Wednesday, 15 October 2014

MBEYA::VIJANA WA FOREST MBEYA WAMUENZI BABA WA TAIFA KWA KUFANYA USAFI

Vijana wa kata ya Forest jijini Mbeya wameungana pamoja bila ya kujali itikadi zao za kisiasa na kufanya usafi maeneo yote yanayozungu  kata yako ya Forest kumuenzi Baba wa taifa zoezi hili litaendelea zaidi ya wiki mbili pia wameahidi kumchukulia hatua mtu yeyote yule atakaekiuka kanuni sa usafi kata hiyo ya Forest 


Hongereni sana vijana wa Forest kwa mfano huo Mbeya yetu tunawapongeza sana  tunaomba vijana wa kata nyingine igeni mfano huu siyo kila siku tuwategemee Halmashauri ya jiji waje watufanyie usafi



Pia vijana hawa wanawashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kuwasaidia vifaa vya kufanyia kazi pamoja na maji ya kunywa






Baadhi ya Vijana wa kata ya Foret wakiwa katika picha ya pamoja 

USAFIRI WA ANGA::FAST JET KIMEO!


SHIRIKA la Ndege la Fast Jet linalotoa huduma ya usafiri wa anga katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na nje ya nchi, limelalamikiwa na wateja wake mbalimbali kutokana na jinsi linavyofanya kazi, Risasi Jumatano lina habari kamili.
Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Fast Jet.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wateja hao wamesema kuwa, matangazo ya kila siku kuwa shirika hilo linatoa huduma ya usafiri wa anga kwa bei nafuu ni usanii, kwani tiketi zinazouzwa kwa bei hizo ndogo, daima huelezwa kuwa zimekwisha.
“Wanatangaza kuna tiketi za shilingi 32,000, ni uongo, mimi binafsi nimewahi kuulizia hizi tiketi mara kadhaa, lakini kila nikiomba ninaambiwa zimeisha na hata ndani ya ndege sijawahi kukutana na msafiri mwenye tiketi ya bei hizo,” alisema Samuel Kuntu, mkazi wa jijini Mwanza.
Aliongeza yeye amewahi kusafiri mara kadhaa na ndege za Fast Jet, lakini amegundua upungufu mkubwa wa shirika hilo, ikiwemo nauli kubwa tofauti na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari.
“Jana (Jumapili iliyopita) nilikuja na ndege hii na nimelipia shilingi laki nne kwa safari ya Dar, bei hii ni kubwa, nadhani ATCL ndilo shirika lenye bei rahisi, lakini si hawa,” alisema Kuntu ambaye alionekana kujua mengi kuhusu Fast Jet.
Abiria wakishuka kutoka kwenye ndege ya Fast Jet.
Alisema shirika hilo la ndege lina utaratibu unaomuumiza mteja hasa pale anapoahirisha safari au kuchelewa ndege, tofauti na mashirika mengine kama Precision Air na Air Tanzania.
“Inapotokea abiria amechelewa ndege (no-show), Fast Jet humtaka alipe tiketi nyingine na kulipa asilimia 100, wakati mashirika mengine humtoza faini abiria ambaye amechelewa ndege kwa asilimia 25 ya bei aliyonunulia tiketi kisha kumpangia siku nyingine ya safari.
“Wakati mwingine wanaahirisha safari au ndege kuchelewa lakini mteja hafidiwi kwa chochote, ila mteja akichelewa, harudishiwi hata shilingi wala kupangiwa siku nyingine, alisema mfanyabiashara huyo anayesafiri mara kwa mara kati ya Mwanza na Dar es Salaam.
Msafiri mwingine , Sunday Shomari ambaye alisafiri na ndege hiyo akitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, alisema alisahau simu yake ya mkononi ya gharama kubwa pamoja na Ipad yake ndani ya ndege hiyo, lakini muda mchache baada ya kurejea hakupata vitu vyake.
“Nilikuwa na mke na watoto tunatoka Arusha, tulipofika Dar es Salaam tukashuka na kuvisahau vitu hivyo kwa bahati mbaya, tulipofika nje mke wangu akaniuliza simu yako ipo wapi? Nikakumbuka nimeisahau ndani ya ndege, nikarudi uwanjani na kuwaomba walinzi wanisaidie niende nikachukue simu yangu.
Marubani wa ndege ya Fast Jet wakiwa mzigoni.
“Wakaniambia wao hawana mamlaka ya kuingia ndani ya ndege ile, badala yake wakanisaidia kuwaambia wafanyakazi wa ndege kuwa waniangalizie vitu vyangu pale nilipokaa, lakini jambo la ajabu eti wakadai hawakuviona, wakati mimi nilikuwa msafiri wa mwisho kushuka kwenye ndege, ina maana hakukuwa na mwingine baada ya mimi kushuka ambaye ningeweza kusema l ndiye aliyechukua vile vitu,” alisema Shomari ambaye ni mtangazaji wa zamani wa ITV na Radio One, kwa sasa anafanya kazi Sauti ya Amerika (Voa) jijini Washington, Marekani.
Abiria mwingine aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema mshangao mwingine kwenye ndege za shirika hilo ni kuuziwa vitu ambavyo katika mashirika mengine, wasafiri hupewa bure akitolea mfano soda, bia na viburudisho vingine.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika ofisi za Fast Jet zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutaka maelezo ya uongozi kuhusu tuhuma hizo, lakini walinzi walimzuia kuingia ndani na kutakiwa kuchukua anuani ya barua pepe ya msemaji wake, kwa maelezo kwamba ndiye angeweza kumsaidia kwa mambo ya kihabari.
Mwandishi aliandika madai yote na kuyatuma kwenye anuani hiyo akitaka kuonana na uongozi kwa ajili ya kujibu maswali kadhaa, lakini afisa uhusiano aliyejibu ujumbe huo, Lucy Mbogoro, baadaye alilitaka gazeti hili kuandika maswali hayo na kuyatuma, sambamba na nakala ya sura ya mbele ya gazeti.
Lakini hata baada ya kutuma maswali hayo kama ilivyotakiwa, Fasjet wameshindwa kutoa majibu na Lucy alipopigiwa simu na kuulizwa, alidai anayehusika na majibu hayo ametingwa na kazi.
Hata hivyo, gazeti hili bado linafuatilia kwa karibu ili kupata majibu ya maswali hayo.

