Monday, 27 October 2014

MAHAFALI::2228 WAHITIMU KATIKA MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO KIKUU CHA IRINGA


Afisa mahusiano wa chuo cha Kikuu cha Iringa, Agness Kitundu akimpaa maelekezo mlinzi wakati wa mahafali ya chuo hicho.
WAHITIMU
WAHITIMU
WAHITIMU
WAHITIMU
WAHITIUMU
WAHITIMU
WAHITIMU
WAHITIMU
WAHITIMU
WAHITIMU
WAHITIMU


HOTUBA YA MAKAMU MKUU WA CHUO PROF. NICHOLAS T. A. BANGU KWENYE MAHAFALI YA KWANZA YA
CHUO KIKUU CHA IRINGA
TAREHE 25 OKTOBA 2014
1.    UFUNGUZI
Mheshimiwa Mkuu wa Chuo, Mh. Judge Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani,
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Iringa, Bishop Dr. O. Mdegela,
Wakuu wa Serikali na Taasisi mbalimbali,
Wafanyakazi wa Chuo,
Wanafunzi mliohitimu,
Wanafunzi mnaoendelea,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
2.    KUKARIBISHA WAGENI:
Awali ya yote kwa heshima na taadhima naungana na Mwenyekiti wa Baraza kuwakaribisha katika mahafali haya ya kwanza ya Chuo Kikuu cha Iringa kuwashukuru kwa kuhudhuria.
3.    PONGEZI:
Natoa pongezi kwa wanakamati ya maandalizi walioongozwa na Bwana Aloyce Suleiman na wengine waliohusika kwa namna mbalimbali kukamilisha maandalizi.
Nawapongeza wafanyakazi wote (wanataaluma na waendeshaji) kwa ujumla na kwa mmoja mmoja kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kipindi cha mwaka 2013/14 na kutufikisha kuwa na mahafali ya kwanza.
Nawapongeza wahitimu wote kwa kufikia hatua hiyo.  Ni dhahiri kuwepo kwenu hapa chuoni kumechangia kuwajenga kielimu, na ninaamini kumechangia kuwajenga kiroho na kimaadili na kuwa mtatumia nyenzo hizo zote kuchangia katika juhudi za kitaifa za kuboresha hali ya maisha ya Watanzania na walimwengu wote kwa ujumla.
4.    SHUKURANI
Katika kipindi cha mafunzo 2013/2014 wafuatao ni baadhi ya waliotufadhili kwa hali na/au mali:
·        Wazazi/walezi wa wanafunzi,
·        Serikali ya Tanzania kupitia taasisi yake ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB),
·        Serikali ya Umoja wa Ulaya,
·        Serikali ya Finland,
·        Serikali ya Uholanzi kupitia Shirika lake la NUFFIC,
·        Chuo Kikuu cha Nelson Mandela,
·        Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia LMC,
·        Shirikisho la Kilutheri la Amerika (ELCA):  kupitia Synod ya Eneo la Mt. Paul (St. Paul ares Synod),
·        Uongozi wa ngazi mbali mbali za Mkoa wa Iringa 
5.     MATUKIO- KIPEKEE MWAKA WA MASOMO 2013/2014
5.1.        Mradi wa Hifadhi ya Utamaduni, Utalii na Maendeleo endelevu Kanda ya Kusini mwa Tanzania (Cultural Heritage conservation, Tourism and Sustainable Development in Southern Highlands of Tanzania.
5.1.1               Mradi huu unafadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya (EU)
5.1.2               Katika Utekelezaji tuna washirika 8 na baadhi yao ni Chuo Kikuu cha Cottingen Ujerumani, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ofisi ya Manispaa ya Iringa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa.
5.1.3               Shughuli zilizofanyika mwaka huu zimo katika makundi matano:
5.1.3.1       Utafiti na uchoraji ramani.
5.1.3.2       Maandalizi ya upatikanaji Boma la Kijerumani toka Serikalini na mipango ya ukarabati.
