Kaimu Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya,
Mhandisi Masuka Nkina (wa kwanza kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu
ya utendaji kazi wa mizani ya Nkangamo katika barabara ya Tunduma – Laela- Sumbawanga.
Utendaji wa mizani hiyo ni kwa kutumia kompyuta ambapo mteja anachapishiwa
risiti yake hapo hapo inayoonyesha taarifa zake zote. Kama mzigo utakuwa
umezidi pia risiti hiyo itaonyesha faini anayotakiwa kulia.
Daraja la Kashahanzi moja ya daraja kubwa na linalojengwa kwa umahiri mkubwa
katika barabara ya Tunduma –Sumbawanga.
Barabara hii inajengwa kwa ufadhili wa Watu wa
Marekani chini ya Mradi wa Milleniam
Challenge (MCC).
Mhandisi Happiness Mgalula, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa
barabara ya Tunduma – Sumbawanga.
Mhandisi Mgalula anaongoza timu ya ukaguzi
wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango.
Hapa anamsikiliza Mhandisi Julius Isoka ambaye ni Mhandisi
Mshauri wa Barabara ya Tunduma-
Sumbawanga kutoka kampuni ya Nicholous Odweyer akiwaelezea timu ya ukaguzi wa
miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao wanatembelea
barabara hiyo jinsi ambavyo daraja linasukwa kutoka chini mpaka juu.
Barabara hii inajengwa kwa ufadhili wa Watu wa
Marekani chini ya Mradi wa Milleniam
Challenge (MCC).
No comments:
Post a Comment