KARIBU NYIKANI::CHADEMA MBEYA NA SURA ZILIZOJAA MACHOZI


 Kulia ni Mwenyekiti wa (CHADEMA) MBEYA MJINI, John Mwambigija, akizungumza na waandishi wa habari
NA GORON KALULUNGA
NIWASHUKURU wasomaji wangu mliotumia gharama kubwa za muda na fedha kwa kunipigia simu na kuandika jumbe fupi za maandishi kuhusu makala zilizopita ikiwemo ile ya athari ya saikolojia kwa taifa.
Ikumbukwe kuwa, meno ya mbele au sebuleni, hayana nguvu ya kutafuna chakula, bali mara kadhaa yamekuwa shujaa kwa ajili ya mwonekano wa mtu na kung’ata ulimi.
Uongozi ni sanaa, inayofanyika kwa watu, ili wafanye kwa manufaa yako, kwasababu unayoitaka au wanayoitaka wao, lakini mdomo kimya unatunza busara kulio mdomo unaobwatuka.
Dhima ya vyama vingi ni kushika dola, lakini hapa kwetu Tanzania,  dhima imegeuka kuwa ni kuundiana tuhuma na kusingiziana.
Kutokana na hali hiyo, jamii imebadilika, badala ya kuwa jamii moja na tulivu, sasa imekuwa jamii ya vita.
Wahanga wa siasa mara nyingi wanakuwa na hila na machoi katika mioyo na nyuso zao, huku wakiwaaminisha wananchi kuwa wao ni watu safi na wanaaa kwa mabadiliko ya fikra na maendeleo ya jamii.

