Wednesday, 1 October 2014

FFU IRINGA WATHIBITI UKAWA KUPENYA KATIKA MAANDAMANO YA WALIMU

Mwenyekiti  wa CWT  Manispaa ya  Iringa  Zawadi Mgongolwa akisisitiza  jambo  wakati akitoa  salamu  zake kwa walimu  leo  uwanja  wa  samora 
Mgongolwa akiwataka  walimu  kuendelea  kufanya kazi kwa  moyo japo mishahara  yao haitoshi 
Walimu  wakiwa katika maandamano  hayo  leo 
Maandamano  ya  walimu Iringa




Walimu katika maandamano  yao  leo 
Ujumbe unasomeka   wadau 
Mgeni  rasmi katika  siku ya walimu Manispaa ya  Iringa Bw Adam Swai wa tatu kulia  ambae  amemwakilisha  naibu  waziri wa TAMISEMI Kasimu Majaliwa  akipokea maandamano ya  walimu 
Walimu  wakiingia katika  uwanja wa Samora kwa maandamano  leo 

Ulinzi  ukiwa  kamili gado 
Walimu  Manispaa ya  Iringa  wakiimba  wimbo  maalum  wa  walimu wakati wa maadhimisho ya  siku ya  mwalimu duniani 

JESHI la Polisi wilaya ya Iringa mkoani Iringa leo limeweka ulinzi mkali kwa kuweka askari wa FFU wakati wa maandamano ya siku ya mwalimu Duniani ili kuthibiti wafuasi wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)kujichomeka katika maandamano hayo.

Askari hao wa FFU na wale wa kawaida   walionekana  katika  maeneo  mbali mbali ya mji  wa Iringa  huku baadhi yao  wakiwa katika  uwanja  wa  Samora  ili  kuhakikisha wanaoshiriki maandamano hayo ya  siku ya mwalimu  ni walimu na si vinginevyo .

Mtandao wa www.matukiodaima.co.tz umeshuhudia  askari  wa  FFU wakiwa wamejiandaa  kikamilifu  kwa  kuwa na mabomu ya machozi  huku   walimu  hao  wakithibiti  vikali wasio  walimu kushiriki katika maandamano hayo kwa  kuweka  uzio mango la  kitambaa nyuma ya  maandamano  hayo na  viongozi  wake  kuwa  nyuma  ya uzio huo na  polisi  na mbele viongozi wengine  wakiwa  wametangulia na polisi.

Mmoja  kati ya  walimu  walioshiriki maandamano  hayo  alisema  kuwa  wamelazimika  kuweka  uzio huo  ili  kuwawezesha  walimu kushiriki maandamano hayo  bila watu  wengine  kujipenyeza kwa malengo  hayo  ili  kuvuruga siku  hiyo ya mwalimu.

Kwani  alisema  tetesi   za  chini kwa  chini  walisikia kuwepo kwa  watu wa UKAWA  kutaka  kushiriki  maandamano hayo kwa malengo  yao ya kupinga katiba jambo ambalo  wao kama  walimu  baada ya  kulipata waliamua  kuwa makini  zaidi  ili kuepusha siku  yao  kuingizwa  mambo ambayo si malengo  haswa ya mwalimu.

Hata  hivyo  hakukuwa na  vurugu zozote  zilizopata  kujitokeza katika maandamano  hayo kutokana na  waandamanaji  hao  kufanya maandamano ya amani  chini ya  ulinzi  wa polisi ambao  walikuwa nyuma  zaidi ya  waandamanaji ili  kuthibiti wale  wasiopenda amani  kujipenyeza .

Akitoa  salamu  za walimu  katika maadhimisho  hayo ya  siku ya mwalimu Duniani mwenyekiti  wa chama cha  walimu (CWT) manispaa ya  Iringa  Zawadi Mgongolwa  alisema  kuwa  mbali ya mwalimu  kufanya kazi kwa  kujituma  ila bado mwalimu ameendelea  kuishi maisha ya  shida  kutokana na  serikali  kushindwa  kuwathimini  walimu nchini.