5.1.3.3       Maandalizi ya kibiashara utamaduni na promotion
5.1.3.4       Kuhusisha wananchi katika biashara ya utalii wa utamaduni
5.1.3.5       Kwa kushirikiana na vyuo vya Ujerumani, Finland kujenga uwezo wa kitaaluma: vijana 9 wamepata ufadhili kwa ngazi ya Masters (M.A) na 1 kwa digrii ya falsafa (Ph.D) lengo ni kufanya utafiti wa utalii wa utamaduni kuwa moja ya agenda ya Chuo cha Iringa.
5.2.        Kuelekea kuwa Chuo Kikuu cha Kizazi cha Tatu (SGU) kizazi hiki kinatofautina na vizazi viwili vya awali kwa kufanya ujasiliamali kuwa sehemu ya taaluma. Tendo la kuingiza ujasiliamali linaenda kwa hatua:
5.2.1.            Kuelimisha waalimu na wanafunzi nafasi ya ujasiliamali katika taaluma.
5.2.2.            Kubadili mfumo wa ufundishaji kuwa mwanafunzi ndio kitovu cha kujenga elimu na pili kuhamasisha tambuzi zote sita za ubongo; kukumbuka (remembering), kuelewa (understanding), kuchambua (analyzing), kuchanganya (synthesizing), kutumia (Application) na kubuni (Creating)
5.3.        Kuwahamasisha wanafunzi kuanzisha makapuni ya kuzalisha mali wakingali choni kwa maana hiyo kuelekeza mafunzo wanayoyapata kwenye kampuni wanaoijenga. Hadi sasa shughuli kadhaa zimeanzishwa na zinaendelezwa na wanafunzi waliohitimu. Kwa mfano SAMIS inafanya shughuli za supermarkets na PESSI inayoshughulika na kuzungusha plastics na kadhalika.
Hatua ya nne ambayo imeanza mwaka huu ni kuimarisha uundaji wa kampuni kutumia nadhania inayoitwa Team Academy. Mwaka huu wa masomo tuna wanafunzi 40 ambao watafanya masomo yao kwa utaratibu huo sambamba na mafunzo ya kawaida na kuanzia mwakani mfumo wa masomo yao utakuwa unaelekea kwenye kampuni ambazo wameamua kuziunda na kuziendeleza.
Mafunzo ya namna hii yalizinduliwa huko Finland. Mwaka 1993 na hivi sasa umesambaa katika nchi kadhaa duniani Netherlands Hungary Argentina hususani Finland, France, UK, Spain, China, Brazil, Austelia). Kwa Africa chuo chetu kitakuwa cha kwanza. Juzi nilipata fursa ya kuelezea mfumo huu kwenye Mkutano wa NEPAD. Wajumbe wengi walifurahia na chuo cha Africa Zimbabwe na Jomo Kenyata wametukarisha tukawaeleze zaidi.
5.4.        Kitengo cha Kilimo (Institution of Agriculture) na kitengo cha mitaji midogo (Inst. Of Microfinance) vimepata ufadhili wa Kitengo cha America kinachoitwa Iringa Hope USA ufadhili wa Jengo litakalokuwa na vyumba vya ofisi na vyumba vya mijadala ya wakulima kuhusu stadi za kilimo na fedha.
5.5.        Kitengo cha Marekani cha ubadilishaji wa elimu kimefungua tawi katika Chuo cha Iringa. Kwa mwaka huu tawi lilipokea wanafunzi 5 mwezi wa Januari na mwezi huu hivi sasa wameongezeka hadi 20. Kila kundi limekuwa hapa kwa miezi mitatu na wanajifunza mambo mbali mbali. Matumaini yetu ni kwamba wanafunzi wetu wataweza kwenda katika vyuo huko Marekani.
6.     WAHITIMU:
Mheshimiwa Kaimu Mkuu wa Chuo,
Katika mwaka 2013/2014 jumla ya wanafunzi 2228 wanahitimu kwa mchanganuo ufuatao:
1.
Astashahada ya Theolojia (Certificate in Theology)
20
2.
Stashahada ya Theolojia (Diploma in Theology)
12
3.
Shahada ya Kwanza ya Tauhidi (Degree of Bachelor of Divinity –  (BD)
5
4.
Astashahada ya Ushauri Nasihi (Certificate in Counseling Psychology)
7
5.
Stashahada ya Ushauri Nasihi (Diploma in Counseling Psychology)
