Wednesday 13 August 2014

KWANIN UNADHANI TUNDU LISSU anafaa kuwa RAIS 2015?

Tundu Lissu: Nitawania Urais Kupitia CHADEMA 2015

Written By Udaku Specially on Wednesday, August 13, 2014 | 12:41 P

MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kwa mara ya kwanza amefunguka na kusema ana nia ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 iwapo chama chake kitaridhia.

Ametoa kauli hiyo ikiwa ni miaka miwili tangu Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), alipojitokeza hadharani akisema kwamba hatawania tena ubunge katika jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu ujao na badala yake atajitosa kwenye urais.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Zitto ilisababisha mvutano mkubwa kati yake na viongozi wenzake ndani ya chama hicho, huku mmoja wa waasisi wake, Edwin Mtei, akipinga uamuzi wa mwanasiasa huyo na akidai hakuutoa wakati mwafaka.

Mtei alisema hatua ya Zitto kutangaza kutaka kuwania urais wa mwaka 2015 haikuwa na shida kwa sababu alionyesha hisia zake lakini alikuwa ikitengeneza mzozo ndani ya chama.

Mwanasiasa huyo alimshauri Zitto kuhakikisha anakiunganisha chama na si kukigawa na kukivuruga.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na MTANZANIA mwishoni mwa wiki iliyopita, Lissu alisema ana uzoefu wa uongozi hivyo yuko tayari kuwania urais iwapo vikao vya chama chake vitaridhia.