" Sherehe  hizi  za mwalimu  duniani hufanyika  kila  mwaka Octoba 5 ila  kwa Manispaa ya  Iringa   tumeamua  kuifanya  leo   ili kuwapa nafasi  walimu  wanaokwenda mkoani Kagera katika sherehe za  kitaifa .....ndugu  mgeni rasmi  huwa  tunapenda  kukutana  mara kwa  mara  ila tunashindwa  kuthiminiwa na serikali  yetu"

Alisema  kuwa    ofisi ya  chama  cha  walimu Manispaa ya  Iringa  iliweka utaratibu wa  kukutana na  walimu  ila ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  imekuwa ni tatizo kuwa  katika  kuwaunganisha  walimu pamoja na hata  katika maadhimisho hayo ni walimu chini ya 10000  ndio  wameshiriki kati ya  walimu  zaidi ya 2000 waliopo mjini Iringa.


Hivyo  alisema  kuwa  wameamua  kufanya sherehe hizo wenyewe   ili  kuuganisha  umoja  wa  walimu mbali ya Manispaa ya  Iringa  kuwatenga  walimu  hao na  kuwa  itafika  siku  watafikisha malalamiko  yao  rasmi katika  ofisi ya TAMISEMI ili chama  hicho  kiweze kuwa  chama  rafiki na serikali .

Mwenyekiti  huyo  aliwataka  walimu  hao  mbali ya  kuendelea  kutothaminiwa  na  Manispaa ya  Iringa  ila  bado  wanapaswa  kuendelea  kuifanya kazi  hiyo kwa  moyo  ili  kuliendeleza Taifa na  kuwa  kazi hiyo ya  ualimu ni  wito na  kuwa  wanapigana  kwa ajili ya  vizazi  vijavyo na  si vinginevyo na  kuwa kauli mbiu  yao ya   Taifa  lisilo jali  walimu  halina mipango ya  kimaendeleo iwe  chachu kwa  pande  zote mbili  walimu na  serikali.
 
CHANZO MZEE WA MATUKIO DAIMA.

VITA YA BENDERA YAREJEA JIMBO LA IRINGA MJINI ,BENDERA ZA CCM POSTA ZASHUSHWA ZACHANWA

Mwenyekiti  wa tawi la CCM kwa madereva Taxi Posa kwa nyuma mjini Iringa James   Mpete kushoto  akionyeshwa  bendera  iliyochanwa 
WATU  wasiofahamika   wamevamia  tawi la CCM eneo la stendi ya  Taxi nyuma ya  posta  mjini  Iringa na  kushusha  bendera  mbili  zilizokuwa  zimetundikwa  eneo  hilo na  kuzichana chana .

Tukio   hilo  limetokea  usiku wa  kuamkia  jana  kwa  watu hao  kufika katika  eneo  hilo  kufanya  hujuma  hiyo   dhidi ya  bendera  za CCM eneo  hilo .

Mwenyekiti  wa  eneo hilo James   Mpete   alimweleza  mwandishi  wa habari hizi  kuwa   bendera   hizo  waliziweka  kwa  ajili ya  kuhamasisha uhai  wa CCM na kushawishi  vijana  zaidi  kubadilika na  kujiunga na CCM baada ya kuwepo  dalili za  ubabaishaji ndani ya Chadema.

Hivyo  alisema  kuwa mbali ya awali eneo hilo  kuwa na bendera  za  CCM na Chadema kutokana na  muda  ulivyozidi  kwenda  ndipo  vijana  wa  eneo hilo  walipoamua  kugeuka na  wale  wa  Chadema  kuungana na  wenzao wa CCM katika  kuhamasisha  uhai wa chama na  kupinga uwajibikaji  hafifu wa mbunge  wa  jimbo  hilo mchungaji Peter Msigwa .

Mpete  alisema  kuwa katika  hali ya  kushangaza ni  baada ya  watu hao  kuvamia eneo hilo na kushusha  bendera  za  CCM na kuzichana  kitendo  ambacho  wao  wanakiona kama ni  hujuma  kubwa na  wapo  katika harakati  za  kuwasaka  waliofanya   hivyo.