40
6.
Shahada ya Kwanza ya Ushauri Nasihi (Degree of Bachelor of Counselling (BCOUNS)
37
7.
Astashahada ya Utawala na Biashara (Certificate in Business Administration – CBA)
125
8.
Astashada ya Ununuzi na Usimaminzi wa Mali (Certificate in Procurement and Material Management)
24
9.
Stashahada ya Utawala na Biashara (Diploma in Business Administration)
353
10. 
Stashahada ya Sayansi katika Uhasibu na Fedha (Diploma in Accounting and Finance)
23
11.
Stashahada ya Ununuzi na Usimaminzi wa Mali (Diploma in Procurement and Material Management)
40
12.
Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Uhasibu na Fedha (Bachelor of Science in Accounting and Finance - BAF )
39
13.
Shahada ya Kwanza ya Uchumi na Fedha (Degree of Bachelor of Science in Economics and Finance)
34
14.
Shahada ya Kwanza ya Utawala wa Biashara (Degree of Bachelor of Business Administration)
88
15.
Astashahada ya Sheria (Certificate in Law)
52
16.
Stashahada  ya Sheria (Diploma in Law)
33
17.
Shahada ya Kwanza ya Sheria (Bachelor  in Law
166
18.
Astashahada ya Sanaa ya Maendeleo ya Jamii (Certificate in Community Development
65
19.
Stashahada ya Sanaa ya Maendeleo ya Jamii (Diploma in Community Development)
48
20.
Shahada ya Kwanza ya Sanaa ya Maendeleo ya Jamii (Bachelor of Arts in Community Development)
198
21.
Shahada ya Kwanza ya Anthropolojia ya Utamaduni na Utalii (Bachelor of Arts in Cultural Anthropology and Tourism)
94
22.
Astashahada ya Sanaa ya Uwanahabari (Certificate in Arts in Journalism)
7
23.
Stashahada ya Sanaa ya Uwanahabari (Diploma in Arts in Journalism)
6
24.
Shahada ya Kwanza ya Sanaa ya Uwanahabari (Bachelor of Arts in Journalism)
68
25.
Astashahada ya Sayansi na Teknolojia ya Habari (Certificate in Information Technology)
62
26.
Stashahada ya Sayansi na Teknolojia ya Habari (Diploma in Information Technology)
36
27.
Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Teknolojia ya Habari (Degree of Bachelor of Science in Information Technology)
43
28.
Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Hisabati (Bachelor of Education Mathematics)
58
29.
Shahada ya Kwanza ya Elimu katika ….. (Bachelor of Education – Arts)
274
30.
Stashahada ya Uzamili ya Elimu Ualimu (Postgraduate Diploma in Education – Teaching)
26
31.
Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Maendeleo ya Jamii na Usimamizi wa Miradi (Master of Arts in Community Development and Project Management)
38
32.
Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Saikolojia (Master of Science in Counseling Psychology)
2
33.
Shahada ya Uzamili ya Elimu – Sanaa (Master of Education –  Arts)
3
34.
Shahada ya Uzamili ya Sheria katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Master of Law in Information and Communication Technology Law
15
35.
Shahada ya Uzamili katika Mfumo wa Sheria za Jinai za Kimataifa na Haki za Binadamu (Master of Laws in International Criminal Justice and Human Rights (LLM-ICJ-HR)
9
36.
Shahada ya Uzamili ya Anthropolojia ya Utamaduni na Utalii (Master of Arts in Tourism, Culture and Society)
6
37.
Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (Master in Business Administration)
72
JUMLA
2228
Prof. NICHOLAUS . T. A. Bangu
VICE CHANCELLOR

