayo.
AUNT NA MOZE IYOBO
Duru za kihabari zinaonesha kwamba hivi karibuni mwigizaji Aunt, bila ya kupepesa macho huku akijua dhahiri kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte alifungua kinywa na kuapa kuwa hawezi kuachana na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ ambaye ni densa wa Diamond.
Aunt alitamka maneno hayo akijua fika kuwa Moze Iyobo ni mume wa mwanamke aitwaye Mwengy ambapo wanaishi Mbagala jijini Dar, wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja.
Mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ akiwa na ‘Diamond Platnumz’.
AUNT KIOO CHA JAMII?
“Dah! Natambua kuwa msanii ni kioo cha jamii lakini si kwa Aunt, hana hadhi ya kuitwa kioo cha jamii kutokana na tabia yake ya kuchepuka wakati ni mwanandoa,” alidai mmoja wa watu wake wa karibu.
Mdau mwingine wa sanaa za nyumbani aliyejitambulisha kwa jina la Said, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, alimshangaa Aunt kukiri hadharani kuwa ana uhusiano usiofaa na Moze Iyobo ambaye ni shemeji wa Wema kwa Diamond na yeye (Aunt) ni shosti wa Wema.
Alisema kwamba, kwa hadhi yake, Aunt hakupaswa kutoa kauli hiyo ili watu waendelee na minong’ono kuhusiana na yeye (Aunt) tofauti na alivyofunguka bila aibu ukizingatia ni mke wa mtu.
“Unajua kwa nini nasema Aunt anajidhalilisha au anawadhalilisha wanawake wenzake ni pale anapokiri kuwa ndoa yake ipo tena bado anampenda mumewe huku anakuja kusema kuwa anampenda Moze Iyobo, huo kama siyo mchepuko ni nini?” alihoji Said.
‘Moze Iyobo’ akiwa na familia yake.
WEMA NA DIAMOND
Uchunguzi ulionesha kwamba, huku wakijua kila kitu waliwaruhusu Ahmed Hashim ‘Petit Man’ (Toto ya Wema) na Esma Platnumz ‘kuchepuka’ huku Petit akiwa ni shemeji wa Diamond kwa Wema.
Pia Diamond alifanya ‘misteki’ kumuacha mdogo wake, Esma ‘kuruka’ na Petit kwa kuwa ni shemeji yake.
KAJALA ANAINGIAJE?
Ilibainika pia kwamba Petit aliwahi kuchepuka na mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ ambaye ni mke wa mtu, Faraji Agostino aliyeko gerezani na hilo likiwa wazi hata kwa hao akina Wema na Diamond.
“Hebu jaribu kuangalia huo mzunguko na mkanganyiko uliopo hapo. Yaani ni aibu tosha,” alisema mdau mwingine kuhusiana na ishu hiyo.
'Petit Man' akipozi kimahaba na Kajala Masanja, 'K'.
STEVE NYERERE AANIKA AIBU YAO
Hivi karibuni kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ aliwavaa mastaa hao na kuanika aibu yao huku akimshutumu Aunt ambaye alifika maeneo hayo akiwa ameongozana na mpenzi wake huyo wa sasa, Moze Iyobo.
Steve alisikika akimwambia Aunt kuwa hamtendei haki Moze Iyobo na anamnyima uhuru mkubwa kutokana na umri wake ambao anaweza hata kumzaa.
“Unajua wewe Aunt unastahili kuwa na mtoto mkubwa mwenye umri usiokuwa tofauti na huyu Moze Iyobo.“Hivi kwa nini unajidhalilisha kiasi hicho kwani wazee wenzako hujawaona hadi kumbemenda mtoto wa watu?” alisika Steve akimpasha Aunt kwa sauti ya juu.
'Petit Man' yule yule akiwa na dada yake 'Diamond Platinum', Esma.
NI SHARTI LA DIAMOND KWA WEMA
Akiendelea kumpasha Aunt, jamaa huyo alikwenda mbali zaidi pale alipomwambia Aunt kwamba anahisi kuwa uhusiano wake na Moze Iyobo ni sharti kutoka kwa Diamond kumpa Wema ili alifanyie kazi na kumwambia kuwa ahakikishe yeye (Aunt) anakuwa na Moze na Petit Man amuoe Esma.
“Unajua hivi karibuni baada ya Diamond kuandika yale maneno katika Mtandao  wa Instagram, nilisikia waliachana sasa naona Diamond alimwambia Wema kama unataka nikurudie ahakikishe kuwa wewe Aunt unakuwa na huyu mtoto (Moze Iyobo) halafu yule dogo mwenye rasta sijui mnamuita Petit Man ahakikishe anamuoa Esma dada yake Diamond,” alisema Steve.
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akifafanua jambo.
AUNT AWA MBOGO
Baada ya Steve kutoa dukuduku lake mwigizaji huyo aligeuka mbogo na kumwambia Steve kuwa amuache kwa raha zake kwani anampenda Moze Iyobo hata aseme nini hawezi kumuacha.
“Hata uongee nini Steve, siwezi kumuacha mpenzi wangu, nampenda sana na hayo masharti unayoyasema kuwa ameyatoa Diamond unayajua wewe, niachie nile raha zangu na Moze wangu,” alisema Aunt akimwangushia Moze Iyobo bonge la ‘kisi’.
KUTOKA IJUMAA
Ni kweli wasanii ni kioo cha jamii lakini kwa kuwa wamekuwa ‘vichwa ngumu’ kutenda yale yanayowafanya kuwa vioo vya jamii ni vema jamii yenyewe ikachuja mema na kuyachukua kisha kuwaacha wabaki na hayo machafu yao.