"  Kila  mmoja ana  chama  chake na  siasa  si ugomvi  sasa  tunashangaa kuona  watu  wanatuchania bendera  zetu .....kweli  tupo katika uchunguzi  mzito  wa  kuwasaka  wanaoendesha  siasa  za  vurugu  hivi" alisema  mwenyekiti huyo .

Kuwa wanaimani  kubwa  kuwa  waliofanya  hivyo ni wafuasi wa UKAWA na  wamefanya  hujuma  hiyo baada ya  kuzuiliwa  kufanya maandamano na  wameona  hasira  zao  wazimalizie katika bendera  za CCM jambo ambalo halina mahusiano na wao  kuzuiwa maandamano  yao.

Hali  ya  kisiasa katika  jimbo  hilo la Iringa mjini bado  si njema kwa vyama  vikuu  viwili Chadema na CCM kutokana na mvutano  uliopo ndani ya  vyama   hivi vikuu katika jimbo  hilo la Iringa mjini .

Kwa  upande  wa CCM wapo  katika mkakati wa kumwondoa mbunge Msigwa  kupitia oparesheni inayoendeshwa chini ya katibu wa mkoa wa CCM Hasan Mtenga oparesheni iliyopewa  jina la ondoa Msigwa Iringa hivyo  kutokana na hali  hiyo  vita  ya  kushindana  kushushiana  bendera  ndio  ambayo imeendelea katika jimbo  hilo .

Tuesday, 30 September 2014

KASELI JAMES: ILIKUWA NIFIE KIJIJINI KUFUATIA UVIMBE MKUBWA

ANATESEKA KWA SIKU 1460
MWANAMAMA Kaseli James mwenye umri wa miaka 29, mkazi wa Kijiji cha Stela Kata ya Kagea Wilaya ya Chato, mkoani Geita, anapata maumivu makali mwilini mwake kufuatia uvimbe mkubwa katika mdomo wake, unaomsumbua kwa muda wa miaka minne sasa.
Bi. Kaseli James, akiwa na uvimbe mkubwa  mdomo wake .
Licha ya kupata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa kipindi chote hicho, lakini maumivu yake yamekuwa yakiongezeka kila siku huku wataalamu wa hapo wakishindwa kutambua tatizo hasa linalomsumbua.
Akisimulia mkasa uliompata, wakati huu akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kaseli anasema alijisikia vibaya baada ya kuambiwa hivyo, kwani hakuwa na fedha na wala hakujua ni nani angeweza kumsaidia.
“Nilikata tamaa nilipoambiwa na madaktari kwamba matibabu yangu mpaka Muhimbili, niliamini ningefia kijijni kwetu, lakini Mungu alinipa nguvu nikawa napita kwa ndugu na maskini wenzangu walinichangia hadi zikafika shilingi 50,000 nilifanya nauli, wakati nakuja hata hela ya kula njiani sikuwa nayo, nilifika  na kulazwa,” alisema.
Tatizo lake lilianza mwaka 2010 alipojisikia kupata uchungu wa jino, uliofuatiwa na kuota kwa kijipele ambacho baadaye kilitumbuka kama vile ni jipu.
“Kimsingi tangu nianze  kuumwa sijawahi kupata matibabu ipasavyo, tatizo sina hela, hata kule nyumbani mara nyingi nilijiuguza kienyeji tu, huku mdomo ukiendelea kuvimba na kushindwa kula vizuri,” alisema mama huyo.
Aliongeza kuwa, wakati akiwa bado mzima, alijaaliwa kupata mtoto na mwanaume aliyemtaja kwa jina la Frank Samson, lakini baada ya ujauzito baba  huyo aliingia mitini na kumtelekeza bila huduma yoyote hadi hivi sasa.
Mwanamke huyo ambaye amelazwa Wodi namba 24 Jengo la Sewa Haji, anasema amefanyiwa vipimo, lakini bado tatizo lake kubwa litakuwa ni gharama za matibabu, kwani hata kaka yake aliyeongozana naye hana sehemu ya kulala wala kula.
Muonekano wa karibu wa uvimbe huo.
“Nimekuja na kaka ili aweze kufuatilia matibabu yangu lakini ndiyo hatuna uwezo wa kipesa na wala mahali pa kulala kaka yangu, kwa kweli tupo katika wakati mgumu sana.“Huko nyumbani kwetu hatuna ndugu mwenye uwezo ambaye anaweza kutusaidia wala hatuna vitu vya thamani ambavyo tungeviuza na kupata fedha za kugharamia matibabu yangu.
“Kwa kifupi maisha yetu ni magumu kwani kule kijijini tunategemea kilimo cha jembe la mkono, kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuna wakati tunakosa mavuno hivyo kuwa na tatizo la chakula.
“Nitoe shukrani kwa madaktari na manesi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, walionipokea vizuri na hadi muda huu nimeshapimwa vipimo mbalimbali nasubiri  majibu, lakini ndiyo bado kilio changu kipo kwenye gaharama za matibabu,” alisema Kaseli.
Mama huyo anasema kuwa baada ya kuondoka  wilayani Chato kwenda Muhimbili kimatibabu, mwanaye aliyemtaja kwa jina la Modesta Frank,  alimuacha kwa baba yake mzazi (babu) ambaye ni mzee akiwa na hali mbaya kiuchumi hivyo haelewi wanaishije.
Kwa yeyote aliyeguswa na matatizo ya mama huyu, anaweza kuwasiliana naye kwa namba yake ya mkononi 0754 912453 au kumtembelea Wodi Namba 24, Jengo la Sewa Haji Hospitali ya Taifa Muhimbili.

