Dk Slaa mbele ya wafuasi wa Chadema wa Iringa Mjini katika mkutano uliofanyika Mlendege mjini Iringa |
Sehemu ya vijana waliohudhuria |
Akisisitiza jambo |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kimefanya mkutano katika uwanja mpana wa stendi ya mabasi ya
Mlandege, mjini Iringa; mkutano uliolezwa na wapekuzi wa mambo ya siasa wa
mjini hapa kwamba umevunja rekodi ya mikutano yote iliyowahi kufanywa na chama
hicho mjini Iringa.
Kwa kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda
wapenzi na wasio wapenzi wa chama hicho waliendelea kumiminika katika stendi
hiyo na kusikiliza kile kilichohotubiwa na baadhi ya viongozi wakuu wa chama
hicho.
Mbali na
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, mkutano huo
ulihutubiwa na Katibu Mkuu wake, Dk Wilbroad Slaa, Makamu Mwenyekiti Tanzania
Bara, Profesa Abdalla Safari na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.
Wakati Mchungaji Msigwa alizungumzia
mambo mbalimbali aliyofanya tangu alipochaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Iringa
Mjini mwaka 2010, wengine wote
walizungumzia uchaguzi wa mwaka huu wa serikali za mitaa na vijiji, uchaguzi
mkuu wa mwakani na dhamira ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja mmoja katika chaguzi zote zajazo.
Katika mkutano huo, Dk Slaa aliwataka
wafuasi wa chama hicho kwenda kwa wenyeviti wa mitaa na vijiji kwa lengo la
kuandikishwa katika daftari la kuandikisha wakazi wa kila kaya ndani ya kata.
Daftari hilo kwa mujibu wa Dk Slaa ndilo
litakalotumika kwajili ya uchaguzi wa Desemba mwaka huu wa serikali za mitaa na
vijiji.
“Ni haki ya kila mtanzania kuandikishwa
katika daftari hilo. Daftari hilo sio la CCM wala la chama chochote, ni kwa
ajili ya watanzania wote, kwahiyo akikisheni mnaandikishwa ili muwez kushiriki
katika uchaguzi huo,” alisema.
Aliwasihi wafuasi wa chama hicho
kutopuuza suala hilo kwani wakianya hivyo nafasi yao ya kushinda katika
uchaguzi huo itakuwa ndogo.
“Kwahiyo msije mkajitokeza kuilalamikia
CCM baada ya kuangushwa katika uchaguzi huo,” alisema.
Kuhusu Katiba
Dk Slaa alisema Ukawa watapita mtaa kwa
mtaa na kijiji kwa kijiji pindi Katiba inayopendekezwa itakapopelekwa kwa
wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.
“Hata ikiletwa kesho, hatuna shida,
lakini CCM ni lazima wajue kwamba tutapita kila mahali kwa lengo la
kuwahamasisha wananchi kuikataa,” alisema na kuongeza kwamba wanaikataa kwa
kuwa haitokani na mapendekezo ya wananchi.
Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwakani
Dk Slaa alisema Ukawa wako katika hatua
za mwisho za makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja mmoja katika chaguzi
zote.
Hata hivyo alisema pamoja na makubaliano
hayo kutakuwa na vigezo vitakavyotumiwa ili kuwapata wagombea safi .
“halitakuwa suala la kupeana tu, eti
kwasababu tumekubaliana hivyo, ni lazima tupate wagombea wenye sifaili tuweze
kukabiliana vizuri na CCM,” alisema.
Ili kufanikisha chaguzi hizo, chama hicho
kilisema kinahitaji rasilimali fedha na ndipo ulipotolewa wito kwa wafuasi wake
kuchangia kupitia mfumo wa simu za mkononi.
“Hatuhitaji fedha nyingi kutoka kwenu,
tuchangieni Sh200, 300 au 500 ili zisaidia katika harakati za mabadiliko,” Dk
Slaa alisema wakati Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu aliyewahi kufanya
kazi na VODACOM akitoa maelezo ya namna ya kukichangia chama hicho kwa kutumia
mitandao ya simu,” alisema.
No comments:
Post a Comment