Baadhi ya watanzania wanahitaji mabadiliko, wanayataka mabadiliko ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) na wasipoyapata huko wapo tayari kuyapata nje ya CCM.
Lakini wanakatishwa tamaa kuyaendea huko nje ya CCM kutokana na baadhi ya mambo yanayotendeka na kutokea, kama ifanyavyo CCM, ama zaidi ya CCM.
Tangu tunadai uhuru wa Tanganyika na hata mapinduzi matukufu ya Zanzibar, tulikataa mfumo wa ukoloni na ubeberu na kuhakikisha tunakomboa hata nchi zingine na kulaani mifumo hiyo.
Leo hii, kuna vyama nje ya CCM, vinakuja na mfumo ule ule ambao watanzania tuliukataa na kuupinga.
Kila anayewapinga kwa hoja hasa ndani ya vyama vyao huishia kutishwa kuwa watamfukuza au ajivue  gamba, badala ya kushindana nae kwa hoja.
Katiba ya nchi hii, imetoa uhuru wa kutoa maoni kwa kila mtanzania, lakini ndani ya baadhi ya vyama vya siasa, baadhi ya viongozi hawataki wengine watoe maoni.
Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, amewahi kunukuliwa akisema kuwa, bila kuwa na majadiliano hai ya chemsha bongo, mpaka hivi leo wanasayansi wasingeweza kuzalisha dawa nyingi za kutuliza maumivu, maana wangepigwa marufuku wengine kufikiri na kutengeneza dawa hizo kama ambavyo tume ya Warioba inavyotaka.
“Mfumo wa ukawa ni mfumo wa kudumaza fikra za watanzania na siyo uhisho wa fikra za taifa ambalo wananchi wake wanatakiwa kufikiri na kutoa maoni yao” anasema Shibuda.
Uongozi imara wa mtu yeyote ni ushawishi na wala siyo ubabe wa kutishia na kuhimiza kauli za ubeberu na kuzira.
Ndani ya Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Mbeya, wimbi hilo la kuikana demokrasia huku kikitangaza kuwa ni cha demokrasia, limeshika kasi.
Wanaotajwa kutaka kuwania nafasi za ubunge katika majimbo ya mkoani Mbeya, kupitia chama hicho, wananangwa kuwa wameamua kupeana nafasi za uongozi na kuwang’oa viongozi wasiowaunga mkono.
Baadhi ya viongozi hao ambao wote ni viongozi wa kanda ya nyanda za juu kusini, wanadaiwa, kutumia jina la Katibu Mkuu, Dr. Wilbroad Slaa, kuwa yeye ndiye hawataki viongozi waliokuwepo, hivyo, kuamua kuunda safu yake mpya kupitia wao.
Wanaotajwa kuratibu na kufanikiwa kung’oa wenzao kwa mtazamo wa kugombea ubunge 2015, ni pamoja na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za juu kusini, Frank Mwaisumbe, mratibu wa hamasa kanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mbeya mjini, John Mwambigija.
Wengine ni mkuu wa kitengo cha utafiti na sera kanda ya Nyanda za juu kusini, Fanuel Mkisi,  mkuu wa kitengo cha sheria na haki za binadamu, Fadhil Shombe,  mkufunzi mkuu kanda, Pascal Ahonga na Jamson Mwiligumo ambaye ni mkuu wa Chadema ni msingi.
Baadhi ya viongozi hao, wanatajwa kuwa ni wagombea tarajari wa nafasi za ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Mbeya, akiwemo Frank Mwaisumbe, anayetarajia kugombea jimbo la Mbeya vijijini.
Jamson Mwiligumo, anatajwa kuwa mgombea tarajari jimbo la Lupa Chunya, John Mwambigija na Lucas Mwampiki ambaye ni mkuu wa ulinzi na usalama kanda, wanatarajia kugombea Ubunge jimbo la Rungwe Magharibi.
Licha ya nafasi ya katibu wa mkoa kuwa wazi kwa sasa mpaka hapo litakapoletwa jina moja kutoka ofisi ya Katibu Mkuu Taifa, mpaka sasa kikosi hicho kinahusishwa na kumtangaza kuwa Katibu wa Chadema mkoa ni Fanuel Mkisi.
Majina ambayo yamepelekwa ofisi ya Katibu mkuu yakingoja uteuzi ni ya Boid Mwabulanga anayetetea nafasi yake, Jidawaya Kazamoyo na Fanuel Mkisi.
Ofisi ya katibu mkuu taifa tayari imepelekewa barua inayoonesha kusigana kwa viongozi hao mkoani Mbeya.
Tayari baadhi yao, wamemwandikia barua Katibu Mkuu wa Taifa, Dr. Wilbroad Slaa, kuhusu mwenendo wa kundi hilo, barua yenye kumbukumbu namba CDM/G/10/113.
Barua hiyo iliandikwa Agosti 9, mwaka huu, ikieleza jinsi kamati ya rufaa ya kanda ilivyo na mipango ovu dhidi ya chama hicho mkoani Mbeya.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa chama hicho, wanasema walisikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Chadema Mbeya mjini, John Mwambigija, aliyoitoa kwenye mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Mbeya Vijijini katika bustani ya Wagadugu Mbalizi, Agosti 29 mwaka huu, kuwa fitina zake zimefanikiwa baada ya kumng’oa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Vijijini, Elia Kabolile na aliyewahi kuwa katibu wa Chadema mkoa wa Mbeya, Eddo Mwamalala.
Kwa mipango hii, je watanzania wanaohitaji mabadiliko kuyapata nje ya CCM, malengo yao yatatimia? Au itabaki mpango ule ule wa “tukose” wote?
Karibuni nyikani.

EBOLA DISASTER::MARK ZUCKERBERG KUCHANGIA EBOLA


Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg (kulia) akiwa na mkewe, Priscilla Chan.
Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg amesema yeye na mkewe Priscilla Chan, watachanga dola milioni 25 za kusaidia vita dhidi ya Ebola.

Monday, 13 October 2014

POLE SANA>>NJEMBA ACHEZEA KICHAPO: KISA UKUWADI KWA MKE WA MTU!

Stori:  Issa Mnally
Adabu ishike mkondo wake! Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Jose amejikuta akichezea kichapo ‘hevi’ kilichomsababishia kuvunjika pua kwa tuhuma ya ukuwadi wa mke wa mtu, Ijumaa Wikienda lilikuwepo eneo la tukio.
Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Jose akivuja damu baada ya kipigo.
Msala huo wa aina yake ambao ulivuta umati mkubwa ulijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Makumbusho jijini Dar baada ya kijana huyo kuwekewa mtego na kukutwa na mke wa mtu akimsomesha.
Kijana Jose akiondolewa eneo la tukio asije kuumizwa zaidi.
Kwa mujibu wa jamaa waliomwekea mtego Jose (wa kwanza kulia pichani juu), jamaa huyo amekuwa sugu mtaani hapo kiasi cha kuwakera baadhi ya vijana wenye wapenzi na wake zao.Jose alishuhudiwa akila kichapo kutoka kwa vijana wasiotaka kufuata sheria bila shurti hadi akatiririkwa damu chapachapa puani baada ya kuvunjika pua.
Baadhi ya vijana bado wakiwa na gadhabu wakati wa kuamulizia ugomvi huo.
“Haiwezekani awe anawakuwadia wake zetu kwa wanaume wengine, leo tulipanga tumtoboe hata jicho moja ili liwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama za Jose,” alisema mmoja wa vijana waliokuwa wakimsulubu jamaa huyo.Vijana waliokuwa eneo la tukio wakizozana katika songombingo hilo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mwanaume aliyemwekea mtego Jose ambaye aliomba hifadhi ya jina gazetini alisema kwamba, waliamua kumpa mkong’oto kijana huyo baada ya kuchoshwa na vitendo vyake hivyo.
Baadhi ya vijana wenye hasira waliochoshwa na tabia ya kikuwadi ya Jose.
Alisema hata mkewe alishamuonya juu ya mazoea na Jose na kumweleza kuwa akimkuta tu na kijana huyo lazima atampa talaka jambo ambalo lipo kwenye ‘prosesi’.
Kwa upande wake Jose alishindwa kusema lolote huku akisikilizia maumivu ya kipigo hadi alipoondolewa eneo la tukio na wasamaria wema.

