Rekodi ya wizi yavunjwa huko Chile
13 Agosti, 2014
Wanaume wanane waliokua
wamevalia mavazi maalumu meupe na vikaragosi usoni wakiwa na mitutu
mkononi walilizuia gari iliyokua ikisafirisha kiasi kikubwa cha pesa
mapema wiki hii kikadiriwa kua ni dola milioni kumi za kimarekani sawa
na paundi sita nukta mbili za Uingereza. wizi huo umeelezwa kua ni wa
kihistoria katika uhai wa taifa la Chile.
Baada ya kulizuia gari hilo, majambazi hao
walianza kupakua pesa kutoka katika gari hiyo ambalo ni mali ya jeshi la
Marekani na kuziingiza katika gari ya mizigo eneo la uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Santiago.Waziri wa mambo ya ndani wa Chile Mahmud Aleuy amesema kua polisi katika uwanja huo wa ndege walichanganyikiwa baada ya kuzidiwa maarifa na majambazi hao waliokuwa wamejipanga sawasawa kutekeleza tukio hilo na kusema kua polisi walipaswa kuchukua tahadhari ya hali ya juu wakati fedha hizo zikisafirishwa , na kwamba kazi ya usafirishaji wa vifurushi na mizigo zilikua ni za mamlaka ya anga na sio polisi.
Baada ya kufanikiwa kupora kiasi hicho cha pesa! Majambazi hayo yalijigawa katika makundi mawili tofauti na kuondoka kila moja na njia yake na kusambaza misumari nyuma yake na baadaye gari moja ilitelekezwa na kukutwa tupu jirani na eneo la tukio .
Tukio kama hilo liliwahi kutokea mnamo mwaka 2006,wakati majambazi walipopora dola milioni 1.6 zilizokua zikiingia kusafirishwa katika uwanja huo huo wa ndege, na majambazi wa tukio hilo walikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani ,
Waziri wa ulinzi wa Chile Rodrigo Penailillo ameahidi kua jeshi litaisaidia polisi kuwapata majambazi waliohusika katika tukio hilo.