Q-CHILLAH ALAMBA MKATABA MNONO
Mbongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’ akipokea mkataba kutoka 'QS Mhonda J Company'.
'Legend' kwenye gemu la Bongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’ akipozi.
LEGEND kwenye gemu la Bongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’ amelamba mkataba wa nguvu kutoka QS Mhonda J Company ambao ndiyo watakaokuwa wakimsimamia kazi zake zote za muziki kwa sasa.
Mmiliki wa kampuni hiyo, Joseph Mhonda amesema atahakikishia anamsaidia kwa gharama yoyote nguli huyo ili arudi pale alipokuwa na kwenda mbele zaidi ikiwa pamoja na kuzindua bendi itakayokuwa ikifanya kazi zake na wasanii wenzake watakaosimamiwa na kampuni hiyo.
Akizungumzia hatua hiyo kubwa katika maisha yake ya muziki, Chillah alisema:
“Kwa miaka mitano nimekuwa kimya kwenye radio na anga ya muziki kwa jumla ikiwa ni sehemu ya kuyapitia maisha mengine nje ya muziki but thanks to God sikutegemea kupata mkataba mkubwa wa kunirudisha tena kwa nguvu zote kwa Watanzania waliomisi muziki mzuri kutoka kwangu, soon ngoma zitaanza kudondoka,” alisema Chillah.
No comments:
Post a Comment