MBEYA::NDENJELA AZINDUA MABASI MAPYA YA KISASA NDENJELA JET.


MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akikata utepe kuzindua mabasi ya kisasa ya kampuni ya Mwaji Group  jijini Mbeya


Ndani ya mabasi ya Ndenjela jet


MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro pamoja na Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahamed Msangi wakifurahia maelezo mafupi toka kwa Mkurugenzi mtendaji    wa Mwaji Group Allan Mwaigaga

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akiongea na wananchi waliohudhuria sherehe hizo za uzinduzi wa mabasi ya kisasa

 Mkurugenzi mtendaji    wa Mwaji Group Allan Mwaigaga
akiwashukuru wageni waalikwa kwa kuhudhuri sherehe ya uzinduzi wa mabasi yake ya kisasa

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahamed Msangi akitoa neno la shukrani na kusisitiza madereva kuwa makini barabarani na kuzingatia alama zote za barabarani

Moja ya wafanyabiashara wakubwa mkoani mbeya anaejulikana kwa jina la TUGHIMBE akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mbeya kuwa kumuunga mkono wenzao kwa kusafiri na mabasi ya Ndenjela jet

Kaimu meya wa jiji la Mbeya Fungo akimshukuru mkuu wa mkoa mbeya kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa katika uzinduzi wa mabasi hayo

Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe hiyo ya uzinduzi wa mabasi hayo


Awilo akitumbuiza katika uzinduzi wa mabasi hayo


Dereva wa kike Nusura akionyesha umahili wake wauendeshaji wa Basi hilo la Ndenjela Jet huku pembeni Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akishangaa
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dereva wa kike Nusura Maguliko mara baada ya kumwona akiendesha moja ya mabasi aliyoyazindua

Kondakta wa basi la  Ndenjela jet akisoma risala mbeya ya mgeni rasmi

Mtaalamu wa mitambo ya magari hayo, Joshua Mshanga, alisema vifaa vilivyofungwa kwenye magari hayo vinasaidia kupunguza ajali zinazotokana na ulevi, mwendokasi na kuyapita magari mengine sehemu za hatari.






MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka vijana kutokuchagua aina ya kazi bali kufanya kila jambo ili mradi wanaisaidia serikali katika kupambana na upungufu wa ajira nchini.
Kandoro alisema Serikali inatengeneza mazingira wezeshi kwa kila mtu kupata ajira na sio kumpa ajira kila mtu hivyo kwa anayetoa ajira kwa mtanzania mwenzake anachangia kutekeleza malengo ya serikalio ya kuhakikisha ajira zinapatikana.
Hayo aliyasema wakati akizindua magari ya kisasa ya Kampuni ya   Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mikao ya Mbeya, Rukwa na Dar Es salaam ya Ndenjela Jet katika hafla iliyofanyika Uyole kwenye ofisi ya kampuni hiyo jijini Mbeya.
Kandoro alizungumza hayo kufuatia mmiliki wa mabasi hayo, Allan Mwaigaga kuajiri zaidi ya watu 50 huku akizingatia haki sawa kwa kuwa na wanawake sawa na wanaume katika ofisi yake na kuwa na dereva wa kike anayeendesha moja ya mabasi yake.
Alisema kuna umuhimu wa watu hususani vijana wa kike kutokubagua aina ya kazi na ajira jambo litakalosaidia Serikali kuondokana na wimbi la upungufu wa ajira kwa wananchi unaolikabili taifa.
Alisema Ndenjela ni mfano wa kuigwa kwa kuwa ameweza kuajiri vijana bila kubagua jinsia ikiwa ni pamoja na kutekeleza maazimio ya Raisi ya kuhakikisha na toa ajira sawa kwa wanawake na wanaume yaani 50 kwa 50.
“ ndugu zangu tuige mfano wa huyu mmiliki wa haya mabasi kutoa ajira kwa watanzania wenzetu kwani kazi ya serikali sio kuajiri kila mtu bali ni kutengeneza mazingira wezeshi kama alivyofanya Mwaigaga kwa kuajiri watanzania zaidi ya 50 bila kubagua” alisema Kandoro.
Kwa upande wake mmiliki wa mabasi hayo, Allani Mwaigaga, ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Mwaji group workshop, alisema amelazimika kubuni magari ya kisasa kulingana na mahitaji ya watanzania yenye lengo kubwa la kyupunguza ajali nchini.
Alisema magari yake yataweza kuwa mfano hapa nchini kwa kupungiuza ajali kwa kiwango kikubwa kutokana na kufungiwa kifaa maalumu ambacho kitakuwa kikiyaongoza magari hayo pamoja na dereva anayeendesha na kutoa taarifa kama atakiuka sheria za usalama barabarani.
Alisema magari hayo yamefungiwa mtandao wa WIFI ambapo kila gari litakuwa likiongozwa na watu wanne akiwemo Dereva hivyo watuwengine watakuwa wakibaki Mbeya katika chumba maalumu wakifuatilia mwenendo wa gari kila hatua linapokuwa likisafiri.
Naye mtaalamu wa mitambo ya magari hayo, Joshua Mshanga, alisema vifaa vilivyofungwa kwenye magari hayo vinasaidia kupunguza ajali zinazotokana na ulevi, mwendokasi na kuyapita magari mengine sehemu za hatari.
Alisema kifaa cha GPS kilichofungwa kwenye magari hayo kinawezesha aliyekuwa kwenye chumba cha kuongozea magari kujua gari lilipo, kama dereva anayeendesha ni mlevi, spidi ambayo gari linatembea au dereva akienda tofauti na alikopangiwa ambapo kifaa hicho hutuma taarifa haraka na kutoa hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kwa wakati huo.
Mwisho.