UKATILI HUO::mwanamke aliyenusurika kubakwa ahukumiwa kunyongwa

Iran Madam
Reyhaneh Jabbari mwenye umri wa miaka 26 amehukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mtu mmoja ambaye alifanya jaribio la kumbaka.

Taarifa iliyoripotiwa na CNN inasema mwanamke huyo amenyongwa katika gereza la Tehrain, Iran ambapo alikuwa amefungwa baada ya kutenda kosa hilo mwaka 2007 wakati huo akiwa na umri wa miaka 19.

Mwanamke huyo amekutwa na hatia hiyo kutokana na kosa la kumuua aliyekuwa mfanyakazi wa wizara ya ulinzi na usalama nchini Iran, Morteza Abdolali.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu Amnesty International limelaani kitendo cha Iran kutoa hukumu hiyo, ambapo mbali na jitihada ya kampeni mbali mbali zilizofanywa ikiwemo zile za kwenye mitandao ya kijamii katika kuipinga hukumu hiyo kuonekana kutozaa matunda.
Taarifa kutoka nchini humo zinasema mahakama ilitoa hukumu hiyo baada ya kutojiridhisha na utetezi alioutoa mahakamani kwamba alitenda kosa hilo akiwa anajilinda.
Utafiti wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2011 unaonesha Iran ni moja ya nchi zinazoongoza kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo nchi hiyo ina wastani wa kutoa hukumu ya kunyongwa mtu 1 kila baada ya masaa 8.

Wednesday, 22 October 2014

KUMBE NI SIFA>>BABY MADAHA: NAWAPANGA TU WANAUME

Stori: Gladness Mallya
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha ambaye anadaiwa kuishi kinyumba na meneja wake Mkenya, Joe Kariuki wa Kampuni ya Candy n Candy Records, ametoa mpya baada ya kudai kuwa kutokana na kusubiri kwa muda mrefu ili apate mwanaume anayefaa kwa ajili ya kumuoa bila mafanikio, sasa ameamua kuwapanga foleni bila kujali idadi yao.
Msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha akiwa na Meneja wake Mkenya Joe Kairuki.
Akipiga stori na gazeti hili juzikati, Baby Madaha alisema amesubiri sana kuolewa lakini hajamuona mwanaume anayefaa, hivyo ameamua kuwapanga kama mafungu ya nyanya kama wao wanavyowapanga wanawake na ikitokea mmoja  ‘akamzingua’ anaachana naye na kumchukua mwingine.
Baby Madaha akiwa na msanii wa Kenya Wyre.
“Mimi sasa hivi nawapanga tu wanaume maana sioni anayenioa ndiyo maana nimechukua uamuzi huu, wanaume wamezoea kutupanga sisi wanawake sasa mimi ndiyo nimewageuzia kibao nao waone utamu wake na ikitokea huyu amenizingua namuacha nahamia kwa mwingine,”alisema Baby Madaha.

