NA GORDON
KALULUNGA, MBEYA
WALIMU wa
wilaya ya Mbeya, Jimbo la Mbeya Vijijini, wameunga mkono sera isiyo rasmi
ambayo imewahi kutolewa hivi karibuni na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa,
kuwa kipaumbele cha Serikali kiwe Elimu kwanza badala ya kilimo kwanza.
Hayo
yameelezwa jana na Mwenyekiti wa Chama cha walimu wilaya ya Mbeya, Anthony
Mwaselela, alipokuwa akisoma risala ya walimu katika maadhimisho ya siku ya
walimu duniani-Wilaya ya Mbeya yaliyofanyika katika tarafa ya Isangati, kata ya
Ilembo, mbele ya mgeni rasmi Prof. Norman Sigalla.
Mwaselela
alisema kuwa, kutokana na serikali kutoweza kuwekeza kikamilifu katika elimu,
walimu kwa sasa wanachopata na kukifurahia kwa taaluma yao ni neno Shikamoo.
“Nchi
zilizowekeza kwenye elimu kwanza, ndizo zinazotisha kimaendeleo duniani mfamo
China, hata sisi tunaweza kutoa tamko maana hatujachelewa, twaweza kimbia,
elimu kwanza badala ya kilimo kwanza” alisema Mwalimu Mwaselela.
Alisema
katika wilaya ya Mbeya inakabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na
kutowekeza katika elimu, ikiwemo suala la nyumba za walimu, madawati, ofisi za
walimu, vyoo, madai ya fedha za likizo, kuchelewa kupanda madaraja hasa kwa
walimu wanaojiendeleza na malimbikizo
Kuhusu
nyumba za walimu alisema mahitaji ni nyumba 1906, zilizopo ni nyumba 477 nazo
zina hali mbaya, mahitaji ya vyoo vya walimu ni matundu 373, yaliyopo ni
matundu 267 yenye hali mbaya na madawati mahitaji ni 21931, yaliyopo ni 17328
lakini nayo yana viraka.
“Hali hii
inatokana na kutowekeza katika elimu. Kutojipanga vizuri kwa serikali upande wa
elimu kiuwekezaji, kumesababisha walimu wengi kuwa na kero nyingi zinazowavunja
moyo kiutendaji na hata kuwafanya vijana wengi kutopenda kazi ya ualimu pamoja
na kuwa na heshima nyingi za Shikamoo”alisema Mwaselela.
Akijibu risala
ya walimu hao, Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, alisema kitaalamu
mwalimu bora zaidi ni yule wa shule ya Msingi akifuatiwa na mwalimu wa
Sekondari.
Alisema changamoto
za walimu walizosema mbele yake ni halali lakini tatizo ni uwoga wa walimu
kueleza kero zao kwa viongozi wanaohusika, ambapo kwa wilaya hiyo, asilimia 90
ya walimu hawajawahi kufikisha malalamiko yao kwa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya
ambaye ni mwajiri wao na kiongozi wa serikali ambaye ni yeye Mkuu wa wilaya.
Akielezea tatizo
la walimu kutopandishwa madaraja kwa wakati alisema kuwa, tatizo siyo la
kimfumo kama walimu wanavyotafsiri, bali ni kutotimiza wajibu wa baadhi ya watumishi
wanaohusika katika suala hilo na bahati mbaya walimu wananungunika badala ya
kufikisha malalamiko yao kwa viongozi wa serikali hasa ofisi za wakuu wa
wilaya.
“Nisisitize
kwenu walimu wenzangu kuwa, serikali yenu ya CCM, ina lengo zuri, bali wakosaji
wengi wa utumishi wa umma wanapokosea wanasingizia wegine. Wakiwazungusha na
kuwajibu kwa dharau, njoo ofisini kwangu, maana Mkuu wa wilaya ndiye mwenye
serikali”alisema mkuu huyo wa wilaya.
Alisema katika
ofisi yake anapokea walevi, wavuta bangi na watu kadha wa kadha kwa ajili ya
kusikiliza hoja wala siyo ulevi au uchafu wa mwonekano wa mtu, na akahoji
sembuse Mwalimu?
baada
ya hotuba yake, aliendesha harambee ya kuchangia madawati ya shule za
msingi za tarafa hiyo ambapo zilipatikana Milioni Shilingi sita.
No comments:
Post a Comment