                            Na Mbeya yetu

MARA::Vicent Nyerere: Kuenzi ni vitendo maneno kelele

 
 
 
 
 
 Na Mathias Canal
 
Katika kuenzi Nyerere Day kwa vitendo Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini (CHADEMA) Vicent Nyerere, amejenga choo chenye matundu 8 katika kijiji cha Bumangi, ambapo anataraji kukabidhi kwa serikali ya kijiji mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.

Kijiji hicho ambacho kipo kata ya Muriaza Wilaya ya Butiama mkoa Wa Mara, wananchi wamekuwa wakijisaidia porini kwa muda mrefu sasa.
Nyerere alisema kuwa gharama kubwa ilitarajiwa kutumika katika ujenzi wa choo hicho lakini hadi hivi sasa, gharama inayotarajiwa kutumika ni shilingi millioni 3 kwa kuwa wanachama wa Chama Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wamejitolea kufanya kibarua bila malipo.

"Tumejenga Choo kijiji jirani cha Bumangi soko ili wananchi wapate kujisaidia kuliko kwenda porini" Alisema Nyerere
Hata hivyo alisema kuwa Choo hicho kitakabidhiwa kwenye serikali ya kijiji mara baada ya kukamilika ujenzi kwa ajili ya utunzaji.

Aliongeza kuwa soko la bumangi hufanyika Mara moja kwa wiki na linahudumia zaidi ya vijijini 37 hivyo wananchi hukumbana na adha kubwa kwa kujisaisaidia porini kutokana na kutokuwa na choo.

Nyerere ametoa wito kwa wakazi wa maeneo ya Bumangi kutumia choo hicho kwa usafi na kukitunza ili kiweze kudumu kwa muda mrefu.

Alisema Maliwato/choo ni sehemu muhimu sana katika eneo lolote linalotumiwa na binadamu na ni sehemu inayohitaji usafi wa hali ya juu sana ili kuepukana na magonjwa ya milipuko.

HABARI::Wauguzi waombwa wasigome Liberia

Zaidi ya watu 4,000 wamefariki kutokana na Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi
Maafisa wa afya nchini Liberia, wanawaomba wauguzi na wasaidizi wao kusitisha mpango wao wa mgomo wa kitaifa huku mlipuko wa Ebola ukiendelea kukithiri nchini humo.
Chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa afya, kinataka serikali iwaongeze marupurupu kwa kuhatarisha maisha yao hasa kwa wale wanaowatibu wagonjwa wa Ebola.

Rais wa Marekani Barack Obama, ameamuru hatua zaidi kuchukuliwa za kuhakikisha wauguzi hawapatwi na ugonjwa huo.

Muuguzi mmoja ambaye alikuwa anamtibu mgonjwa wa Ebola yeye mwenyewe aliambukizwa ugonjwa huo.

Naibu waziri wa afya wa Liberia , Tolbert Nyenswah alisema ikiwa mgomo utafanyika sasa hivi utakuwa na athari kubwa kwa walioathirika na pia kuathiri hatua zilizofikiwa hadi sasa katika vita dhidi ya ugonjwa huo.

Serikali inasema kuwa janga la Ebola ni kubwa na ina maana kuwa serikali haiwezi kutimiza ahadi ya kuwalipa pesa zaidi wafanyakazi hao kwa kuhatarisha maisha yao.

Kiwango wanacho lipwa ni dola 500 kila mwezi , pamoja na mshahara wao wa kati ya dola 200 na 300.
Wauguzi hao sasa wanataka kulipwa dola 700 kama marupurupu ya kuhatarisha maisha yao wakiwatibu wagonjwa wa Ebola.

Wafanyakazi hao wa afya, pia wanataka vifaa vya kuwalinda kutokana na maambukizi pamoja na kupewa bima ya afya na serikali.

Wauguzi wengine 95 wamefariki kutokana na Ebola nchini humo.

Liberia ni moja ya nchi zilizoathirika vibaya sana na Ebola.

Zaidi ya watu 4,000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo tangu ulipoanza kuwa kero hasa kwa mataifa ya Afrika Magharibi.