WANANCHI WAWASUBIRI WARIOBA, SITTA MTAANI


Stori: Ojuku Abraham
BAADA ya kutokea malumbano kati ya Mwenyekiti wa Tume Maalum ya Kukusanya Maoni ya wananchi juu ya mchakato wa Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba, Samuel Sitta, wananchi waliohojiwa wamesema wanawasubiri kwa hamu wanasiasa hao mitaani ili kuwasikiliza maneno yao.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba, Samuel Sitta.
Mara baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi katika Bunge Maalum la Katiba (BMK) Andrew Chenge kuwasilisha rasimu ya katiba inayopendekezwa, ambayo iliyaacha baadhi ya mambo yaliyokuwa katika rasimu iliyowasilisha na Tume ya Warioba, Waziri huyo mkuu wa zamani wa Tanzania, alisema anamsubiri Sitta mtaani waweze kujieleza mbele ya wananchi, ili hoja zao zipimwe.
“Ni kweli, kama alivyosema Warioba, waje huku mitaani watuambie hoja zao nani tumsikilize na kumfuata, maana sisi wengine tunaona kama wanatuchezea tu akili, rasimu rasimu, yaani wanatuchanganya kabisa,” alisema Tom Sisiri, mfanyabiashara wa nguo za mitumba aliyetakiwa kutoa maoni yake.
Mwenyekiti wa Tume Maalum ya Kukusanya Maoni ya wananchi juu ya mchakato wa Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba.
Shoyoza Ibrahim, mwanamke mjasiriamali mwenye duka la vyombo Mwenge jijini Dar es Salaam, alisema viongozi wanatakiwa kutoa elimu ya kutosha ili kuwafanya watanzania waelewe kinachojadiliwa, kwani hata maneno yenyewe yanayotumika, ni msamiati mkubwa kwao.
“Utawasikia wanasema sijui rasimu, akidi, muswada, mchakato na mambo mengine kama hayo, watu kama mimi naweza kuwa naelewa wanamaanisha nini wakisema hivyo, lakini ninajua kuna idadi kubwa ya watu hawajui maana ya maneno haya, sasa hii misamiati ingefafanuliwa kwa lugha rahisi za watu kuelewa, halafu ndiyo watoe somo sasa la nini kinachobishaniwa,” alisema.
Bunge Maalum la Katiba ambalo lilikuwa likipitia rasimu ya katiba iliyowasilishwa bungeni na Jaji Warioba, linategemewa kumalizika mwishoni mwa wiki ijayo mjini Dodoma, likiwa na rasimu mpya inayopendekezwa.

