Tuesday, 28 October 2014

HABARI::Tanzania yakataa rasmi ndoa za jinsia moja kwenye agenda za maendeleo ya milenia

001
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba yake wakati akifungua warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.iliofanyika Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF)
Na Mwandishi wetu
SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.
“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy.
Amesema kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si agenda ya maendeleo.
002
Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini zinazoendelea.
Balozi Mushy aliongeza kwamba serikali ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Waziri husika kukataa shinikizo la kukubali swala ushoga kama agenda za maendeleo.
Amesema kwamba watanzania wanataka maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu, huduma bora za afya, miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa umaskini wa kipato.
Balozi Mushy alifafanua zaidi kwamba mambo ya ushoga na ndoa za jinsia yanakwenda kinyume na maadili ya watanzania, maisha, historia, utamaduni, mila na desturi za mtanzania sinakataza maswala ya ushoga.
Amesema kwamba serikali inatambua kwamba sheria ya mwenendo wa makosa ya kujamiiana yaliwekwa na mkoloni mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya Tanganyika imerithi kutoka kwenye serikali ya mwingereza.
003
Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.
“Watanzania na Afrika kwa ujumla inataka malengo ya millennia na haki za binadamu zizifike mahali kuwadharirisha watu kutoka bara hili kwa kuruhusu mambo yanayokwenda kinyume na historia yao, mila na desturi za mwafrika,”aliongeza.
Kwa upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano amesema kwamba malengo ya milenia kwa kiasi kikubwa yamefikiwa na Tanzania hasa katika upande wa elimu na kupunguza vifo vya wakinamama na watoto wakati wa kujifungua.
“leo tumekutana hapa kuzungumza ni kwa kiasi ngani nchi yetu ya Tanzania imefikia malengo ya milenia na changamoto ni zipi katika malengo mapya ambayo ni 17 badala ya 8 ya awali,” aliongeza
Dkt Mashindano alifafanua kwamba ni lazima sasa serikali kutazama katika Nyanja za ubora katika huduma hizi muhimu kwa jamii baada ya kufikia lengo la kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule kwa asilimia 85.
004
Mhadhiri wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
Aliongeza kwamba Tanzania na dunia kwa ujumla wameona ni muhimu kuweka agenda ya ubora katika kila agenda za malengo ya milenia kwa nchi zote ambao ni wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii, amesema kwamba malengo haya ya milenia ni lazima yaguse maisha ya watu katika ngazi ya chini ili matokeo chanya yaweze kuonekana kwenye jamii
Amesema kwamba ni lazima nchi zilizoendelea ziweke mkazo katika kuhakikisha kwamba nchini zinazoendelea zinajengewa uwezo wa kutafuta fedha za kutimiza malengo ya milenia.
005
Mdau akichangia mada yake.
006
Wadau wakifurahia jambo wakati ya warsha hiyo.
007
Wadau mbalimbali walioudhuria wakifuatilia mada mbalimbali.
008
009

SONGEA::JWTZ WATEGUA BOMU LILOTEGWA KATIKA ENEO LA KITUO CHA KURUSHIA MATANGAZO CHA TBC SONGEA

Bomu lililotengenezwa kienyeji  kama linavoonekana katika picha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa mtaaram wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili.

Hili ni eneo la tukio ambalo limezungushiwa mkanda huu wa pilisi uliandikwa hairuhusiwi kupita eneo hili,Lakini chini ya huo mti kama inavoonekana katika picha kukiwa na udongo umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa bomu hili la kutengenezwa kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa Usalama barabarani kwa kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa kazini
Bomu lililotengenezwa kienyeji
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiwa anaonyesha umahili wake alionao aweze kulitegua bila kuleta madhara yoyote yale katika jamii(Picha na demasho.com)
-------------------------
 Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia matangazo kilichopo mshangano cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja jioni.

Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji nawatu wasiojulikana lilitegwa hatua  zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao za kila siku.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu wa milipuko kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili linaonekakana limetengenezwa kienyeji.
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi watatu  wakiwa katika doria katika kata ya misufini manispaa ya songea.

Msikhela amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwapata watu hawa wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji, Aidha ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze kuwabaini watu wanaousika na matukio ya namana hii.

Na hii ni mara ya pili katika manispaa ya songea kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,  walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini songea mkoani Ruvuma.

Askari hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika doria ambao ni WP Felista Abel, PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na mtandao huu wa demasho  kwa njia ya simu amesikitishwa na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani iliyopo katika mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata walewote wanaohusika na vitendo hivi.