Mwanaume apata hisia za ujauzito

Harry Ashby ameripotiwa kuwa na dalili za ujauzito kama mchumba wake
Harry Ashby ni mwanaume wa kwanza nchini Birmingham kupata ruhusa ya kupumzika nyumbani baada ya kusumbuliwa na homa mithili ya mwanamke mja mzito.
Amekuwa akipatwa na homa za vipindi hasa nyakati za asubuhi baada ya mchumba wake aitwae Charlotte kuwa mjamzito, mtandao wa Itv news umeeleza.
Habari zinasema mwanaume huyo mwenye miaka 29 anayefanya kazi ya ulinzi ,amesema ameongezeka uzito na tumbo limekua mithili ya aliye mjamzito na kudai kuwa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo na cha ajabu amekuwa na hamu ya baadhi ya vyakula.
Harry ameripotiwa kuwa na dalili za kuwa mja mzito miezi miwili baada ya kubaini kuwa mchumba wake ni mjamzito.
Harry amekuwa akipatiwa dawa na inasemekana anaweza kudai mafao wakati akiwa katika mapumziko hayo.

KWANI BONGO HAMNA HIYO??Mfungwa apatikana na simu mwilini Kenya

Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ya Kenya imekuwa kero kubwa kwa maafisa wa magereza
Kwa baadhi ya watu simu ya mkononi ni kifaa tu cha mawasIliano ilihali kwa wengine ni kifa ambacho kinaweza kukuweka katika hali ya kufa kupona.
Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake. Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini mwake kupitia sehemu yake nyeti ya nyuma.
Mfungwa huyo wa gereza la King'ong'o katika jimbo la Nyeri alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo ambazo alikuwa amezificha mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma.
 Mfungwa ambaye alitolewa simu mwilini kwa kufanyiwa upasuaji 
 
Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.
Wamekuwa kwa miaka mingi wakijaribu kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika magereza nchini Kenya kinyume na sheria za magereza.
Maafisa wa magereza wanakiri kwamba wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.

SOMO LA LEO::SITTA awapa somo Viongozi wanaojiita UKAWA.


 
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongoza bunge hilo.
 
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
 MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amewaadaa baadhi ya viongozi wanaojiita UKAWA kwa taarifa yao ya kutaka kumfikisha Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa kwa kuendeleza mchakato huo wa Katiba.
 
Kauli hiyo imetolewa leo 12 Septemba, 2014 mjini Dodoma na Mhe. Sitta kufuatia baadhi ya viongozi hao, kudai kuwa watampeleka katika mahakama hiyo.
 
Mhe. Sitta ameeleza kuwa baadhi ya viongozi wa kundi hilo kuwa wanakipaji kikubwa cha uigizaji huku akifafanua kuwa wakati walipokuwa Bungeni wakati wa mchakato wa kupiga kura za siri, viongozi wa kundi hilo walizifanya kura hizo kuwa wazi na baadaye kuja na kauli kuwa Bunge Maalum la Katiba linaloendelea sasa sio halali lihairishwe.
 
