Diva:Sijampenda Gk Sababu ya Pesa Au Umaarufu Nampenda Yeye Kama Yeye
Ile hatua ya U boifriend na U girlfriend
ikiwa imepita na kuingia katika hatua ya uchumba wa mahaba kedekede,
dada yetu Diva alijikuta anamwaga chozi baada ya watu mbalimbali
kumtupia maneno kwamba amempendea King Crazy Gk umaarufu wake ili abaki
kupata KIKI Mjini.
Diva alijikuta anatoa maneno makali ya
hasira na kuangua kilio na kudai kuwa hajampendea Gk umaarufu wake
sababu yeye ni Diva ni maarufu pia hapa Tanzania, hakuishia hapo alizidi
kudai ya kuwa amechoshwa na watu wengi kusema ana mahusiano na Gk ambae
hana Pesa na ameachana na mwanaume ambae anapesa na cheo kikubwa
Tanzania.
Diva:Nimechoshwa kuulizwa maswali ya
Prezzo au mwanasiasa sababu huko siko tena na sina mahusiano nao zaidi
ya urafiki wa kawaida wa kuongea nao kama watanzania wenzangu na pili
amedai kuwa hana hisia zozote za kimapenzi na watu hao sababu yeye yuko
na Mpenzi wake na anafurahia mapenzi hayo na mume wake ambae ni Mungu wa
Muziki Tanzania.
Diva Binti mwenye mvuto na umbo la
kuvutia na mvuto wa sura ya babyface na macho ya duara alidai kuwa King
Crazy Gk ni Mtu mwenye kipato kizuri tu ila sio mtu wa kujionyesha au
kuishi maisha ya kujionyesha na ni mtu mtaratibu anaeishi maisha yake
alioridhika nayo na anatumia pesa zake kulipia elimu na kufanya mambo
yake na biashara zake binafsi tofauti na watu wanavyomfikiria. Diva la
Diva alisema kuwa Hakumpendea Gk Pesa au Umaarufu wake amempenda yeye
kama yeye na anachukia baadhi ya watu kumuingilia kimawazo maisha yake
ya mapenzi ambayo mashabiki wengi wameonekana kuvutiwa nayo kupitia
mtandao wa instagram.
No comments:
Post a Comment