Mwenyekiti wa Chama cha walimu CWT Mkoa
wa Iringa Mwalimu Stanslaus Mhongole, akisikiliza jambo katika mkutano
wa kutoa tamko baina ya uongozi wa CWT na baadhi ya wanahabari mkoani
Iringa.
Katibu wa CWT Mkoa wa Iringa Mshamu
Ally Mshamu akiwa katika mkutano baina ya baadhi ya wanahabari mkoani
Iringa na uongozi wa CWT - wakati wakitoa tamko.
Baadhi ya viongozi wa CWT mkoa wa
Irinbga wakisikiliza jambo kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati
wa utoaji wa tamko.
Frenk Leonard- Mwandishi wa habari wa
gazeti la Habari leo na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari
mkoani Iringa akiwa katika mkutano huo wa CWT.
Geofrey Nyang'olo- mwandishi wa habari
wa gazeti la Mwananchi akiwajibika katika mkutano huo wa CWT.
Heriety mwandishi na mtangazaji wa kituo
cha redio County fm akisikiliza jambo kutoka kwa viongozi wa CWT mkoa
wa iringa.
Yohana Mgaya mtangazaji na mwandishi wa
habari wa kituo cha redio Furaha akiwa kazini katika mkutano huo.
Victory Meena mtangazaji na mwandishi
wa habari wa kituo cha redio Nuru fm akiwajibika kazini.
Eliasa Ally mwandishi wa habari wa
gazeti la Majira akifuatilia jambo katika mkutano huo baina ya viongozi
wa CWT na wanahabari.
Silvanus Kigomba mwandishi wa habari wa
Televisheni ya ITV na radio One, akiwa kazini katika mkutano huo wa
CWT.
Yuvenary Kimario mwandishi wa habari wa kituo cha radio Country fm na mwakirishi wa gazeti la Nipashe. akiwa kazini
CHAMA cha walimu
Tanzania- CWT mkoa wa Iringa kimetoa siku 14 kwa Serikali mkoani humo,
iwe imelipa
madeni yote inayodaiwa na walimu wake–
huku kikitishia kutofanyakazi kuanzia Septembe
15 endapo agizo hilo halitatekelezwa.
CWT imesema
kamwe haiwezi kuendelea kuifumbia macho serikali, huku walimu wake
wakiishi
maisha duni na yenye kukatisha tamaa, na mbaya zaidi kikilalamikia
punguzo la fedha
za mifuko ya jamii, ambazo huwasaidia watumishi pindi wanapostaafu.
Akisoma tamko
hilo mbele ya baadhi ya waandishi wa habari mkoani Iringa – Mwalimu
Stanslaus Muhongole
ambaye ni mwenyekiti wa CWT mkoa wa Iringa amesema…
“Chama cha Walimu
Mkoa wa Iringa kinaunga mkono Tamko la Chama makao makuu (CWT) na chama
cha
wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) kwa tamko lao
walilolitoa kwa pamoja katika kupinga mpango wa serikali wa kupunguza
Mafao ya
wastaafu kupitia Mifuko ya hifadhi ya jamii.
Muhongole amesema
wao kama walio wa mkoa wa Iringa wanasisitiza kuwa mpango huo wa
serikali hauna
nia njema kwa maendeleo ya nchi, hasa kwa walimu ambao wamekubali
kulipwa
mishahara midogo isiyokidhi mahitaji.
Amesema licha ya
walimu kuwa na mishahara duni lakini wamekubali kukatwa sehemu ya
mishahara
hiyo na kuiwekeza katika mifuko ya hifadhi ya jamiiili iwe na manufaa
pindi
wanapostaafu.
…..“Chakushangaza
serikali badala ya kuboresha mafao ya walimu ndani ya mifuko hiyo, tena
inashiriki kuchukua fedha kwenye mifuko yetu kwa ajili ya kuendeshea
shughuli
zake na hivyo kuwaacha walengwa wa mifuko wakiambulia fedha kiduchu
tofauti na
hali halisi ya uwekezaji,” amesema.
