Posted August 13, 2014
Treni
iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 200 imepata ajali kwa kuteleza
pembeni ya reli na kusababisha baadhi ya mabehewa kuwa nje ya reli
ambapo abiria waliokuwemo ndani ya treni hiyo walilazimika kukimbilia
upande wa pili wa treni ili kuepuka lisidondoke kwenye maporomoko.
Juhudi hizo zilisaidia na hakuna mtu aliyefariki kwenye hiyo ajali
lakini watu 11 walipata majeraha na watano kati yao kupata majeraha
makubwa kwenye hii ajali iliyotokea nchini Uswisi.