Monday, 27 October 2014

UDAKUZZZ::ROSE NDAUKA HAKAMATIKI

Stori: Musa Mateja
Acha kabisa! Baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba’ke, Malick Bandawe kisha kurudi kwao, Kigogo jijini Dar, staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka anadaiwa hivi sasa hakamatiki hivyo hakauki viwanja.
Staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka akiinjoi uhuru wa kuwa 'Single' Viwanja.
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ambalo limekuwa likimnyatia kwa ukaribu Rose unaonesha kwamba tangu ametengana na mwanaume huyo amekuwa huru kupita maelezo huku akionesha jeuri ya fedha kama ilivyokuwa kwa mastaa wenzake, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja.
Rose Ndauka akianza kukata mauno.
Pia uchunguzi huo ulibaini kwamba, mara tu baada ya kutoka ‘kifungoni’, Rose aliangusha bonge la sherehe ya ‘bethidei’ yake ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na ndiko alikoanza kuonesha jeuri ya fedha.
Rose Ndauka akimwagia midolari mtangazaji wa Times FM, 'Dida'.
Data zilionesha kwamba siku tishio ni ile ya Oktoba 18, mwaka huu ambapo Rose alikuwa kinara wa ushangiliaji wa timu yake ya Yanga, jambo ambalo siku za nyuma alikuwa hafanyi hivyo.
Siku hiyohiyo, baada ya kutoka uwanjani alikwenda kubadilisha mavazi yake ya njano na kijani kisha akatupia pamba za kuruka viwanja, akaibuka katika Tamasha la Fiesta kwenye Viwanja vya Leader, Kinondoni jijini Dar.
Rose Ndauka akiendeleza mauno.
Akiwa ndani ya Leaders, Rose aliambatana na Mtangazaji wa Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ ambapo alikuwa akihaha kumnasa mwanamuziki wa Marekani, T.I aliyetimba Bongo kutumbuiza kwenye tamasha hilo.
Kama hiyo haitoshi, Alhamisi iliyopita, Rose alithibitisha kwamba kwa sasa hashikiki kwani alitimba kwenye pati ya bethidei ya shoga’ke, Dida iliyofanyika nyumbani kwake, Mwananyamala, Dar ambapo alikuwa kinara wa kujiachia kwa kusakata muziki na kumwaga ‘madolari’.
Wasanii wa Bongo Movies 'Riyama' na 'JB' wakiwa na Rose ndauka katika Viwanja hivyo.
Ulipofika muda wa muziki, hapo ndipo Rose alipopagawa na kujikuta akikata mauno huku akipiga kelele ‘raha jipe mwenyeweee…’
Mwanahabari wetu alipotaka kujua kulikoni Rose kujiachia kiasi hicho, aliomba aachwe afurahie maisha.

#BBA:::KWAHERIIII

UMOJA HUO::NYOMI LA JANGWANI....


 

USAFI:::TATIZO LA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA MWILINI

Harufu mbaya ni kitu kisichompendeza mtu yeyote. Unapotoa harufu mbaya toka mwilini mwako, haikupendezi wewe mwenyewe wala mtu wa jirani. Kama kitu hukipendi wewe na ukakiona hakifai basi usimlazimishe mwenzio akipende au akione cha kawaida.
Harufu mbaya mwilini inatoka maeneo yote ya mwili kuanzia kichwani hadi miguuni.
Zipo sababu nyingi zinazomfanya mtu atokwe na harufu mbaya, inaweza kuwa uchafu, maradhi au maumbile.
Hali ya uchafu ipo wazi endapo mtu haogi, hafui au hanawi. Uchafu wa kichwani inaweza kuwa nywele au wigi au kitu chochote kinachowekwa kichwani.Uchafu unaweza kuwa maeneo mbalimbali ya mwili.
Maradhi ya ngozi, kansa au vidonda vyenye maambukizi vinaweza kusababisha kutoa harufu mbaya au vitambaa vilivyofungiwa vidonda.
Kwa hiyo kundi la maradhi ni pana kwa kuwa tatizo la ngozi pekee linaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa.
Sababu za kimaumbile linawahusu zaidi watu wanene ingawa hata wembamba pia wanaweza kupatwa na tatizo hili kutegemea na harufu inatoka eneo gani la mwili.
Watu wanene hupatwa na matatizo ya kutoa harufu mbaya kama hawatazidisha usafi na kuhakikisha miili yao sehemu za mikunjo inakuwa mikavu. Sehemu hizo ni chini ya kifua au matiti, nyama za tumboni, chini ya tumbo, mbavuni, sehemu za siri na mapajani.
Unene pamoja na matatizo mengi yanayoweza kujitokeza pia huweza kusababisha magonjwa ya ngozi na kutokwa na jasho lenye harufu kali.
MAENEO YANAYOTOA HARUFU MBAYA
Sehemu yoyote ya mwili inaweza kutoa harufu mbaya kama tulivyoona hapo mwanzoni kuanzia kichwani hadi miguuni. Lakini yapo maeneo kama masikioni na puani pia harufu mbaya hutoka. Harufu za maeneo hayo mara nyingi haziwi kali.

KUTOKWA HARUFU MBAYA KINYWANI
Tatizo la kutokwa na harufu mbaya mdomoni au kinywani hutokana na matatizo mbalimbali kama kuwa na meno mabovu, magonjwa ya fizi, ulimi, fangasi za kinywani na uchafu kutokana na kutosafisha kinywa vizuri.
Wapo watu ambao kwa asili hutoa harufu mbaya kinywani pasipo kuwa na magonjwa ya kinywa na huwa makini kusafisha kinywa, lakini harufu haiishi.
Tatizo hili hutibika baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina katika tabaka linalotandika ndani ya kinywa.
Wakati mwingine harufu mbaya ya kinywa husababishwa na ulaji wa vyakula, unywaji pombe, uvutaji wa sigara, bangi na ugoro.
KUTOKWA NA HARUFU MBAYA KWAPANI
Kutokwa na harufu mbaya kwapani au kunuka kikwapa inatokana na mambo mbalimbali hata kama unajisafisha mara kwa mara na kutoa vinyweleo vya kwapani.
Harufu ya kikwapa husababishwa na njia ambazo ngozi ya kwapani hupumua zinaziba, hivyo kusababisha njia za kutolea jasho kuwa chache na jasho kutoka kidogo kidogo na kujaa kwapani.
Hivyo kujaa na kulowesha nguo sehemu hizo, hali hii ikiendelea kwa muda mrefu husababisha bakteria aina ya ‘staphylloccocus’ kuanza kuishi hapo na jasho linalojirundika kukauka na kuganda, hivyo kutoa harufu mbaya.
Tatizo la kikwapa likiendelea kwa muda mrefu baadhi ya njia za jasho huziba kabisa na bakteria kujipenyeza. Hapo ndipo unaweza kusumbuliwa na majipu ya mara kwa mara kwapani, kutokwa na vipele vikubwa kwapani na muwasho mkali baada ya kunyoa kwapani na hata vidonda vidogovidogo.
Matumizi ya baadhi ya pafyumu husababisha mzio ambapo kwapa litawasha sana kila wakati au utatokwa na vipele vingi au ngozi ya kwapani inabadilika na kuwa nyeusi sana huku ikitoka harufu mbaya. Tatizo hili linaweza kutibika hospitali.
HARUFU MBAYA SEHEMU ZA SIRI
Harufu mbaya sehemu za siri inaweza kuwa kwa wanaume na wanawake. Zipo sababu mbalimbali kwa wanaume ambazo zinahitaji uchunguzi wa kina na tiba.
Kwa wanawake harufu inaweza kutoka ukeni ikiambatana na uchafu au la. Harufu ya ukeni huwa mbaya inayofanana na shombo la samaki hutokana na kutokuwa makini kiusafi.
Maambukizi ya fangasi na bakteria, magonjwa ya zinaa, kisonono na kaswende ni sababu mojawapo.
Wapo wanawake ambao hutokwa na harufu sehemu za siri kutokana na mikunjo ya kwenye mapaja yao, hasa kwa wale wanene. Harufu pia inaweza kutoka katika sehemu ya haja kubwa na hii ni ya kinyesi endapo hutanawa vizuri au kuwa na maradhi sehemu hiyo.
NINI CHA KUFANYA?
Endapo utakuwa na tatizo hili la kutoa harufu mbaya maeneo tofauti ya mwili au unahisi mwenzio ana tatizo hili na anakukwaza, inashauriwa uwaone madaktari katika hospitali za wilaya kwa uchunguzi wa kina.
Tatizo hili linatibika na hupotea kabisa na kukuacha huru. Tatizo la kutokwa na majipu, vipele, kubadilika rangi ya ngozi kwapani, chini ya matiti na sehemu za siri, pia linatibika kabisa endapo utawaona wataalamu. Wahi mapema hospitali.

BURUDANI>>JOKATE: HAKUNA KAMA DIAMOND

Stori: Waandishi Wetu
Jumamosi iliyopita, Oktoba 25, 2014 ilikuwa ni Siku ya Msanii Duniani ambayo kwa mara ya kwanza, Tanzania iliiadhimisha siku hiyo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Gharib Bilal.
Dr Chris Mauki na Jokate Mwegelo walikuwa washehereshaji wa tamasha hilo kwenye Ukumbi wa Mlimani City uliopo Dar es Salaam.
Siku hiyo ilipambwa na matukio kibao nyuma na mbele ya pazia, ambapo kubwa lilikuwa ni la Jokate Mwegelo ambaye alikuwa miongoni mwa ma-mc wa shughuli hiyo ya kitaifa, kumfagilia waziwazi msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwamba hakuna kama yeye, Ijumaa Wikienda lilikuwa ndani ya nyumba na kunasa matukio lukuki yaliyojiri.

Mc Jokate Mwengelo (kulia) akikata mauno baada ya burudani kumnogea.
SHUGHULI YAANZA
Kwa kuzingatia itifaki, ukiacha waalikwa wengine, kiongozi aliyeanza kutimba alikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia na baadaye alifuatiwa na Dk. Bilal ambapo shughuli hiyo ilifunguliwa rasmi.
Kikundi cha ngoma za kinyeji kikitoa burudanu usiku huu Siku ya Msanii Mlimani City.
MA-MC
Washereheshaji wa shughuli hiyo walikuwa ni Chriss Mauki na Jokate Mwegelo ambao walifanya vizuri lakini mwanzoni kidizaini f’lani Jokate alionekana kuwa na kigugumizi na baadaye akatengeneza vichwa vya habari kufuatia kitendo chake cha kumsifia Diamond.
BURUDANI ZA AWALI
Katika burudani za mwanzo, kulikuwa na vikundi vya kudansi kisha ngoma ya asili kutoka Ukerewe ikafuatia, baadaye ikaja Bendi ya Mashauzi Classic chini ya Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ ambayo haikuamsha kama ilivyozoeleka.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akifanya yake.
TUZO ZAANZA KUTOLEWA
Tuzo ya kwanza kutolewa ilikuwa ni ya Msanii Aliyejitolea Maisha yake Yote Katika Sanaa ambayo ilikwenda kwa mchora katuni mahiri aliyechora michoro ya Tingatinga.
Tuzo ya pili ilikwenda kwa Msanii Aliyetoa Mchango Mkubwa kwa Jamii ambapo aliyeibuka kidedea ni Joseph Kanuti.
BURUDANI TENA
Baada ya tuzo hizo mbili, burudani iliendelea tena ambapo Ako Mpiluka Band walionesha mbwembwe za kucheza na moto na kuwakosha mashabiki waliohudhuria.
Diamond Akicheza na wanenguaji wake.
DIAMOND STEJINI
Baada ya Mpiluka Band, staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz alitimba stejini ambapo aliangusha bonge la shoo mbele ya makamu wa rais na kushangiliwa.
Wakiendelea kucheza wimbo wa 'Mdogomdogo'.
Huku Diamond akiimba nyimbo zake nyingi za zamani, zile zomeazomea kama zilizotokea Fiesta zilizodaiwa kuwa ni kutoka kwa ‘Team Ali Kiba’, zilizimwa na uwepo wa makamu wa rais aliyeonekana kumkubali msanii huyo kwa kutingisha kichwa wakati anafanya shoo na sapoti kubwa aliyoipata kutoka kwa Jokate aliyeimba naye Wimbo wa Nimpende Nani.
Isha Mashauzi akifanya yake na wacheza shoo wake.
JOKATE: HAKUNA KAMA DIAMOND
Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, Jokate alimfagilia waziwazi Diamond na kusema hakuna msanii anayeweza kumiliki jukwaa kama yeye.Sifa hizo alizozitoa Jokate kwa Diamond, zilisababisha ukumbi mzima ulipuke kwa kelele hasa ukizingatia kuwa wawili hao walishawahi kuwa wapenzi ila wakatengana na kile kinachodaiwa kuwa ni maneno ya watu.
Ukichanganya na kilichotokea kwenye Serengeti Fiesta 2014 ambapo Diamond ‘alikula za uso’ ukilinganisha na mpinzani wake, Ali Kiba ambaye alishangiliwa kwa nguvu, kitendo cha Jokate kumnadi Diamond jukwaani kilizidi kutengeneza vichwa vya habari.
DIAMOND ASAFISHA NYOTA
Baadaye Diamond aliangusha Number One na Mdogomdogo ambazo ziliwafanya watu wachizike hivyo kudaiwa kusafisha nyota yake iliyochafuka hivi karibuni kwenye Tamasha la Fiesta katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar alipozomewa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiongea jambo usiku wa kuamkia jana Mlimani City katika Siku ya Msanii.
DK BILAL AONDOKA
Baada ya neno kutoka kwa waandaaji, Waziri Nkamia alimuaga Dk. Bilal ambaye aliondoka ukumbini humo baada ya kukabidhi kitita cha Sh. milioni tano kwa kila mshindi wa tuzo mbili zilizotolewa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akiongea na wasanii katika Siku ya Msanii.
NJENJE WAKONGA NYOYO
Baada ya Dk. Bilal kusepa, burudani iliendelea ambapo Kilimanjaro Band ‘Wananjenje’ walikamatia jukwaa na kukonga vilivyo nyoyo za wahudhuria.
Waimbaji wanaounda kundi la Yamoto Band Aslay, Becka, Bella na Maromboso wakitoa burudani.
JOKATE AKATA MAUNO
Katika shoo ya Njenje, mwimbaji wake mashuhuri, Nyota Waziri alikuwa akitembea ukumbini kuwakatisha mauno wahudhuriaji na kuwataka wataje mahali wanakotokea  ambapo alipofika kwa Jokate, staa huyo alionesha umahiri mkubwa wa kukata mauno huku akijinadi kwamba anatokea Songea.
KOMEDI KUTOKA NAIROBI
Kilichofuata baadaye ni Kundi la The Omonds kutoka Nairobi, Kenya kupanda jukwaani na kuangusha komedi zilizowavunja mbavu wengi.
Baadaaye, ma-mc, Mauki na Jokate walipata nafasi ya kuzungumza chochote kabla ya kuwakaribisha Yamoto Band waliomaliza shughuli hiyo kwa kukamua ngoma zao kali zinazokimbiza mtaani kwa sasa.
Kwa picha zaidi angalia Uk. 8.
Imeandaliwa na Erick Evarist, Musa Mateja, Andrew Carlos, Nicolaus Trac na Dennis Mtima.

SHARIA:::wanawake wa Saudia waamua

Najla Hariri akiendesha gari kinyume na sheria inayomzuia kufanya hivyo
Harakati za kutetea haki za wanawake nchini Saudi Arabia kutaka na wao wapewe haki ya kuendesha magari kama wanaume zashika kasi kubwa, sasa wanaadhimisha mwaka mmoja wa kupinga amri ya kwatazo kwa wanawake wasiendeshe magari na wanawake wanapinga na kuendesha magari kinyume na amri waliowekewa.
Kwenye mitandao ya kijamii kumetolewa miito kadhaa ya kuwataka wanawake wapinge amri hiyo kwa wingi na waendeshe magari,wanaharakati wanaopinga amri hiyo wameiambia BBC kuwa harakati zao zinaendelea vizuri na mwito umepokelewa vyema ingawa mwaka huu utatumika kuongeza uelewa zaidi juu ya suala hilo.
Nayo mamlaka ya Saudi Arabia imetoa onyo kali na kuwataka wasaudia wote wasijihusishe na mgomo huo,na mmoja kati ya wanaharakati ambaye ana ushawishi mkubwa ameelezea mgomo huo uloanza mwaka wa jana kuwa umeitia hofu kubwa serikali ya nchi hiyo.

DARASA::NINI CHA KUFANYA WAZAZI, NDUGU WANAPOMCHUKIA UMPENDAYE?

Je, upo kwenye uhusiano wa kimapenzi, unampenda sana mume, mke, mchumba au mpenzi uliyenaye lakini wazazi au ndugu zako wanamchukia na kila siku wanampiga vita?
Mada ya leo ni kwa ajili ya wewe msomaji wangu ambaye upo kwenye mazingira kama haya ya wazazi au ndugu kumkataa umpendaye kwa sababu ambazo wanazijua leo. Kwa ambao wamewahi kupitia changamoto hii au bado wapo ndani yake, watakuwa wanaelewa vizuri ugumu uliopo linapokuja suala kama hili.
Wazazi wako wamekuzaa na kukulea tangu ukiwa mdogo mpaka umekuwa mkubwa, umempata umpendaye lakini wao wanamkataa na kukwambia unatakiwa kuchagua moja, wao (wazazi) au huyo unayempenda. Utachukua uamuzi gani? Utamuacha kwa sababu wazazi hawampendi? Utakubali kuwadharau wazazi wako na kuendelea naye?
Bila shaka kila mmoja atakuwa na jibu lake tofauti, hata mimi ukiniuliza nitakuwa na jibu langu lakini tunachokihitaji hapa, ni kujadiliana, kupanuana mawazo, kupeana uzoefu ili mwisho kila mmoja awe na uwezo wa kuivuka changamoto hii kwa sababu hata kama bado haijakukuta, huenda ipo siku na wewe yatakutokea.
MFANO HAI
Hebu soma ushuhuda wa msomaji wangu mmoja ambaye yupo kwenye hali mbaya na anahitaji ushauri:
“Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 42, nilioa miaka kumi iliyopita na tumejaliwa kupata watoto wawili. Tatizo linalonisumbua na kuniweka njia panda, mke wangu anawachukia sana wazazi wangu na ndugu wote kutoka upande wangu.“Wazazi wangu wamekuja mjini kwa zaidi ya miezi miwili sasa kwa ajili ya matibabu lakini huwezi kuamini, mke wangu anawachukia kiasi kwamba hata salamu kwake ni mtihani. Anawadharau, wanapishana ndani kama wake wenza, anazungumza maneno machafu dhidi yao ambayo mengine nayasikia, hawapi matunzo mazuri, anawanyanyasa na kibaya anawafundisha mpaka wanangu kuwadharau babu na bibi.
“Hali hiyo imesababisha wazazi nao waanze kumchukia sana, wananiambia nimekosea kuchagua mke na wananitolea maneno makali ambayo mengine hayaandikiki. Nipo njia panda, sijui niamue nini, bado nampenda mke wangu lakini mambo anayoyafanya yamesababisha mapenzi yangu kwake yapungue mpaka nafikiria kumpa talaka ili kuwafurahisha wazazi wangu. Naomba ushauri, nifanyeje?”
Amehitimisha msomaji wangu huyu, bila shaka umemuelewa. Najua huyu ni mmoja tu lakini wapo wengi ambao wanatokewa na visa kama hivi. Naomba tujadiliane pamoja, ungekuwa ni wewe kwenye nafasi ya msomaji huyu, ungefanya nini? Kama ungepewa kazi ya kumshauri, ungemwambia nini?
TAFUTA CHANZO CHA TATIZO
Hakuna chuki ambayo huwa haina chanzo. Kama mumeo, mkeo anawachukia ndugu zako, jambo la kwanza ambalo unatakiwa kulijua, ni kwamba lazima kuna chanzo kilichosababisha hali hiyo. Na kama yalivyo matatizo mengine yote, huwezi kupata muafaka kama hujakijua chanzo.
Wengi hushindwa kutumia busara katika kutafuta chanzo. Yawezekana umpendaye ndiyo chanzo ila kwa sababu ya mapenzi yako kwake, unaukataa ukweli na kumtetea.

UMOJA NI NGUVU::Upinzani TZ waungana kuing'oa CCM


Wabunge wa TZ, ambao baadhi yao wa upinzani wameungana, kuing'oa CCM.
Upinzani nchini Tz umetia saini makubaliano ya pamoja, kuking’oa madarakani Chama tawala.
Utiaji huo saini makubaliano ya kukishinda Chama cha Mapinduzi CCM, katika uchaguzi ujao, umefanywa na viongozi wa vyama vinne, huku tukio hilo likishuhudiwa na wafuasi wao.
Katibu Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Dr. Willibrod Slaa ni miongoni mwa viongozi waliotia saini makubaliano hayo na amesema vyama hivyo vitasimamisha wagombea wake kwa pamoja kwenye ngazi zote za uchaguzi kuanzia serikali za mitaa mpaka ngazi ya urais.
Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim seif Sharif Hamad anasema tukio hilo la vyama kusaini makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kuing’oa CCM ni muhimu na la kihistoria.
Viongozi waliotia saini waraka huo wa makubaliano ni Freeman Mbowe Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Profesa Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF, Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye pia ni Makamu wa kwanza rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, James Mbatia Mwenyekiti NCCR Mageuzi, Mosena Nyambabe Katibu Mkuu NCCR Mageuzi, Dr Emmanuel Makaidi Mwenyekiti NLD na Tozzi Matwanga Katibu Mkuu wa NLD.

UTATA::LUNDENGA AKANUSHA MISS TANZANIA KUJIUZULU



HMB_3760
Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, amekanusha uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo, kuwa Sitti Abbas Mtemvu (pichani katikati) amelazimika kuvua taji la Uremo la Tanzania (Redd’s Miss Tanzania 2014).Uvumi wa Sitti kuvua taji hilo umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia akaunti ya Facebook mrembo huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, akisema kutokana na vidole vya lawama anavyooshewa kiasi cha kuosa amani, amelazimika kuvua taji ili awe huru.

“Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.
misstz1
Akizungumzia uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa hiyo, na kwamba kama lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu kampuni yake, inayoratibu kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20 mwaka huu.
“Hakuna taarifa iliyotufikia hadi sasa kuhusiana na taarifa hizo. Sitti anajua anapaswa kufanya nini kama anaamua kulitema taji, ambapo anapaswa kutuarifu sisi kabla ya kuripoti hilo mahali popote. Kwa kuwa hajafanya hivyo, tunaamini hilo halipo nab ado tunamtambua kuwa mrembo wetu,” alisema Lundenga.
Kwa upande wa mama wa mrembo huyo, alisema ameshtushwa na taarifa za mwanaye kujiuzulu na kusema si za kweli, kwani kama angepanga kufanya hivyo asingefanya kwa kificho, badala yake angeitisha mkutao na wanahabari: “Hawezi kujiuzulu kienyeji hivyo na hata mimi mama yake sina taarifa hizo, hayo ni matumizi mabaya ya mitandao.

TAHADHARI::NJIA 5 ZA KUEPUKA VIRUSI HATARI VYA EBOLA





Njia za kuepuka kuambukizwa Ebola
Ebola:Njia tano za kujiepusha virusi hatari vya homa ya Ebola

Ebola ni mojawapo ya virusi hatari zaidi ulimwenguni lakini haiambukizwi kupitia hewa, hivyo basi huwezi kuambukizwa Ebola kama homa ya kawaida.
Madaktari wanasema kuepuka Ebola ni rahisi sana iwapo mtu atafuata tahadhari hizi muhimu zaidi:
1. Sabuni na maji
Nawa mikono kila baada ya shughuli yeyote kwa kutumia sabuni na maji safi- na utumie taulo kujikausha.
Hili huwa jambo gumu kwa wanaoishi kwenye makazi duni, na walio vijijini ambako aghalabu maji safi hayapatikani moja kwa moja- lakini ni mbinu iliyothibitishwa ya kuua virusi vya Ebola.

Osha mikono kwa sabuni na Maji
Unachohitaji tu ni sabuni ya kawaida.
Kusalimiana kwa mikono kunafaa kuepukwa kwa ujumla, daktari Unnis Krishnan wa Plan International aliarifu BBC, kwani Ebola husambazwa haraka watu wanapowasiliana ana kwa ana na maji maji ya kimwili ya waliougua.
Dalili ya ugonjwa huu huchukuwa muda kabla ya kudhihirika.
Tumia njia zingine za kujuliana hali
2. Hakuna kugusana
Iwapo unashuku kuwa mtu ana Ebola, usimguse.
Inaokena kuwa si maadili mema unapoona unaowapenda wakihisi uchungu na unataka kuwakumbatia na kuwahudumia, lakini maji maji ya kimwili- mkojo na kinyesi, matapishi, kamasi, mate, machozi, na mbegu za kiume na majimaji ya uke- vyote huweza kueneza Ebola.
Dalili za mtu aliyeugua ni joto mwilini, maumivu kwa misuli na viungo, vidonda kooni, kuumwa na kichwa, na uchovu- kufuatiwa na kichefuchefu, kutapika, na kuharisha, ambapo mtu huweza kutoa damu pia.

Usimguse mtu anayeonesha dalili za ugonjwa
Tia watu hao moyo kutembelea kituo cha afya haraka iwezekanavyo.
Pia ni uamuzi mzuri usiguse nguo au malaza ya waliougua Ebola- na Medecins Sans Frontieres anashauri kuwa malazi ya waliougua yanafaa kuteketezwa.
3. Epuka miili ya wafu
Iwapo unadhani mtu amefariki baada ya kuugua Ebola, usiguse mwili wao, hata kama ni mila au desturi ya maziko.
Baada ya mtu kufa, bado unaweza kuambukizwa Ebola kutoka kwa miili yao kwani bado inatoa maji maji ya mwili ambayo huweza kuwa hatari zaidi hata kuliko ya mtu alieugua.
Fanya mipango kupata timu ya magwiji kushughulikia mwili huo haraka iwezekanavyo kwani ni hatari kuwacha mwili wa mfu kwa muda mrefu katika eneo la makazi.

Usile nyama ya porini
4. Usile nyama ya porini
Epuka kuwinda, kugusa, au kula nyama ya porini, kwa mfano popo, nyani na sokwe, kwani wanasayansi wanaamini kuwa hiyo ndiyo chanzo cha maambukizi kwa binadamu.
Hata kama mnyama fulani wa porini huliwa katika eneo lenu na nyama yake ni tamu epuka myama huyo kwani nyama yake au damu yake huweza kuwa na virusi hivyo.
Hakikisha vyakula vyote vinapikwa inavyostahili.

Usieneze uvumi kuhusu Ebola
5. Usiwe na hofu
Kueneza uvumi huongeza hofu.
Usiogope wafanyakazi wa huduma za afya- wako hapo kukusaidia na kliniki ndipo mahali mwafaka kwa mtu kuponywa- wataongezewa maji na kutulizwa maumivu.
Takriban nusu ya watu walioambukizwa Ebola kufuatia mzuko wa hivi punde wa Ebola walifariki.
Kumekuwepo na matukio ya madaktari kushambuliwa na watu kutorokwa wanaposhukiwa kuwa na Ebola- hata wakati wanaugua ugonjwa tofauti.
Kuamini matibabu ya kiasili ambayo hayajathibitishwa kutoa afueni, pia kumechangia ongezeko la kuenea kwa virusi vya Ebola.
"Kinga ndiyo jinsi bora zaidi ya kukabiliana na Ebola, hivyo basi wacha uvumi na usiwe na hofu; inawezekana kupunguza maumivu na kuokoa maisha,” daktari Krishnan asema.
Ugonjwa wa virusi vya Ebola (EVD):
Dalili za Ebola ni homa, kufuja damu na kuharibika kwa mfumo mkuu wa neva.

Epuka miili ya watu walioambukizwa Ebola
Maafa ya ugonjwa huu huweza kufika asilimia tisini- lakini mzuko wa hivi punde unasababisha maafa 55% .
Ugonjwa huo huchukua muda wa siku ishirini na moja kukomaa.

Hakuna kinga wala tibaHuduma za msaada na kudhibiti kupoteza maji mwilini kutokana na kuharisha au kutapika husaidia katika kuponaInafikiriwa kuwa popo ndo vilemea vya ugonjwa huo.CHANZO BBC SWAHILI

HABARI::WAZIRI MKUU: SERIKALI KUOMBA MKOPO POLAND

*Ni wa kujenga maghala makubwa ya kuhifadhia chakula
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali inaangalia uwezekano wa kupata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland utakaoliongezea Taifa uwezo wa kuhifadhi chakula tofauti na hali ilivyo sasa.

Alisema uzalishaji mwaka huu umetoa ziada ya tani milioni 1.5 za nafaka na tani 800,000 za mpunga ikilinganishwa na ziada ya tani 300,000 iliyokuwepo mwaka jana. “Serikali inakabiliwa na changamoto ya kupata soko la uhakika kwa mazao ya wakulima kwa sababu tulizoea kumtumia Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kama mnununzi mkuu na uwezo wezo wake ni tani 240,000 tu kwa mwaka,” alisema.
Akizungumza baada ya kutembelea kampuni ya MLYNPOL ambayo inanunua mazao kwa wakulima na kusindika nafaka jana mchana (Ijumaa, Oktoba 24, 2014) Waziri Mkuu alisema teknolojia ya ujenzi wa maghala makubwa ya kuhifadhia chakula katika muda mfupi ndiyo suluhisho pekee kwa wakulima wa Tanzania katika kipindi tulichonacho.
“Wenzetu wana teknolojia ya kisasa ya ujenzi wa SILOS (maghala makubwa ya kuhifadhia chakula) pamoja na namna bora ya kuhifadhi chakula, na sisi tuna changamoto ya kuwasadia wakulima kuuza mazao kutokana na uzalishaji mkubwa wa nafaka ambao umetokea mwaka huu,” alisema.
Alisema ni mapema mno kujua kiasi cha fedha ambacho Serikali inatarajia kukopa lakini alithibitisha kwamba atatuma timu ya wataalamu kutoka sekta husika ili wafanye mazungumzo rasmi na Serikali ya Poland na kukamilisha taratibu za upatikanaji wa mkopo huo.
Waziri Mkuu ambaye alisafiri km. 500 kwenda mji wa CHOJNOW kilipo kiwanda cha kutengeneza maghala (SILOS) na kusindika nafaka aliguswa na teknolojia inayotumika kwenye kiwanda hicho cha MLYNPOL ambapo kwa siku moja kina uwezo wa kusindika tani 360,000.
Mji wa CHOJNOW upo kusini Mashariki mwa Poland na pia hauko mbali na mipaka ya nchi za Ujerumani, Czeck na Austria. Kwa gari dogo ni kati ya saa 3 hadi 4 hadi kufika miji mkuu ya nchi hizo ambayo ni Berlin, Prague na Vienna.
Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, mmiliki wa kiwanda hicho kikubwa nchini Poland, Bw. WITOLD KARCZEWSKI alisema kiwanda hicho kinaposindika ngano kina uwezo wa kutoa unga laini wa mikate (refined flour), unga wa lishe (grain/brown flour), unga wa kutengeneza pasta na tambi na wa mwisho hutolewa kwa ajili ya chakula cha mifugo.
“Nafaka zikifika, zinasafishwa, zinakaushwa, zinapimwa unyevunyevu uliopo na kuanza kusindikwa kulingana na aina ya nafaka inayoletwa. Tunakusanya mazao haya kutoka kwa wakulima kwenye majimbo 16 ya nchi hii,” alisema.
Akifafanua kuhusu matumiai ya umeme kwenye kiwanda hicho, Bw. ALEKSANDR ZINGMAN ambaye pia ni mshauri na mbia wa Bw. KARCZEWSKI, alisema kiwanda hicho kinatumia megawati moja ya umeme kwa saa moja lakini matumizi yanaweza kupungua kuligana na ukubwa ama udogo wa kiwanda.
“Kama Serikali inahitaji kiwanda kidogo zaidi ya hapa, tunaweza kuwajengea na matumizi ya umeme lazima yatapungua,” alisema.
Kampuni ya MLYNPOL ina wafanyakazi 250 ambao kato yao, 200 wanafanya kazi kiwandani kwa shifti tatu za saa nane nane kila moja.
Waziri Mkuu anamalizia ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara wa jiji la Warsaw. IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU,

SIASA::DK.SHEIN AHUTUBIA MKUTANO WA CCM KIBANDA MAITI UNGUJA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja leo.[Picha na Ikulu.]unnamed1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyeekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafya Silima,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakifuatana katika mkutano hadhara uliofanyika leo katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja,[Picha na Iku
Wananchi na WanaCCM waliofirika katika viwanja vyaDemokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja wakiwa katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo ambao umeweka bayana na kufanya uchambuzi baadhi ya vifungu vya katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.[Picha na Ikulu.] unnamed 
Wananchi na WanaCCM waliofirika katika viwanja vyaDemokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja wakiwa katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo ambao umeweka bayana na kufanya uchambuzi baadhi ya vifungu vya katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.[Picha na Ikulu.]  unnamed3 
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais Mama Pili Balozi wakiwa katika Mkutano wa Hadhara katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja leo uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyeekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  .[Picha na Ikulu.]