14 Agosti, 2014
Rubani mmoja nchini Uingereza
alipoteza mwelekeo angani akiendesha ndege ya biria baada ya mkono wake
wa bandia kuchomoka wakati alipokua akielekea kutua.
Rubani huyo wa shirika la ndege la Flybe mwenye
umri wa miaka 46 , aliruka kutoka uwanja wa ndege wa Birmingham, akiwa
na abiria wapatao 47 ndani yake, wakati alipokaribia kutua katika uwanja
wa ndege wa mji wa Belfast alikumbana na upepo mkali angani ambao
ulimsababisha atue kwa ghafla ilivyo bahati hakukuwa na madhara kwa
ndege yenyewe wala abiria.Muda mfupi tu kabla ya kuielekeza ndege Dash 8 kutua kwa dharula rubani huyo alijikagua na kuona kwamba mkono wake bandia wa shoto ulikua sawa lakini baada ya tukio hilo ghafla akajikuta mkono huo umechomoka.
Ndege hiyo ilitua kwa mlio mkubwa ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa na pia ndege haikuharibika.
Rubani alisema atakuwa makini zaidi katika siku za usoni kuhusiana na mkono wake huo bandia.
CHANZO:bbcswahili.