Friday 12 September 2014

IGA UFE::Hawa Ndio Watu 10 walioshindwa chuo na kuleta mabadiliko makubwa duniani


Image result for Steve jobs
1. STEVE JOBS
Inawezekana komputa za Mac na bidhaa nyinginezo kama iPhone zisingekuwepo kama Steve Jobs angebakia chuo.
2. Bill Gates
bill-gates-jpg
Moja wa watu walioacha chuo Harvard na wamefanikiwa na ni tajiri mkubwa duniani. Mwanzilishi wa Microsoft. Kauli aliyoitoa kwenye mahafali pale Harvard mwaka 2007 alisema ” Mimi ni mshawishi mbaya ndio maana mmeniita niongee wakati wa mahafali. Ningeongea wakati wa kuanza masomo yenu ni wachache sana mngekuwepo hapa.”
3.Frank Lloyd Wright
Mbunifu mkubwa wa vyuo vingi marekani lakini hajawahi kuhudhuRia hata kimoja. Ingawa Frank Lloyd Wright alichaguliwa kwenda chuo cha  Wisconsin-Madison mwaka 1886, lakini aliacha baada ya mwaka mmoja.
4. Buckminster Fuller
Bwana Huyu alifukuzwa Harvard mara mbili lakini ni mtu ambaye amefanikiwa sana na kuleta mawazo mapya katika ulimwengu huu. “He was expelled from Harvard twice: first for spending all his money partying with a vaudeville troupe, and then, after having been readmitted, for his “irresponsibility and lack of interest.”
5. James Cameron
Muongozaji maarufu wa filamu za Hollywood aliyetengeneza filamu nyingi za kubuni na za kisayansi na zenye gharama kubwa zikiwemo Titanic na Avatar.
6. Mark Zuckerberg
Mark Zuckerberg
Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook na aliyekuwa mwanafunzi wa Harvard. Baada ya Facebook kuanza kupata umaarufu aliamua kuacha chuo.
7. Tom Hanks
Mwigizaji maarufu aliyeamua kuacha chuo Sacramento State na kujiunga na Great Lakes Theater Festival kule Cleveland, Ohio. Huko akajifunza vitu vingi kumfikisha kuwa moja ya waigizaji na watengeneza filamu maarufu huko Hollywood.
8. Harrison Ford
Jamaa hut=yu aliacha chuo pale Ripon College siku chache kabla ya kumaliza. Ni moja ya watu waliofanya vitu vikubwa kwenye filamu za Star wars miaka 1977.
9. Lady Gaga
Lady-Gaga-HD-Pics-3
Kabla ya kuwa  Gaga, alikuwa anaitwa  Germanotta. alizaliwa na  Stefani Joanne Angelina Germanotta, msanii ambaye kwa sasa anaitwa   Lady Gaga alianza kusoma New York University’s Tisch,  Shule ya Usanii na baada ya hapo aliacha chuo baada ya mwaka mmoja na kuanza uimbaji wake pale  New York club na kuweza kusaini mkataba wake na Interscope Records akiwa na miaka hiyo hiyo 20.
10. Tiger Woods
tiger-woods
Mtu maarufu katika mchezo wa golf, baada ya miaka miwili aliacha kusomea uchumi pale Chuo cha  Stanfold, kwa sasa analipwa zaidi ya dola milioni 100 kwa mwaka.
Chanzo cha habari (Time)
Kwa wasomaji wetu sijasema uache chuo ila fikiria kwa kina utaleta tofauti gani kwa kile unachofanya, na je mafanikio yako umelenga kwenye nini? Je unaweza KUjifunza kitu gani kutoka kwa hawa watu?

No comments:

Post a Comment