Friday, 15 August 2014

Wema Sepetu Afunguka 'Namchukia Halima Kimwana Mpaka Basi'

Wema Sepetu Afunguka 'Namchukia Halima Kimwana Mpaka Basi'

Udaku Specially on Friday, August 15, 2014 

 
Na Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
Wema Sepetu a.k.a Beautiful Onyinye amekula kiapo cha kumchukia dada wa hiyari wa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’, Halima Kimwana ambaye wamekuwa na bifu kwa kipindi kirefu huku sababu zikiwa hazijulikani.

Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Wema alisema ugomvi wake na Halima Kimwana hautaisha na siku zote atamuonyesha chuki za wazi sababu hana upendo naye hata kidogo.

“Kusema kweli yule dada namchukia mpaka basi, simpendi na sitompenda kamwe, haitatokea hata siku moja kwenye maisha yangu nikapatana naye, yaani suala la kupatana mimi na yeye halipo kabisa, hata yeye mwenyewe anajua simpendi maana damu zetu zimekataana, siwezi hata kuonyesha upendo wa maigizo kwake,” alisema Wema.