Thursday, 14 August 2014

Msafara wa Urusi waelekea Kusini Ukraine


 14 Agosti, 2014

Msafara wa Urusi waelekea Kusini mwa Ukraine
Msafara wa lori zaidi ya 1000 unaobeba msaada kutoka Urusi kuelekea Mashariki mwa Ukraine sasa umebeta na kuelekea kwenye mpaka na Ukraine.
Msafara huo unaonekana kuelekea mji wa wa Rostov mji ulioko upande wa Urusi karibu na maeneo yanayodhibitiwa na waasi Mashariki mwa Ukraine.
Urusi imepinga vikali dhana kuwa msafara huo wa misaada unatumika na taifa hilo kutuma shehena ya zana za kivita kwa waasi wanaounga mkono kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.
Ukraine inasisitiza kuwa inataka wachunguzi wa kimataifa wapekue shehena hiyo kabla haijaruhusiwa kuingia ndani ya nchi hiyo.
Wakati huohuo UN imesema kuwa idadi ya vifo imeongezeka katika mapigano ya hivi punde mashariki mwa Ukraine.
Msafara wa Urusi waelekea Kusini mwa Ukraine
Kufikia sasa takwimu za Umoja wa Mataifa zinasema kuwa zaidi ya watu 2,086 ameuawa tangu mapigano hayo yaanze mwezi April.
Asilimia 50% ya vifo hivyo vimetokea katika majuma mawili yaliyopita.
Mwanahabari wa BBC anayeandamana msafara huo wa Urusi Steve Rosenberg, amesema kuwa zaidi ya lori 100 zimeondoka kuelekea kusini mwa Ukraine kabla ya alfajiri.
Haijabainika kufikia sasa iwapo magari zaidi yangeelekea mjini Kharkiv.