Chanzo;BBC SWAHILI

UDAKU::MNIGERIA AOZA PENZI LA JOKATE

Stori:  Hamida Hassan na Gladness Mallya
Kutoka moyoni! ‘Ubuyu’ mpya mjini ni madai ya staa wa muziki wa Nigeria, Panshak Zamani ‘Ice Prince’ kuoza akilitamani penzi la staa wa Kibongo, Jokate Mwegelo ‘Jojo’.
Staa wa muziki wa Nigeria, Panshak Zamani ‘Ice Prince’ kuoza akiwa na staa wa Kibongo, Jokate Mwegelo ‘Jojo’.
MNIGERIA ABEMBELEZA
Habari kutoka kwa vyanzo makini zilidai kwamba, Mnigeria huyo amekuwa akiwasiliana na kumbembeleza Jokate usiku na mchana akiomba wawe pamoja kwa jinsi moyo unavyomtuma.
Ilidaiwa kwamba hivi karibuni, Ice Prince anayekimbiza na ngoma yake ya I Swear amekuwa akitumbukiza vipande vya video kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram akimsifia Jokate ambaye anapendelea zaidi kumwita Kidoti.
ICE PRINCE: I MISS YOU KIDOTI!
Ilisemekana kwamba katika moja ya video hizo jamaa huyo anayefanya kazi na Jokate kwenye Runinga ya Chanel O nchini Afrika Kusuni ‘Sauz’ alisikika akimwambia mwadada huyo; ‘I miss you Kidoti’.
CHANZO CHATIRIRIKA
“Jamaa amemzimika Jokate ile mbaya. Unaambia anapiga simu na kumwita Jokate Sauz kila siku.
“Jamaa kafa kaoza. Kama unasikia mahaba niue ndiyo hayo sasa. Ishu ipo kwa Jokate tu kumkubali maana Ice Prince amekuwa akimuahidi kumpa maisha ayatakayo mtoto wa kike. Kazi anayo bidada, aamue kusuka au kunyoa,” alisema mmoja wa watu wa karibu wa Jokate.
Staa wa muziki wa Nigeria, Panshak Zamani ‘Ice Prince’
JOKATE ABANWA
Baada ya kunyetishiwa ‘mchele huo ulionyooka’ Ijumaa Wikienda, gazeti namba moja la mastaa Bongo lilimsaka Jokate ambapo aliulizwa juu ya uhusiano wake na mwanamuziki Ice Prince na iwapo anajua kuwa ana mapenzi na yeye na kama akimtamkia ndoa, je, atakubali?
Huku akionekana kushtushwa na habari hiyo, Jokate alisema kwamba iwapo Ice Prince atamwambia jambo hilo, atamchunguza tabia zake na kama zitamridhisha basi hana shaka atamkubalia.
MWANAMKE SHURTI APENDWE
Jokate alisema kwamba mwanamke kupendwa ni habari nzuri, ingawa hadi sasa bado hajaona wa kumuoa.
BOFYA HAPA KUMSIKIA KIDOTI
“Sijaona bado wa kunioa lakini kama Ice Prince ana nia, nitamchunguza kama anafaa ishallah,” alisema Jokate huku akicheka.
ATAKA MTOTO
Kwa upande mwingine staa huyo wa sinema na Bongo Fleva alisema kwa sasa matamanio yake yote anahitaji mtoto kutokana na umri wake (miaka 27) kuzidi kuyoyoma.
Staa wa Kibongo, Jokate Mwegelo ‘Jojo’.
BABA BORA MPO?
Jokate alisema kuwa kama kweli akijitokeza baba bora (husband material) atazaa haraka.
Mwanadashoti alisema kwamba, yeye kama msichana, anatamani siku moja aitwe mama na kila akikaa anapata mawazo ya kuzaa lakini anashindwa kwa sababu Mungu bado hajamjalia mume ambaye atazaa naye.
“Natamani mtoto kiukweli basi tu ni Mungu anapanga ndoa lakini akinijalia tu mimi nitazaa mapema, sitasubiri ndoa yangu ikae sana kama wanavyofanya wanandoa wengine,” alisema Jokate.
KUKUTANA CHANEL O
Jokate mwenye mipango lukuki na bidhaa za Kidoti na Ice Prince wanatarajia kukutana kwenye kipindi kipya cha Runinga ya Channel O kinachokwenda kwa jina la Top Ten Most na huko ndiko kitaeleweka.
KWENYE ‘PROFAILI’ YA JOKATE
Huko nyuma Jojo aliwahi kuhusishwa kutoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mbongo ambaye ni staa wa Mpira wa Kikapu (NBA) nchini Marekani, Hasheem Thabeet Manka.

Saturday, 11 October 2014

WAZO LA MCHEPUKO::MCHEPUKO SI NDIYO DILI, KWA NINI UWE UPANDE MMOJA!