VITA NZITO: ALI KIBA VS DIAMOND, CLOUDS VS TIMES

Stori: Erick Evarist, Musa Mateja na Chande Abdallah
MTIFUANO! Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 limepita lakini nyuma yake limeacha vita nzito iliyowahusisha mafahari wawili, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba huku waandaaji wa tamasha hilo, Clouds FM wakisigana na Times FM kumgombea msanii wa Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’, Risasi Mchanganyiko linakupa mchongo kamili.
Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba akipafomu.
TIFU LILIVYOKUWA
Kwenye shoo hiyo iliyofanyika wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Ali Kiba (Team Kiba), walipiga kelele za ‘buuu’ pale alipopanda Diamond kutumbuiza ili kumharibia.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
CHANZO CHANENA
Chanzo makini kimedai kuwa, vurugu hizo hazikutokea kwa bahati mbaya bali zilipangwa na wafuasi wa Kiba ambapo inasemekana ziliandaliwa gari aina ya Toyota-Costa zipatazo 25 zilizokuwa zimejaa watu na kwenda kuwamwaga viwanjani hapo kwa shughuli mbili muhimu; kuzomea na kuhamasisha wengine wazomee pindi Diamond atakapopanda jukwaani.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifanya shoo na Davido wa Nigeria.
“Ishu ilipangwa, Team Kiba waliibuka na Costa kama 25 hivi, wakajipanga katika maeneo tofauti ya uwanja huo lakini zaidi walikaa karibu na jukwaa ili kuweza kutimiza vizuri azma yao ya kuharibu pindi Diamond atakapokuwa akitumbuiza,” kilidai chanzo hicho.
WALIFANIKIWA?
Kwa namna moja mashabiki hao walionekana kufanikiwa kwani waliweza kuwashawishi watu wengi wazomee kiasi cha kumfanya Diamond ashtukie  na kuamua kutamka hadharani: “Jamani kuna uhuni unaendelea hapa.”
Mkurugenzi wa Times FM, Rehure Nyaulawa.
TEAM DIAMOND WACHARUKA
Madai yanasema mara baada ya Team Kiba kufanya vurugu hizo na kufanikiwa, baadhi ya mashabiki ambao waliaminika ni wa Diamond (Team Diamond), walicharuka na kusema hawakubaliani na uhuni huo ambao umefanywa hivyo watahakikisha wanapambana kulipiza kisasi kwa namna yoyote ile.
“Hatukubali, wao si walijipanga hapa kumharibia Diamond, sasa na sisi tutahakikisha tunalipiza kisasi kwa namna yoyote,” walisikika wakisema mashabiki wa Diamond.
TALE AKIRI KUSIKIA
Paparazi wetu aliwatafuta Diamond na Kiba ili kujua wanazungumziaje vurugu hizo. Baada ya kumtafuta Diamond bila mafanikio, alipatikana meneja wake, Hamis Taletale ‘Bab Tale’ ambaye alikiri kuwepo kwa maandalizi ya zomeazomea ambayo yalikuwa na lengo ya kumharibia msanii wake.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mtahaba.
“Hizi kwetu tumezichukulia kama changamoto, tulisikia kwamba kuna watu wamelipwa kwa ajili ya kufanya fujo lakini hatukujali sana kwani lengo letu si kugombana na mtu, sisi tunafanya muziki mzuri ambao ndoto zetu ni kuufikisha katika levo za Kimataifa,” alisema Bab Tale.
KIBA ANAHUSIKA?
Alipotafutwa Kiba kuzungumzia suala hilo alikataa kuhusika nalo na kudai halina ukweli wowote kwani si rahisi kuwalipa pesa mashabiki wengi kiasi kile waliojitokeza uwanjani.
“Hiyo si kweli ni uzushi tu, sasa mimi nitawalipa nini hao mashabiki wote waweze kumzomea huyo Diamond? Siyo rahisi. Kwanza mimi nifanye hivyo ili iweje? Mimi si mtu wa kushindana na Diamond hata siku moja, nafanya muziki wangu, mashabiki wanauelewa, nashukuru Mungu kwa hilo,” alisema Kiba.
CLOUDS FM VS TIMES FM
Kwa upande mwingine, vita nzito ilizidi kutokota kupitia tamasha hilo baada ya msanii Davido kupanda jukwaani na kutumbuiza ilhali akiwa amewekewa pingamizi la kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) sambamba na zuio la Mahakama ya Kisutu lililowekwa na Redio Times FM waliodai kuwa na mkataba wa kufanya shoo na msanii huyo Novemba, mwaka huu Bongo.
TIMES WANASEMAJE?
Mkurugenzi wa Redio Times FM, Rehure Nyaulawa alipotafutwa kwa simu kuhusiana na suala hilo alisema mahakama ilishaweka pingamizi, anashangaa kuona msanii huyo alipanda jukwaani lakini akasema hawezi kukaa kimya, atakwenda mbele zaidi ili haki itendeke.
CLOUDS JE?
Kwa upande wao, Clouds walipotafutwa hawakupatikana hewani lakini kimsingi na wao wana hoja zao ambazo zitabainika pindi kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.
Hata hivyo, kuna madai kwamba, zuio la Davido kutopanda jukwaani Leaders Club lilipelekwa na mahakama kwa Clouds Media Group wakati Tamasha la Fiesta linaandaliwa na Kampuni ya Primetime Promotion, kwa hiyo barua hiyo ilikuwa ‘missing in action’.

