Habibu Mchange Akana Tuhuma za Kuhusika Kulipua Helkopta iliyombeba Mnyika na Slaa
Leo mchana katika mkutano wake na
waandishi wa habari,Mchange amewashambulia waziwazi viongozi wakuu wa
chama cha demokrasia na maendeleo na kuwatuhumu kuhiska na mauaji ya
aliyekua mbunge wa CHADEMA Tarime,marehemu Chacha Wangwe,kisha kumkana
mtu aliyehusika na mauaji hayo Deus Mallya,wakati alikuwa mjumbe katika
kamati iliyokuwa chini ya John Mnyika,na rafiki wa Mnyika lakini Mnyika
kumkana hajawai hata kumuona.
Kisha kawataja Lissu,Mbowe na Slaa
kuajiri vijana na kuwalipa kuwatesa vijana wanaoonyesha kuiunga mkono
CCM katika kampeni mbalimbali za chama,hasa kwa kumwagia watu tindikali.
Pia amesema Lissu ni mbinafsi na fisadi
aliyedhurumu fedha za miradi ya mazingira,na kujenga nyumba ya ghorofa
Tegeta,Mbowe anahujumu mamilioni ya CHADEMA,na Slaa akihujumu fedha za
chama kulipia mkopo wa NSSF.