Bila shaka mu wazima wa afya wasomaji wa safi hii. Ni siku nyingine tena Mungu ametujalia tunakutana katika safu yetu na kujuzana mawili matatu yahusuyo maisha yetu ya uhusiano. Muhimu kupeana darasa maana ni moja ya kujifunza vitu vipya au kukumbushana vile ambavyo tayari tunavifahamu.
Hakika hakuna asiyejua mchepuko katika kizazi cha leo. Watu wanachepuka kwenye ndoa na hata kwenye uchumba. Anayechepuka huwa akilini mwake ana dhima moja tu, “nachepuka ili kukidhi haja yangu lakini namuheshimu mke wangu.”
Anayechepuka anaamini kwamba anafanya tendo la siri. Anaamini ni siri yake hivyo si rahisi kwa mwenzake kuweza kushtukia mchezo. Tatizo hilo liko katika pande zote mbili japo ukubwa na athari zake zinatofautiana.
Uchepukaji wa mwanamke ni tofauti na ule wa mwanaume. Mwanamke ili achepuke anahitaji muda mrefu kujishauri kabla hajachepuka. Hakurupuki kuchukua uamuzi wa kuchepuka ndiyo maana anahitaji mtu wa kumshawishi sana ili aweze kuchepuka.
Tofauti na mwanamke, mwanaume yeye huligeuza suala la kuchepuka kama ni halali yake. Mara nyingi wanaume huwa wanaamini kuchepuka ni halali yao. Hawachukui muda mrefu sana kujishauri kuingia kwenye mchepuko. Anamuona mwanamke, haraka tu anachepuka.
Wanaume wanaamini kwamba wanapochepuka hawawezi kushtukiwa haraka. Wanaamini kitendo kile watakifanya kwa siri na umakini mkubwa ili wake zao wasiweze kugundua janja yao. Kutokana na kujiamini na kujipa taito ya kuwa mwanaume ndiyo kichwa cha familia, ndiyo maana wengi wanahalalisha tendo hilo na kulifanya eti liwe la kawaida kwa wanaume.
Ukifanya tathimini ya wanaume wengi, utagundua kwamba wanajipa uhalali kwamba bora wachepuke wao na si wanawake. Wanasema wanawake wanapaswa kuheshimu ndoa zao kama wao wanavyoheshimu lakini katika kipengele cha kuchepuka, wanawake ndiyo wakiheshimu zaidi lakini wao kipengele hicho wanakilainisha kidogo.
Wanakilainisha kwa maana kwamba wanaweza kuchepuka, wao ndiyo wenye majukumu ya kulea familia. Wanaongozwa na tamaa ya miili hususan kwa vibinti vidogovidogo ambavyo vinahamasisha kwa mavazi, shepu na muonekano wao kwa jumla.
Wanachepuka kwa madai kwamba wapate ladha tofauti. Eti anapokutana na kibinti kidogodogo kinamfanya aweze kuinjoi zaidi kwa sababu anakutana na vionjo vipya. Leo ataanza na huyu, kesho atakutana na mwingine ataonja ladha mpya kesho tena atahamia kwa mwingine.
Tabia inazidi kukua, haimchukui muda suala la kuchepuka kwake linakuwa ni mazoea. Haridhiki kabisa na uwepo wa mkewe peke yake. Hawezi tena kubaki njia kuu, kila siku ataendelea kuchepuka tena akiamini kwa kuwa mkewe hashtukii basi kwa upande wake ni halali lakini si kwa mkewe.
Hoja ya msingi ya kujiuliza hapa ni moja, kama mwanaume ameamua kuchepuka, siku mwanamke naye akichepuka itakuwaje? Kwa nini uamini kwamba mchepuko ni wa upande mmoja na si wa pande zote mbili? Utamu anaoupata mwanaume katika mchepuko ndiyo huohuo unaoweza kumpoza.

NAPE AKUTWA NA MAJANGA IRINGA

katibu  wa  itikadi na uenezi  wa chama  cha mapinduzi  (CCM)  Taifa  Nape  Nnauye apatwa na majanga  mkoani  Iringa baada ya  kuanguka na kuteguka mkono  wake wa  kulia wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya  timu ya  msafara wa Kinana  na Veteran mjini Iringa.


Tukio  hilo limetokea  mapema  asubuhi ya  leo na hivyo  kulazimika  kukimbizwa  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa kwa matibabu  zaidi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara  uliofanyika katika  uwanja  wa Mwembetogwa mjini hapa Nape  ambae  alikuwa amefungwa mkono  wake  alisema amepatwa na tatizo hilo leo asubuhi baada ya  kuanguka uwanjani japo  mbali ya kuanguka alisema hajaweza  kuacha kupanda  jukwaani  kuwaeleza  wananchi wa  Iringa mjini juu ya mbunge wao mchungaji Peter Msigwa(  Chadema)

Kwani  alisema ni lazima  mbunge Msigwa  aondoke  katika  jimbo  hilo baada ya  kushindwa  kuwatumikia  vema  wananchi wa  jimbo hilo na kuendelea  kuwaletea  mabalaa mbali mbali .

Nape  pia  ametymia nafasi hiyo kutaja ahadi  lukuki za mbunge  Msigwa ambazo alipata  kuwaahidi  wananchi pasipo  kuzitekeleza katika  jimbo  hilo.

UTAFITI:Viagra husababisha upofu.

Kipofu
Watafiti nchini Australia wanadai kwamba dawa inayotumiwa kuongeza nguvu za kiume VIAGRA husababisha upofu baada ya mda mrefu.
Kulingana na Watafiti hao kutoka Australia, kiungo fulani katika dawa hiyo inayotumiwa kukabiliana na ukosefu wa nguvu za kiume,huathiri uwezo wa kuona miongoni mwa wanaume ambao wana ugonjwa wa macho.
Kulingana na gazeti la Nation nchini kenya,Madaktari nchini Australia wamebaini kwamba kiungo fulani katika dawa hiyo kinaweza kusababisha upofu miongoni mwa wanaume wenye tatizo la ugonjwa wa macho.
Vilevile inadaiwa kuwa dawa hiyo pia inaweza kuwaathiri watumiaji ambao wanaona vizuri.
Utafiti huo uliofanywa katika panya,ulibaini kwamba hata watu wasio na ugonjwa wa macho wanaweza kuathirika.
                                                  ....bbcswahili.....