KENYA::'Taulo Kenya zina ukimwi',asema mhubiri

Kituo kimoja cha televisheni nchini Marekani kinachorusha kila siku kipindi cha mhubiri Pat Robertson kiliomba radhi Jumatatu kwa madai yake potofu kwamba wasafiri wanaokwenda Kenya wanaweza kupata maambukizi ya Ukimwi kwa njia ya taulo.
"Dr Robertson alikosea kusema juu ya uwezekanao wa kupata Ukimwi kwa njia ya mataulo," kimesema kituo cha Utangazaji cha Kikristo, CBN, katika mtandao wa Facebook.
"CBN imegundua mara moja kosa hili na kuondoa kauli hiyo kutoka kwa maktaba ya mtandao huo. CBN inaomba radhi kwa mkanganyiko wowote."
Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 84, mwinjilisti mkongwe ameonya katika kipindi chake cha "700 Club" cha Oktoba 16 kwamba wasafiri watalazimika kuchukua tahadhari ya hali ya juu ya kiafya wawapo nchini Kenya.
"Unaweza kupata Ukimwi nchini Kenya," Bwana Robertson aliwaambia watazamaji wake wanaokadiriwa kufikia milioni moja. "Watu wana ukimwi. Unatakiwa kuwa makini. Nina maana kuwa, mataulo yanaweza kuwa na virusi vya Ukimwi."
Virusi vya HIV vinapatikana tu katika damu ya mwili na huenezwa tu kutoka kwa mwathiriwa
Madai ya Bwana Robertson haraka yalishambuliwa na makundi yanayojihusisha na masuala ya ugonjwa wa Ukimwi.
Wamesema kuwa Ofisi ya serikali ya Marekani ya Masuala ya Afya ya kina Mama inasema virusi vya Ukimwi haviwezi kuambukiza kwa njia ya "kushirikiana vyombo vya chakula, mataulo na mashuka, simu au vyoo ."
'Hatari ya kutembelea Kenya'
Matamshi ya Bwana Robertson yamekuja kutokana na swali alilotumiwa kwa njia ya barua pepe na mtu asiyejulikana ambaye alielezea wasiwasi juu ya madhara ya kutembelea Kenya wakati wa mlipuko wa Ebola barani Afrika.
Alimhakikishia mtazamaji wa kipindi chake kuwa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini Kenya akisema Kenya iko mbali na kitovu cha mlipuko wa Ebola, Afrika Magharibi.
Lakini Bwana Robertson alieleza hatari ya kuambukizwa magonjwa mengine nchini Kenya pamoja na Ukimwi.
Mbu wanaweza kusababisha madhara makubwa ya ugonjwa, amesema, akiongezea kwamba, "usafi akielezea kuwa tatizo lingine. Unakunywa maji, hayajachujwa, unaweza kupata ugonjwa wa matumbo"

NDANI::MADANSA WA DIAMOND WAKAMATWA,SARE ZA JESHI....


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' (wa pili kutoka kushoto), akiwa na madansa wake pamoja na Nay wa Mitego wakitoa burudani katika tamasha la Serengeti Fiesta 2014, Leaders Club jijini Dar.
Madansa wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinum wamekamatwa leo na wapo Kituo cha polisi cha Oyster Bay, Dar kwa kuvaa sare za JWTZ.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond'.
Wakati huohuo polisi  wanaendelea kumtafuta bosi wao, Nasibu Abudul ' Diamond Platinumz' kwa mahojiano naye kwa kuvaa sare za Jeshi hilo katika Tamasha la Serengeti Fiesta, lililofanyika Leaders Club, Dar usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita.
Meneja wa  Diamond, Babu Tale, hakupatikana kuzungumzia suala hili, juhudi za kumtafuta zinaendelea.
(HABARI NA MUSA MATEJA/GPL)