TASWIRA TOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba, Kapteni John Komba, Bungeni mjini Dodoma
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Fahmi Dovutwa wakiteta, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 29, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir kificho (kushoto) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi wakiteta, Bungeni mjini Dodoma Septemba 29, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Lazaro Nyarandu (kushoto) na Mwigulu Mchemba wakiteta, bungeni Mjini Dodoma Septemba 29, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza, Bungeni Mjini Dodoma Septembe 29, 2014.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta akifafanua kuhusu namna wajumbe wa Bunge hilo watakavyopiga kura, bungeni mjini Dodoma Septemba 29, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Sheikh Hamid Masoud Jongo akichangia, Bungeni mjini Dodoma, Septemba 29, 2014.

Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikani nchini na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Donald Mtetmela akichangia Bungeni mjini Dodoma Septemba 29, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Bernard Membe wakiteta kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UMOJA NI NGUVU::MKUTANO WA JUMUIYA YA WATANZANIA SWEDEN NA KUMKARIBISHA BALOZI DORAH MSECHU

 Mama Dora Msechu Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchi za kinordic na Baltic alipokelewa kwa shangwe.
 Muziki hadi lyamba.
 Wadau wakiserebuka.
DJ Richie akitoa burudani.
  Dj Richie na Erick Kalebi wakiwajibika.
 Mama Dora Msechu Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchi za kinordic na Baltic alipokelewa kwa shangwe.
 Palipendeza.
 Mbili zatosha???
 Ukumbi ukiwa nyomi.
 Ngoma na nyimbo za kwetu.
 Nyomi ya watu waliofika.
 Watu wakia katika ukumbi

Monday, 29 September 2014

Baada ya shule ya Ifunda Tech kufungwa kwa vurugu uongozi wa shule waita wanafunzi 28


Uongozi wa shule ya sekondari ya Ifunda tech umewaita wanafunzi 28 kufika shuleni hapo octoba 2 .

Hatua ya uongozi wa shule hiyo kuwaita wanafunzi hao imekuja zikiwa ni zaidi ya siku 4 kupita toka shule hiyo kufungwa kufuatia vurugu kubwa shuleni hapo.

Makamu mkuu wa shule hiyo  Ernest Sakafu ameyasema hayo Leo wakati akizungumza na mtandao wa matukio daima ofisini kwake .

Amewataja wanafunzi wanaotakuwa kufika shuleni hapo kuwa ni steven Nyiriri,petro Kalolo,Iddi shaban,John Zephania,Edwin Rwegoshora,Adinan mrisho mtiti ,Izengo Dotto,Gaspar Manyagi,shemson Amoni ,Halid Omari,said sambo ,paschal lusukanija ,Fred Kidava na Eliji Nguvila

Wengine ni Stambuli Daluweshi,Jackson Mlowe,Sidi Kayombo,Yusuph Makale , Joseph Antony ,Allan Laurent , Rose Kayombo,Enoce John ,Rashid Kandoro ,Abdul Zumo ,Petro Silwimba ,Joyce Nestory ,Michael Kimario na Athuman Ahamad

Alisema kuwa kwa sasa shule hiyo imefungwa kutokana na vurugu hizo hivyo shule hiyo itafunguliwa wakati wowote kuanzia sasa.

USHAURI::NINI CHA KUFANYA MPENZI WAKO ANAPOWASILIANA NA EX WAKE?