HABARI::KATIBU MKUU CCM;SINA HABARI NA MSIGWA,KAZI KUTUKANA..

Kinana  akiwahutubia  wananchi wa Iringa mjini leo

KATIBU  mkuu  mkuu  wa   chama  cha mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana awakuna  wananchi   wa jimbo la Iringa mjini   linaloongozwa na mchungaji Peter Msigwa (chadema) kwa  kuwataka  wana CCM kusoma alama  za nyakati badala ya  kuendelea   kutaka kuendelea  kugombea huku  wakijua  wakati  wao wa  kupendwa umekwisha.
Kuwa  rushwa  ndani ya  CCM na  serikali yake ndio ambao inakipeleka pabaya  chama    hicho  pamoja na ugomvi usiokwisha  ndani ya CCM.
Alisema  kuwa tabia ya   baadhi ya  wagombea  kulazimisha  kuendelea  kugombea  huku  wakijua wamechaja ni  moja kati ya  sababu ya  CCM kuendelea  kuchokwa na  wananchi na  hivyo kuamua  kuchagua  wapinzani.
Akiwahutubia  wakazi wa  jimbo la Iringa mjini katika  uwanja wa Mwembetogwa  leo  Kinana  alisema  kuwa tatizo la CCM  kupoteza  jimbo hilo ni uroho wa madaraka kwa  wale ambao  hawakubaliki  kwa wananchi kosa  ambalo kamwe  CCM haitarudia kulifanya.
 Kinana  alisema  kuwa  kuna  mitaa 150 katika  jimbo la Iringa mjini na mtaa mmoja pekee  wa Chadema  huku kata  zipo zaidi  ya 17 kata  moja ni ya Chadema  sasa  ni namna gani  CCM ishindwe  ubunge   jimbo hilo  hilo kama si tamaa za  uongozi  kwa baadhi ya  wagombea.
Hivyo  aliwataka   viongozi hao wa CCM kujaribu kusoma  alama za nyakati na  iwapo watajua  kuingia  wajifunze na kutoka kwani  kuna  wakati wa  kuchokwa  ni lazima  wakubali  kuondoka badala ya  kung’ang’ania  kugombea .
Pia  katibu   huyo aliwataka  wana CCM kujifunza  kujiuliza kwa  wananchi  wengine kama  wanakubalika ama  hawakubaliki badala ya  kusimamia  maamuzi yao ya  kuingia kugombea  bila  kupendwa  na  wananchi na kuwa kosa  lililofanyika mwaka 2010  kamwe  halitajirudia  tena.
“ Ni mambo ya  ovyo yaliyokuwa yakifanyika ndani ya  CCM ndio ambayo yamekigharimu chama   na kuwa jimbo la  Iringa mjini  hakuna  mpinzani  ila wapo wanaotafuta  kusikilizwa  katika mambo yao na  iwapo CCM itatenda  mema kwa kusikiliza  wananchi  jimbo la Iringa mjini  hakuna  upinzani  ila  upuuzi ,rushwa ndani  ya CCM na  serikali  yake ndio  imekigharimu  chama   hicho “alisema 
Alisema kuwa  ndani ya  serikali   hii mwananchi anatafuta haki yake hapati  hadi atoe  rushwa  huku  viongozi  waliopo ndani ya CCM badala ya  kushughulika na mambo ya  wananchi wanashughulika na mambo yao  wenyewe  kwa ugomvi usio kwisha .
“ Tunapoteza majimbo na kata kwa  ajili ya  uroho  wa  uongozi kwa baadhi yetu na  kushindwa  kushuka kuwasikiliza  wananchi wa chini hali  inayozalisha malalamiko ya  wananchi na  kupelekea  kuhamia vyama  vya  upinzania”
Akihutubia huku  akishangiliwa na  umati mkubwa  uwanjani  hapo  Kinana  alisema  kuwa  amefika  jimbo la Iringa mjini  kuwaeleza mambo ya  kimaendeleo  sio  kumsema  mchungaji Msigwa  .
Hivyo  alisema  kuwa  iwapo  jimbo la Iringa mjini  litapata  mgombea  mgombea  mzuri  hakuna   upinzani  katika  jimbo  hilo ila  kama  ugomvi  wa madaraka  utaendelea  itakuwa ni kazi kupata  mgombea  wa  CCM .
Katibu  mkuu  huyo alieleza  kusikitishwa kwake na  ushuru mbali mbali   kwa wananchi wanaojitafutia maisha  yao huku  viongozi  wakijiweka mbinguni na  wananchi  wao.
Japo alisema  kuwa  kazi  zilizofanywa na CCM na serikali yake ni kubwa na kuwa hata  miradi ya  barabara  inayoendelea  kujengwa  ni jitihada za  serikali ya  CCM chini ya rais  Benjamin Mkapa  hivyo  mbunge hana sababu ya  kujisifu  kwa  kazi hizo.
“ Nawaambieni  wala  hamta nisikia  nikishughulika na kumzungumzia mbunge  wenu hapa  sina Time  mimi nashughulika na  mambo ya  wananchi kwani  mbunge  wenu ni klazi yake  kutukana kila mmoja na kuhamasisha maandamano yasiyo kwisha “