“Juzi Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana nao mara mbili kwa muda wa saa Saba na katika kukutana huko wakafikia maafikiano, lakini siku moja baadaye wao wamekana yote waliyokubaliana hapa mjini Dodoma, kwa hiyo ni vyema wananchi wakawapima hawa watu”, alisema Mhe. Sitta.
 
Aidha, Mhe. Sitta aliasa kwa kusema kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kujua kuwa mchakato wa bunge Maalum la Katiba sio jambo la mzaha na wao hawapo hapo bungeni kwa mzaha mzaha.
 
“Mimi nawaambia kuwa hapo mwakani watakaposhindwa uchaguzi basi warejee katika fani zao ambazo Mwenyezi Mungu kawajalia”, alisema Mhe. Sitta.

MWANADEMOKRASIA WA LEO::Picha aliyoiweka Rais Kikwete twitter baada ya kukutana na Wapinzani na alichoandika?

Screen Shot 2014-09-12 at 2.02.33 AM 
Baada ya kukutana na viongozi wa vyamba mbalimbali vya upinzani Tanzania na kuzungumzia ishu ya bunge la katiba, iliamuliwa kwamba katiba ya zamani ndio itakayotumika kwenye uchaguzi mkuu ujao ila itafanyiwa marekebisho.
Kwenye ukurasa wake wa twitter President JK ambae alikua hajaandika chochote toka Aug 6 2014, aliweka hiyo picha hapo juu ikimuonyesha kwenye mkutano na viongozi hao na kuandika >> Mazungumzo na Wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Dodoma, Septemba 8, 2014. Demokrasia ni majadiliano
Screen Shot 2014-09-12 at 2.10.10 AM

KUTOKA BONDENI:::OSCAR PISTORIUS HATIANI KWA KUUA BILA KUKUSUDIA


Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius.
MWANARIADHA mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa bahati mbaya.

Oscar Pistorius akisikiliza hukumu yake.
Akitoa uamuzi wake, Jaji Thokozile Masipaa alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa choo akiwa katika hali ya mshtuko akidhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Baba mzazi wa Oscar, Henke Pistorius akifuatilia kwa makini hukumu ya kijana wake.
Alisema kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp na kutekeleza mauaji hayo kwa kusudi.

Wanafamilia kutoka uoande wa marehemu Reeva wakiwa na simanzi wakati wa hukumu hiyo.
Pia alipatikana na hatia ya kosa la kutumia silaha yake visivyo alipokwenda mgahawani.
Adhabu yake itatolewa Oktoba 13 mwaka huu.
Jaji Thokozile Masipa alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya.
Dada wa Pistorius, Aimee (katikati) akisikiliza hukumu ya kaka yake.
(CREDIT: BBC)

Ex-Wife wa Prezzo Afunguka kuhusu Prezzo, Kumbe Prezzo si Lolote wala Chochote, Jisomee Hapa

Mwanamama mmoja ajulikanaye kama DAISY KIPLAGAT ambae amejitambulisha kuwa yeye ni Baby Mama wa rapper kutoka nchini Kenya Prezidaa PREZZO, aliingia kwenye group hilo na kuanza kumwaga radhi kuhusiana na msanii huyo kuwa hana ushirikiano kabisa katika kulea mtoto ambae amezaa na mwanamama huyo. Daisy aliongeza kuwa hataki chochote kutoka kwa rapper huyo ila kinachomboa ni pale jinsi msanii huyo ambae hajawasiliana na mtoto wao huyo wa kike tokea akiwa na miaka 2 lakini anaendelea kujitamba kuwa ana mtoto wakati hajawahi kutoa hata senti moja kusaidia kulea mtoto huyo.

“He goes around on TV and since he is able to hold a mic or have fake written interviews he is always claiming to be taking his daughter to the best school in Kenya and that she is her princess spoils her rotten. He has never paid her fees never paid any dime for her up keep all this is my sweat and my blessed parents and family support. I don’t need to communicate with him but I wanted to have this space to let you all know that this guy instead chooses to go around with women and lie to them how rich he is and yet he doesn’t have anything and stays at his mum’s house. So when you all hear how he does and loves his daughter please don’t be fooled,” – Daisy Kiplagat.