Shukrani ziende kwake Muumba ambaye kwa mara nyingine ametupa nafasi ya kukutana kwenye uwanja wetu huu, tukijuzana, kuelimishana na kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi.Wiki iliyopita tulianza kuijadili mada hii kama inavyosomeka kwenye kichwa cha habari kuhusu hatua unazopaswa kuzichukua unapogundua kuwa mpenzi wako, mumeo au mkeo ana mawasiliano na mpenzi wake wa zamani (ex wake).
Tulianza na mfano halisi wa jinsi mwanamke mmoja aliyeishi na mumewe kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kupata watoto, alivyoumia baada ya kugundua kuwa mumewe ana mawasiliano na mpenzi wake wa zamani kiasi cha kutamani hata kuyakatisha maisha yake.
Niwashukuru wote waliochangia mada hiyo kwa ujumbe mfupi wa maandishi, nilichokibaini ni kwamba tatizo linalomsumbua mwanamke huyo, linawasumbua watu wengi sana lakini hawana pa kusemea.
Leo tunaendelea kuangalia dalili za hatari ambazo ukiziona kwa mwenzi wako, zinaashiria kwamba bado anampenda ex wake na kuna uwezekano mkubwa bado wanaendelea kuwasiliana. Tulianza na dalili ya kwanza ambayo ni mpenzi wako kumzungumzia ex wake mara kwa mara, iwe kwa mazuri au kwa mabaya.
2. Anazo namba zake za simu. Mapenzi yakishafika mwisho, namba ya simu ya mliyeachana haina umuhimu tena lakini ukiona bado mpenzi wako ameisevu namba ya ex wake kwenye simu yake au ameiandika kwenye diary, hiyo ni dalili mbaya kwamba wanawasiliana. Endelea kuchunguza.
3. Anabadilika ghafla akimuona hata mkiwa pamoja. Yawezekana mpo kwenye matembezi au shughuli za kawaida na mpenzi wako, ghafla ex wake akapita mbele yenu na ghafla mwenzako akabadilika.
Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio, akakuachia mkono hata kama mlikuwa mmeshikana kimahaba, akatangulia mbele, kubaki nyuma au akamgeukia ex wake, hiyo ni dalili kwamba bado anampenda na kuna uwezekano mkubwa wakawa wanaendelea kuwasiliana.
4. Anajifanya ni rafiki yake wa kawaida. Hakuna urafiki wa kawaida kati ya mtu na ex wake. Ukiona walishaachana lakini bado wanajifanya ni marafiki wa kawaida, lazima ujue kwamba kuna mchezo unaochezeka nyuma ya kisogo chako.5. Anakasirika akisikia ex wake anatoka na mtu mwingine. Hii ni dalili nyingine muhimu, hata kama walishaachana siku nyingi zilizopita, kama bado ana hisia juu ya mpenzi wake wa zamani, atajisikia wivu na kukasirika akisikia anatoka na mtu mwingine. Ataonesha wivu waziwazi, atamchukia, atamsema vibaya na wakati mwingine hata kupigana na mpenzi mpya wa ex wake.
6. Anaendelea kumpa misaada mbalimbali. Ukiona mpenzi wako anaendelea kumsaidia ex wake kama kumtumia muda wa maongezi, fedha za matumizi au kodi ya chumba, ujue bado wanapendana na anafanya hayo kwa sababu anaamini ipo siku watarudiana.
7. Bado anazo zawadi walizokuwa wanapeana kipindi cha nyuma. Ukiona mpenzi wako bado anatunza zawadi walizowahi kupeana na ex wake kipindi cha mapenzi yao, ni dhahiri kwamba bado anampenda na wanaendelea kuwasiliana.
Yawezekana pia kwenye simu yake bado kuna sms au picha walizokuwa wakitumiana kipindi cha nyuma, amezihifadhi hataki kuzifuta! Hiyo ni dalili kwamba bado anampenda.
MBINU ZA KUKABILIANA NA TATIZO HILI
Kuna usemi wa wahenga kwamba ukishalijua tatizo ni rahisi sana kukabiliana nalo ndiyo maana kabla ya kukupa mbinu za kupambana na tatizo la mpenzi wako kuwasilianana ex wake, nimeanza kwa kukupa dalili ambazo ukiziona, ujue bado anampenda ex wake na wanaendelea kuwasiliana.

RAIS KIKWETE KUZINDUA UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE - TEGETA


Rais Dk. Jakaya Kikwete.
Na Haruni Sanchawa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa upanuzi wa barabara ya Mwenge - Tegeta yenye urefu wa kilomita 12.9 Oktoba 1 mwaka huu katika eneo la Lugalo, njia panda ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Injinia Musa Lyombe amesema uzinduzi huo utafanyika kuanzia majira ya saa 4 asubuhi na kuongeza kuwa upanuzi huo ni mkakati wa serikali ya Tanzania kupunguza msaongamano katika Jiji la Dar es Salaam.

