Na Rhoda Josiah
MJINI
kuna vituko! Kitendo cha kutojaaliwa makalio makubwa kwa staa wa filamu
za Kibongo, Esha Buheti kimemsababishia anangwe na wasanii wenzake.
Akipiga stori na paparazi wetu, Esha alisema anafahamu na
anawashangaa watu wanaoponda maeneo hayo ya mwili wake kwani kwa upande
wake anaamini kuwa mwanamke sura, makalio majaaliwa kwani hata mwanaume
aliyemuoa analijua hilo na anampenda jinsi alivyo.
“Kwa kuwa mume wangu ananikubali jinsi nilivyo hainiumizi kichwa
kwani mimi naamini sifa ya mwanamke ni tabia na wala siyo shepu kama
wengine wanavyofikiria,” alisema Esha.
No comments:
Post a Comment