Shutuma kufuatia mauaji ya mwandishi
20 Agosti, 2014
Kumekuwa na shutuma za kimataIfa
kufuatia kuuawa ukatili kwa mwandishi wa habari raia wa Marekani na
kundi la islamic state nchini Syria.
Waziri wa masuala ya kigeni wa Uingereza Philip
Hammond amesema kuwa mashirika ya kijasusi yanajaribu kumtambua yule
aliyemuua Foley ambaye anaoneka kuwa na lafudhi ya Uingereza.Kikosi cha wapiganaji wa kiislam wenye msimamo mkali Islamic State kimeachilia video inayoonesha mauaji ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani aliyetekwa nyara nchini Syria 2012.
Naye waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesitisha mapuziko yake na anarejea mji London .
James Foley alipotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria yapata miaka miwili iliyopita.
Mamake mwandishi huyo ambaye aliuawa na wapiganaji wa jimbo linalodhibitiwa na wapiganaji wa kiislamu nchini Syria, ametoa risala za rambirambi kwa kijana wake na kusema kuwa alipoteza maisha yake akijaribu kufichua dhuluma walizokuwa wakipitia watu wa Syria.
Katika video hiyo mwandishi huyo wa kujitegemea anaonekana kuuawa na mtu anayemruhusu kutoa semi yake ya mwisho.
Mpiganaji mmoja wa kundi hilo akizungumza kwa kizungu anailaumu Marekani kwa kifo cha mwandishi habari huyo.
''Kila siku mnaposhambulia jamhuri ya kiislamu manadhuru maisha ya muislamu na hivyo tunachukua maisha yetu ili iwe onyo kwako (rais) Obama''
anasikika akisema kabla ya kutekeleza kitendo hicho cha kikatali.
Punde baada ya kukamilisha hotuba yake bwana huyo anaanza kumchinja Foley lakini video hiyo inazimwa .
Sekunde chache baadaye mwaandishi mwengine pia raiya wa Marekani Steven Sotloff, anaonekana kabla ya ilani kutolewa kuwa hatima yake iko mikononi mwa Obama na hatua atakayochukua .
Scotloff alitekwa mwaka wa 2013 nchini Syria karibu na mpaka wa Uturuki.
Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley auawe.
Katika video hiyo iliyobeba ujumbe unaosomeka kua ujumbe kwa Marekani,mwandishi huyo pia alionekana akiwa chini ya ulinzi wa mtu aliyekua amevalia kinyago usoni,askari huyo alikua akizungumza ndani ya lafidhi yenye athari za Uingereza,akisema kua kifo cha mwandishi huyo ni matokeo ya mashambulizi ya mabomu yanayowalenga wa Iraq