Mhongole amesema
Wizara ya kazi na ajira kwa kushirikiana na Mamlaka ya mifuko ya hifadhi
ya jamii
(SSRA) inadiriki kuandaa mpango wa kupunguza mafao ya wanachama wastaafu
wa
mifuko hiyo ya pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) na watumishi wa
serikali
za mitaa (LAPF) ili kuibeba Serikali dhidi ya madeni inayodaiwa na
mifuko.
Amesema mpaka
sasa Serikali inadaiwa takribani shilingi Tilioni 7, Bilioni 134,
Milioni 300
ilizokopa kwenye mifuko hiyo ambayo watumishi hukatwa mishahara yao kwa
lengo
la kuhifadhi kwa matumizi wakati wanapostaafu.
Akitaja mifuko na
kiwango cha fedha zilizochukuliwa na serikali, amesema...
Mfuko wa PSPF
inadai shilingi 4, 827, 800, 000, 000/=
Mfuko wa LAPF unadai
shilingi 2017, 700, 000, 000/=
Mfuko wa NSSF unadai
shilingi 1, 333, 600, 000, 000/=
Mfuko wa PPF unadai
shilingi 288, 600, 000, 000/=
Mfuko wa GEPF unadai
shilingi 18, 000, 000, 000/=
Mfuko wa NHIF (wa
afya) unadai shilingi 458, 600, 000/=
Aidha amesema
hali mbaya ya mifuko hiyo inatokana na fedha nyingi zilizochotwa na
serikali
pasipo kuzirejesha kwa wakati, na sasa imeanza kupunguza malipo ya
Pensheni ya
mkupuo kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 33.3 ya mshahara kabla
ya
kustaafu.
Pia amedai kuwa
serikali inatumia wastani wa mshahara wa miaka 3 badala ya mshahara wa
mwisho
kukokotoa Pensheni.
Na kuwa imekuwa
ikipunguza makadirio ya umri wa kuishi – badala ya kustaafu kutoka miaka
15.5
hadi miaka 12.5.
Amesema pia
iunafanya hira katika kurekebisha vikokotoo limbikizi (Accrual rates )
vya
mifuko kutoka 540 kwenda 580 kwa mifuko ya PSPF na LAPF, na kuwa hali
hiyo
kamwe haikubaliki.
Hata hivyo
amesema kama chama wanaisihi serikali iachane kabisa na mpango huo
dharimu
kwani unaua nguvukazi ya Taifa la leo, kesho nala miaka ijayo.
Naye katibu wa
CWT Mkoa wa Iringa Mwalimu Mshamu Aly Mshamu amesema serikali inatakiwa
ilipe
madeni yake yote inayodaiwa na walimu, ifikapo septemba 14, na kama
haitafanya
ivyo Septemba 15 walimu wa Wilaya zote watakutana katika ofisi ya
mwajiri wao
kwa kila Wilaya.
Mshamu amesema
lengo la kufanya hivyo ni kuishinikiza serikali iwalipe stahiki zao
walimu,
kwani madeni hayo yanachangia kudhorotesha utendaji kazi wa walimu, na
kuwa
sasa kila mwalimu amdai mwajiri wake mpaka anapomlipwa.
Mshamu amesema
tamko hilo linaitaka serikali kuanzia Septemba 1 mwaka huu mpaka 15 iwe
imekamirisha madeni yote, kwani bila kufanya hivyo walimu watakaa katika
ofisi
za waajiri wao mpaka kutimia kwa sharti hilo.
Amesema walimu
wilayani Mufindi wanadai serikali zaidi ya shilingi Milioni 159, huku
Manispaa
ya Iringa ikidaiwa na walimu wake zaidi ya shilingi Milioni 279, na
Walimu wa
Wilaya ya Iringa wakiidai Halmashauri hiyo zaidi ya shilingi Milioni
160.
Mshamu amesema Wilaya
ya Kilolo nayo inadaiwa deni la zaidi ya shilingi Milioni 270 na walimu
wake,
na hivyo walimu mkoani Iringa kuidai Serikali jumla ya shilingi Milioni
871,
639, 188 na senti 70.
MWISHO.
CHANZO:matukiodaima
No comments:
Post a Comment