UNANG’ANG’ANIA KUPENDA USIPOPENDEKA ILI IWEJE?

Bila shaka wasomaji wa safu hii mko vizuri na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Kwa upande wangu mimi ni mzima wa afya.Ni siku nyingine Mungu ametujalia uzima tunakutana kupeana mawili matatu yahusuyo maisha ya uhusiano.
Mapenzi yana nafasi kubwa katika maisha ya wanadamu, mapenzi ni hisia kali zilizoko ndani ya miili yetu ndiyo maana inatokea mtu anampenda mtu kiasi cha kutaka hata dunia nzima ijue kama amependa.
Uzuri wa mapenzi ni kupendana, kila mmoja ampende mwenzake. Ikitokea mmoja amempenda mwenzake halafu huyo anayependwa haoneshi ushirikiano hapo ndipo kunapokuwa na tatizo.
Anayependa anafanya jitihada za nguvu kuhakikisha somo lake linaeleweka lakini wapi, jibu linakuwa ni ‘no’. Jibu linakuwa hilo kwa sababu unayempenda yeye hakupendi.
Nimekuwa nikipata maswali mengi katika safu ya ushauri, wengi wanang’ang’ania kupenda mahali ambapo kimsingi hapapendeki. Yule anayependwa, moyo wake unakuwa hautaki tu kuridhia. Upendo haupo kwake, kuna aina ya mtu ambaye yeye anampenda na si wewe.
Kwa kuwa mapenzi ni hisia, mtu anakuwa mgumu kukubaliana na matokeo. Anang’ang’aniza penzi kwa nguvu zote. Anakuwa tayari kuligharamia penzi hilo kwa namna yoyote. Akili inamtuma kwamba ipo siku atamuelewa na moyo wake upate pumziko.
Akili yake hapo haiwazi kabisa kwamba kuna mtu unaweza ukampenda na yeye asikupende. Anasahau kabisa ule msemo wa ndege mzuri  hutua katika mti aupendao. Hawazi kwamba sifa alizoziona kwa huyo anayempenda naye ana sifa zake kwa mtu anayempenda.
Kabla hatujaendelea, ngoja nikupe mfano hai. Kuna mtu tumpe jina la A (jina lake halisi lipo). A yeye ameteseka kwa muda mrefu kumpenda mtu ambaye hampendi, amefanya jitihada nyingi kuhakikisha anampata binti mmoja lakini wapi. Majibu anayopewa ni zaidi ya kuudhi lakini eti akawa hakati tamaa.
Anasema amemweleza binti huyo kwamba anampenda, amewatuma marafiki zake, ametuma zawadi mbalimbali kama maua, vocha na nyinginezo lakini vyote hivyo vilikuwa ni kazi bure.
Mtoto wa kike haoni wala hasikii, hataki tu! Alionyesha msimamo wa hali ya juu. Hakutaka kugeuka nyuma. Sasa je, kupitia mfano huo tunajifunza nini?
Binti alifanya vile kwa sababu moyo wake haupo pale. Kama ingekuwa ni tamaa basi pengine angekubali mapema kutokana na mbinu mbalimbali ambazo A alizitumia. Ndugu zangu, penzi halilazimishwi maana ukilazimisha athari zake ni kubwa huko mbele ya safari.
Mbaya zaidi, uking’ang’ania sana, anaweza kukubalia leo kwa kuwa umemwonyesha fedha au zawadi mbalimbali, kesho zinaweza kuwa hazipo, hawezi kuona umuhimu wako tena. Wapo watu wa aina hiyo, wanaweza kukuvumilia kwa muda mrefu wakachoka na kwa kuona unazo, wanaamua kukubali ili wakutumie.
Watu wa namna hiyo ndiyo wale wanaosema: “acha nimlie maana kila unavyomueleza hakuelewi. Mwanaume king’ang’anizi huyu.” Atakula, atatumia fedha zako lakini akili na mawazo yake yanakuwa kwa mtu mwingine tofauti ampendaye.
Atakuficha juu ya mpenzi wake, atakuongopea na kukurubuni kwa maneno ya wizi ili aweze kukuibia vizuri kumbe akili yake haipo kwako. Utamsindikiza katika safari yake ya kuelekea kwenye ndoa huku wewe ukiamini ndiyo mume wako, kisha anakuacha solemba.
Watu wa namna hiyo ni hatari. Wanakuua huku unajiona. Tena wengine wanakuchekea kabisa machoni kumbe akili zao hazipo kabisa. Hatoangalia ameishi na wewe muda gani zaidi ya kuufuata moyo wake unapopenda. Utajuta!
Wakati anataka kuchukua maamuzi magumu, hatoangalia umedumu naye miaka kumi au kumi na tano. Siku moja tu anaamka na kukwambia hakutaki, hakutaki kwa sababu hakupendi...

SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA

Naendelea kuelezea mambo yanayosababisha mwanamke kutopata mimba. Endelea...
Kipimo cha upevushaji wa mayai kupima mirija ya uzazi, upasuaji mdogo kwenye tumbo na kumulika ndani ya mwili wake pia kipimo cha Ultrasound kitafanyika.
Vipimo kwa upande wa wanaume
Baada ya kuchukuwa historia  ya mgonjwa kwa urefu  kinachofuata ni vipimo vya kuangalia kama yupo kawaida  au kama kuna hitilafu. Vipimo hivyo ni kumchunguza  mwanaume kwa ujumla hali ya afya yake kwa kumpima kuanzia kichwani hadi miguuni.
Kupima mbegu zake,  kupima vichocheo vyake vya uzazi, kupima na Ultrasound kwenye korodani zake.
Ushauri
Muda wa kufany   Mwanamke anashauriwa kulalia mgongo huku ameinua magoti baada ya kufanya tendo la ndoa kwa muda wa dakika 20.
Kutotumia mafuta yoyote ya kulainisha uke kwani baadhi ya mafuta huua mbegu za kiume.
Kuacha kuvuta sigara kwa mwanaume na mwanamke  kwani uchunguzi huonyesha  kuwa uvutaji wa sigara  unasababisha ugumba na utasa.
Kupunguza uzito kwa mwanamke na mwanaume na kutumia vidonge vya madini  ya foric acid kwa ushauri wa daktari kumeonyesha msaada mkubwa kwa akina mama wanaopata shida ya kupata mimba.
Upimaji wa mbegu za kiume
Mbegu za kiume baada ya kutolewa zinatakiwa kufikishwa maabara kabla ya dakika 30 kwa upimaji.
Mwanaume anashauriwa kukaa siku 3 bila kufanya tendo la ndoa ndipo atoe mbegu zake. Ujazo au wingi wa mbegu kawaida ziwe zaidi ya milioni mbili. Kwa kawaida wingi wa mbegu ni zaidi ya milioni 25.

ZAWADI NI ZAWADI::DIAMOND AMZAWADIA WEMA MURANO

Gari aina ya Nissan Murano alilozawadiwa Wema Sepetu na mpenzi wake Diamond Platnumz.
Wema Sepetu akiwa na 'baby' wake Diamond Platnumz.
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amemzawadia gari aina ya Nissan Murano mpenzi wake Wema Isaac Sepetu katika bethidei yake jana.
Kupitia akaunti yake ya Facebook na Instagram, Diamond ameweka picha ya gari aina ya Nissan Murano aliyompatia Wema na kuandika kuwa alitamani ampe mpenzi wake huyo vitu vingi, pengine ingesaidia kueleza ni kiasi gani anapenda amuone akifurahi kwenye siku yake ya kuzaliwa japo hana uwezo huo.
Diamond aliongeza kuwa, tafadhali pokea hiki nilichojaliwa na siku zote tambua kwamba Platnumz wako anakupenda sana! Nakutakia bethidei njema beibi. Alimalizia Diamond kupitia Facebook.
Kupitia ukaunti yake ya Instagram, Diamond ameandika hivi: