Tuesday, 28 October 2014

NIGERIA::Unafahamu kilichoandikwa kwenye mitandao ya kijamii Nigeria kuhusiana na msanii Wizkid? Kisome hapa.

Taarifa zilizoenea mitandao mbali mbali ya Nigeria saa chache zilizopita zinazungumzia tukio kutoka Kenya linalohusiana na kukamatwa kwa msanii wa Nigeria Wizkid ambaye alishikiliwa na na jeshi la Polisi nchini humo saa chache kabla ya kupanda ndege kurejea Nigeria.
Taarifa iliyoandikwa na Standard Digital Kenya imesema, Wizkid alikamatwa hotelini Nairobi Crown Plaza ambapo amekaa kwa takribani wiki moja baada ya kufanya onesho lake.
Kwa mujibu wa habari kutoka chanzo hicho, Wizkid alikamatwa kwa kosa la kuvuta bangi hotelini hapo na baada ya mzozo wa muda mrefu baina yake na mhudumu wa hoteli hiyo, mhudumu wa hoteli alitoa taarifa polisi ambao walimkamata na kumfikisha kituo cha Capital Hill ambapo alipigwa faini ya sh. 50,000 za Kenya kwa kosa hilo na baadaye kuachiwa huru.
Wizkid alikamatwa hotelini hapo siku ya jumamosi kwa kosa hilo, ambapo Victoria Kimani, msanii wa Kenya ambaye wamefanya kolabo hivi karibuni ametajwa kuhusika kumtoa Wizkid kutoka kituo cha Polisi.

MTANDAONI::Soma hapa alichokiagiza Zitto Kabwe kwa CAG na BoT leo..

 Taarifa zilizotufikia hivi punde zimesema Kamati Ya Hesabu za Serikali (PAC) Tanzania imeagiza ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kufanya ukaguzi wa mchakato wa ubinafsishaji wa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali Zitto Kabwe, kupitia ukurasa wake wa Instagram (@zittokabwe) dakika chache baada ya kumalizika kwa kikao alichokifanya na waandishi wa habari Dar es Salaam leo.
 Zitto IIZitto I

WAIJUA HIYO::MWANAMKE,MWANAUME, NANI ANAONGOZA KUTOA SIRI ZA UHUSIANO?

NIJumanne tena, safu hii ya maisha na mapenzi ipo kukuelimisha na kukupa maujuzi ili ikibidi siku moja msomaji wangu ubadilike.
Wiki iliyopita tulimalizia mada yetu ya; Unaachana naye unachukua kila kitu ulichomnunulia. Wiki hii tuna mada nyingine ndiyo hiyo hapo juu; mwanamke na mwanaume katika uhusiano nani anaongoza kwa kutoa siri nje? Au kufanya umbeya.
Nilibahatika kuzungumza na jinsia zote kuhusu mada yetu wakati naiandaa, hoja ilikuwa nusu kwa nusu, yaani ilionekana kama wote tu na si suala la jinsia.

WASEMAVYO WANAWAKE
Nilibaini kuwa baadhi ya watu walizungumza na mimi kwa utetezi huku wakiwa na ukweli mwingine moyoni, lakini pia nilijifunza kitu cha ziada kwamba, kumbe baadhi ya wanawake wenyewe wana majibu ya wazi.
Mama Piliani, mkazi wa Sinza-Palestina jijini Dar, yeye alisema kwa kawaida, mwanamke anamudu kutoa siri za ndani wakati wote, akiwa na furaha na akiwa na hasira lakini mwanaume mara nyingi hufanya hivyo pale anapokuwa na hasira ya jambo fulani.
“Mwanamke akiwa na hasira anamwambia shoga yake; ‘mimi huyu mwanaume wangu nadhani amenishinda sasa. Nikitaka tendo la ndoa anakuwa mvivu, hawezi, sijui nitoke nje, eti unanishauri vipi?’
“Akiwa na furaha atamwambia shoga yake; ‘yaani mwanaume wangu nampenda sana, kitandani yuko vizuri, ukikutana naye leo, unaweza kukaa hata wiki maana anakuwa amekata kiu yote.’
WANAUME WAO
Utafiti nilioufanya nilibaini kuwa, wanaume wengi hutoa sira za uhusiano pale tu wanapohitaji ushauri wa masuala magumu yanayowatokea. Lakini pia wapo baadhi ya wanaume nao wanapenda sana ‘ubuyu’ hivyo huanika siri zao za uhusiano bila kutaka ushauri.
ETI NI TIBA
“Mimi siwezi kumficha rafiki yangu kipenzi kuhusu magumu yanayonitokea ndani ya uhusiano. Unajua kusema pia ni tiba tosha. Kama wewe huna tabia ya kuficha mambo magumu unaweza kuja kufa kwa presha,” alisema Tamimu, mkazi wa Tandale Kwatumbo, Dar.
Kauli ya Tamimu iliungwa mkono na mkewe aliyekuwa naye kwenye Kituo cha Daladala cha Kwaremi, Dar wakisubiri usafiri.
Mke huyo alisema: “Unajua hata mtoto, akitendewa ubaya asipolia anapata tabu sana, lakini akilia anakuwa sawa. Ndiyo umbeya pia, kama una magumu katika uhusiano halafu huwaambii wenzako utapata tabu, watu watakushangaa kukuona unakonda tu, lakini ukisema unapata nafuu.”
Kuhusu kutoa sifa ya mambo mema, mke huyo alisema: “Huo sasa ni uendawazimu. Unamwambia shoga yako kuhusu mumeo anavyokutosheleza kitandani si ndiyo mwanzo wa kuibiwa!”
KITABIA
Kwa mujibu wa wataalam wa mambo ya tabia za binadamu, mwanamke kwa siku anazungumza maneno 20,000 na kumzidi mwanaume kwa maneno 13,000. Ina maana mwanaume anazungumza maneno 7,000 tu kwa siku!
Wataalam hao wanatanabaisha kwamba, tabia hiyo ndiyo inayomfanya mwanamke kuongoza katika kutoa siri za uhusiano kuliko mwanaume kwa vile wanaongea sana.
Wataalam hao wanakwenda mbele zaidi kwa kusema, umbeya au kutoa siri za uhusiano kwa mwanamke ni jambo la asili ndiyo maana watoto wa kike huanza kutangulia kuongea kuliko wa kiume ambaye yeye huwa mwepesi kwenye kuanza kutembea.
Baadhi ya wanawake wanalijua hilo ndiyo maana unaweza kumsikia mwanamke akisema: “We mwanaume mzima unakuwa mbeya kama mwanamke bwana.”Kuthibitisha hilo, vuta kumbukumbu kama kuna siku ulikuta ugomvi kati ya mwanamke na mwanaume, nani alishindwa kwa sababu ya kusema sana, lazima mwanaume alishindwa!
MADHARA
Si vibaya kwa mtu kuanika mabaya anayokumbana nayo kwenye uhusiano lakini ni vyema kufaya hivyo kwa nia ya kusaka suluhu na si kumsema mwenzako kwa lengo la kumwanika, madhara yake marafiki unaowaambia nao watawaambia wengine na wengine, na mwenzio atakuwa mtu wa kudharauliwa kwa sababu udhaifu wake utajulikana.
Ni vyema kama mwenzako katika uhusiano ana udhaifu, umsitiri kwani wewe ndiyo mwenzake. Kama udhaifu wake ni wenye kukera na kutokuvumilika nenda kwa viongozi wa dini au wazazi ili suala liwe ni shauri lenye kutatuliwa kwa hekima.

MAHAKAMANI::Picha 12 za Chid Benz alipofikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza

chid 4
Rapper Chidi Benz alikamatwa na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam juzi ambapo Mkuu wa Polisi kwenye viwanja vya ndege Tanzania alithibitisha kwamba staa huyu wa hiphop alikutwa na kete 14 alizokiri ni zake za kutumia.
Alikua kwenye safari ya kwenda Mbeya kufanya show lakini ikashindikana manake alibaki mikononi mwa polisi mpaka leo October 28 2014 alipopandishwa Mahakamani Kisutu Dar es salaam kwa mara ya kwanza na kusomewa mashitaka matatu ambayo ni kukutwa na dawa na vifaa vya kutayarishaji uvutaji wa dawa, kusafirisha dawa ya kulevya na utumiaji wa dawa za kulevya.
chid 3
Chid 1
chid 2
chid 5
chid 6
chid 7
chid 8
Chid 9
chid 10
chid 11
chid 12

HABARII::VOA YAZINDUA MATANGAZO YA ALASIRI VOA EXPRESS

Kutoka kushoto waliosimama ni Producer Dwayne Collins, Engineer Zaynab,Sunday Shomari na Harrison Kamau na waliokaa kutoka kushoto ni Idd Ligongo,Esther Githui Ewart, Mary Mgawe na mkuu wa idhaa ya Kiswahili Mwamoyo Hamza.
Timu ya VOA EXPRESS iliyofungua matangazo ya kwanza ya Alasiri saa za Afrika Mashariki saa 10.30 Jumatatu hadi Ijumaa Oktoba 27,2014.  Kutoka kushoto Mary Mgawe, Idd Ligongo ,Sunday Shomari, Esther Githui Ewart, Khadija Riyami, Dwayne Collins, Mkuu wa idhaa Mwamoyo Hamza na Harrison
Kamau.

PROFESA JK::RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YAKE RASMI YA SIKU MBILI VIETNAM

 President Dr Jakaya Mrisho Kikwete lies a wreath at
the Mausoleum of the First President Ho Chi Minh in Hanoi on  his last
leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014 .
 
  President Dr Jakaya Mrisho Kikwete visits the Hung Fen Food Stuff
Corporation at Trung Son in Hanoi on his last leg of his two-day
official visit to Vietnam today October 28, 2014
  President Dr Jakaya Mrisho Kikwete in a souvenir photo with workers of  the Garment 10 Corporation textile mill he visited at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014
 :President Dr Jakaya Mrisho Kikwete shown some historical items as
he visits the Garment 10 Corporation textile mill at Nguyen Van Linh
Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on  his last leg of
his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete visits the Garment 10
Corporation textile mill at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward,
Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit
to Vietnam today October 28, 2014.PICHA NA IKULU.

DIVISION 5 NO::JWTZ YAKATAA WANAFUNZI " VILAZA",HAKUNA NAFASI KWA WALIOFELI

 


Brigedia Jenerali, Kongo Zoma amesema Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) linahitaji wasomi wanaoendana na teknolojia iliyopo na wala halina nafasi kwa waliofeli.

Brigedia Zoma alisema hayo jijini Dar es salaam jana katika mahafali ya 19 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Airwing.
“Jeshini tunahitaji watu waliobobea katika elimu kwa kuwa tunatumia sayansi ya hali ya juu. Tunahitaji wasomi wenye uelewa wa kutosha na siyo mapooza,” alisema Brigedia Zoma.
Aliwataka wanafunzi hao kuzingatia elimu kwa kuwa ndiyo ufunguo na msingi wa maisha yao ya baadaye.
Pia aliwataka wazazi na walezi kuwekeza elimu kwa watoto wao ambayo ndiyo utajiri pekee usiofilisika.
Brigedia Zoma aliwataka wanafunzi kuwa makini na matumizi ya simu za mkononi kwa kuwa zinaweza kuharibu mfumo mzima wa malengo yao.
“Hakikisheni mnakuwa makini na simu za mkononi, mjihadhari na mjiepushe na vitendo vya uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya, zingatiemi sana maadili mliyopewa na mjiendeleze zaidi kielimu... msikubali kuishia hapa mlipo,” alisema.
“Taifa bila elimu ni sawa na upuuzi mtupu, hivyo tunahitaji viongozi wenye elimu wanaojua kuchanganua mambo na siyo wapuuzi.”
Kwa upande wa wahitimu hao, waliahidi kufanya vizuri katika mtihani wa taifa wa kumaliza kidato cha nne.
Pia walisema wazazi na walezi wanapaswa kuwalipia ada kwa wakati watoto wao ili wasome kwa amani.

KUMBE HATA HUKO:Wizi wa magari yasio na ufunguo wazidi

Range Rover
Magenge ya uhalifu yanaendelea kuyalenga magari yasio na funguo.
Kulingana na kundi moja la kampuni za magari nchini Uingereza,wezi hao huweza kulemaza mfumo wa usalama wa magari hayo kupitia vifaa vinavyotumika na fundi wa magari.
Hatahivyo watengezaji hao wa magari wanajaribu kuwa mbele ya teknolojia inayotimiwa na wezi hao kwa kuimarisha programmu inayotumika.
Imeripotiwa kuwa wamiliki kadhaa wa magari ya Range Rover nchini Uingereza wamenyimwa bima kutokana na swala hilo.
Na huku umaarufu wa magari yasio na funguo ukiongezeka,wezi wamekuwa wakinunua vifaa kupitia njia ya mitandao ambavyo vinaweza kuyafungua magari hayo.
''Uhalifu wa kuiba magari kupitia utengezaji wa rimoti zinazotumika kama funguo ni tatizo kubwa'', ilisema kampuni ya Jaguar Land Rover.
''Hatahivyo tunalichukulia swala hilo na uzito mkubwa huku timu yetu ya wahandisi wakiendelea kufanya kazi na kampuni za bima na maafisa wa polisi ili kutatua swala hili''..

JITANGAZIE NAWE::TANGAZO TANGAZO NYUMBA ZA KUPANGISHA NA KUUZWA ZINAPATIKANA JIJINI MBEYA



BMW 13m , Harrier 14m, na Spacio ya 2001, 9m, zinauzwa zote , zipo  jijini Dar es salaam.
 Kwa mawasiliano wasiliana na bwana
Daniel Golden Ngumbuke
P.O Box 7636,
Dar Es Salaam.
Email: ngumbukeson@yahoo.com, Mob Phone: 0714-160222 / 0684-160222, au dada ZAMA 0754060350.




Nyumba yenye kila kitu ndani inapangishwa: ina vyumba vitatu vya kulala, sebule kubwa, jiko, chumba cha chakula, nyumba kubwa ya uani. Kwa ujumla nyumba hii ni nzuri sana: Kodi maelewano. Nyumba zenye kila kitu ndani kwa sasa ninazo nyingi.
Kwa mawasiliano wasiliana na bwana Benard Malasuka,  0714038851,0784442681, au dada ZAMA wa simu namba 0754060350






Nyumba inazuwa ipo Ituha Tshs. 30m. Ina vyumba vitatu vya kulala self contained, ina tiles, ina nyumba ya uani ambayo haikwisha.
Nyumba nyingi zinauzwa maeneo mbalimbali kwa bei tofauti. 


Nyumba inapangishwa: ina vyumba vitatu vya kulala, kila chumba kina choo ndani,  sebule kubwa, jiko, chumba cha chakula, nyumba kubwa ya uani. Kwa ujumla nyumba hii ni nzuri sana: Kodi maelewano; Endapo utapenda uwekewe furniture inawezekana kabisa
Kwa mawasiliano wasiliana na  dada ZAMA simu 0754060350.


Mashamba yanauzwa, yapo wilayani Mbozi, Songwe, Tukuyu na kwingineko, bei maelewano. Pia tuna viwanja maeneo mbalimbali, majengo kwa ajili ya matumizi ya ofisi, maghala, majengo kwa ajili ya uanzishwaji wa viwanda , Yadi, mahoteli yanayayouzwa,nyumba zilizopo barabarani, sheli zinazouzwa Magari aina mbalimbali, Kontena  nk. 

                                   ZAMA REAL ESTATES & ADVERTISEMENTS COMPANY

Deals with: Buying, Selling, Renting Houses, Car, Land, and Advertisements
P.O.BOX 1970, Mob: 255754060350, +255686957255. BlogSpot: matangazombeya.blogspot.com, Email:matangazom@gmail.com,
Mama John, Mbeya

HABARI::Tanzania yakataa rasmi ndoa za jinsia moja kwenye agenda za maendeleo ya milenia

001
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba yake wakati akifungua warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.iliofanyika Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF)
Na Mwandishi wetu
SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.
“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy.
Amesema kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si agenda ya maendeleo.
002
Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini zinazoendelea.
Balozi Mushy aliongeza kwamba serikali ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Waziri husika kukataa shinikizo la kukubali swala ushoga kama agenda za maendeleo.
Amesema kwamba watanzania wanataka maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu, huduma bora za afya, miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa umaskini wa kipato.
Balozi Mushy alifafanua zaidi kwamba mambo ya ushoga na ndoa za jinsia yanakwenda kinyume na maadili ya watanzania, maisha, historia, utamaduni, mila na desturi za mtanzania sinakataza maswala ya ushoga.
Amesema kwamba serikali inatambua kwamba sheria ya mwenendo wa makosa ya kujamiiana yaliwekwa na mkoloni mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya Tanganyika imerithi kutoka kwenye serikali ya mwingereza.
003
Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.
“Watanzania na Afrika kwa ujumla inataka malengo ya millennia na haki za binadamu zizifike mahali kuwadharirisha watu kutoka bara hili kwa kuruhusu mambo yanayokwenda kinyume na historia yao, mila na desturi za mwafrika,”aliongeza.
Kwa upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano amesema kwamba malengo ya milenia kwa kiasi kikubwa yamefikiwa na Tanzania hasa katika upande wa elimu na kupunguza vifo vya wakinamama na watoto wakati wa kujifungua.
“leo tumekutana hapa kuzungumza ni kwa kiasi ngani nchi yetu ya Tanzania imefikia malengo ya milenia na changamoto ni zipi katika malengo mapya ambayo ni 17 badala ya 8 ya awali,” aliongeza
Dkt Mashindano alifafanua kwamba ni lazima sasa serikali kutazama katika Nyanja za ubora katika huduma hizi muhimu kwa jamii baada ya kufikia lengo la kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule kwa asilimia 85.
004
Mhadhiri wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
Aliongeza kwamba Tanzania na dunia kwa ujumla wameona ni muhimu kuweka agenda ya ubora katika kila agenda za malengo ya milenia kwa nchi zote ambao ni wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii, amesema kwamba malengo haya ya milenia ni lazima yaguse maisha ya watu katika ngazi ya chini ili matokeo chanya yaweze kuonekana kwenye jamii
Amesema kwamba ni lazima nchi zilizoendelea ziweke mkazo katika kuhakikisha kwamba nchini zinazoendelea zinajengewa uwezo wa kutafuta fedha za kutimiza malengo ya milenia.
005
Mdau akichangia mada yake.
006
Wadau wakifurahia jambo wakati ya warsha hiyo.
007
Wadau mbalimbali walioudhuria wakifuatilia mada mbalimbali.
008
009