WEEEHH::Maajabu ya Ndege kugeuka mtu Nigeria

Mmoja wa waliomuangushia kichapo mwanamke huyo hadi akafariki
Kisa cha kushangaza kilitokea nchini Nigeria ambapo mwanamke mmoja alipewa kichapo cha mbwa hadi akafariki kwa madai ya yeye kuwa mchawi.
Mwanamke huyo inasemekana alikuwa Ndege iliyokuwa inaruka mtini kabla ya kugeuka na kuwa binadamu.
Umati wa watu ulikusanyika eneo alilokuwa mwanamke huyo baahi wakinasa matukio kwenye simu zao za mkononi. Polisi wawili walilazimika kurusha mabomu ya petroli kuwatawanya watu hao na kuwazuia kunasa picha za mwanamke huyo aliyekuwa anachapwa sana.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, mmoja alisema kuwa mwanamke huyo dakika chache zilizopita alikuwa Ndege mtini kabla ya kugeuka na kuwa mwanamke.
Ndege huyo alikuwa anazunguka mti mjini Oshodi , kisha akagonga mlingoti wa stima kabla ya kuanguka ardhini ambapo aligeuka na kuwa mwanamke.
Hii ni kwa mujibu wa wakazi wa mjini Oshodi wanaodai kuwa mwanamke huyo alikuwa mchawi.
'Kitu cha kushangaza'
''Ni kitu cha kushangaza lakini ni cha kweli,'' alisema bwana Sobowale.
"tulipozungumza na mwanamke huyo alidai kuwa na nguvu za kiganga, na kwamba alikuwa amewaua watu kadhaa. Aliongeza kuwa alikuwa anarejea kwa mumewe anayeishi katika eneo la Mushin kabla ya tyukio hilo. Baadhi ya watu walianza kumpiga picha. ''
Video ya umati huo ukimtandika mwanamke huyo imeenea kama moto msituni na kutazamwa na maelfu ya watu kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube.
Mwanamke huyo alikuwa uchi wa mnyama huku ngozi yake ikiwa inatoka baada ya kuchomwa.
Banke Idowu ni mmoja wa watu walionasa video ya mwanamke huyo akiwa anachapwa na umati na kwamba alikuwa amearifiwa na wenzake kuhusu mwanamke huyo alivyobadilika.
Aliambia BBC kuwa "sijawahi kuona jambo kama hili maishani mwangu,lakini nimesikia na kuona tu kwenye filamu kwa hivyo waliponiambia kuwa limetokea , mimi nimeamini. ''
Alisema angedhubutu kumuokoa mwanamke huyo umati huo ungemgeukia na yeye.
Polisi hawajuzungumzia tukio hilo, hususan kabla ya umati huo kukusanyika na kuanza kumchapa mwanamke huyo.
Alifariki mda mfupi baadaye huku mwili wake ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu.

GOOD KISSER OR::'Busu' lamtia mashakani Obama

Obama akibusu Cooper
Rais wa Marekani, Barack Obama, ametoa kauli yake kuhusu mwanamume aliyeshikwa na wivu baada ya yeye kumbusu mpenzi wake kwenye mashavu.
"rais tafadhali usimguse mpenzi wangu," alisema mwanamume, aliyetambuliwa na CNN kama Mike Jones.
Yote hayo yalitokea wakati Obama alipokuwa anapiga kura ya mapema katika jimbo la Illinois karibu na mwanamke aliyetajwa tu kama Aia Cooper.
''Kusema kweli sikuwa nimepanga kufanya hivyo,'' alisema Rais Obama , huku akiendelea kupiga kura yake huku Copper akiangua kicheko.
Baadaye Copper aliyeonekana kushikwa na aibu aliomba radhi kwa niaba ya mpenzi wake.
Obama alionekana naye kashikwa na aibu na kusema kwa tabasamu kuwa ,''hiki ni kisa tu cha mwanamume ndugu yangu kutaka tu kuniabisha bila sababu,''
Baada ya maongezi ya muda mfupi kati ya Obama na Cooper, wawili hao walimaliza kupiga kura, na kamera ikaonyesha Obama akimbusu Cooper mashavuni na kumpa mpenzi wa Coopper sababu nyingine ya kuongea.

MAAJABU::KUMBE BABA AKE ALIDAKA!

20_415e5.jpg