Sunday, 7 September 2014

7 WAHUKUMIWA KIFO KWA UBAKAJI AFGHANISTAN

Posted September 7, 2014
Mmoja wa watuhumiwa hao waliohukumiwa kifo.
Hukumu hiyo wakati ikitolewa.
WANAUME saba nchini Afghanistan, leo wamehukumiwa kifo baada ya kubainika kuwa waliwabaka kwa zamu wanawake wanne waliokuwa wakitoka harusini Agosti 23, mwaka huu nje ya mji mkuu wa nchi hiyo, Kabul.
Hukumu hiyo inajiri baada ya kesi iliyochukuwa masaa mawili na nusu ambapo wawili kati ya saba hao walikana madai hayo.
Wanaume hao wakiwa wamevaa nguo za polisi Agosti 23, 2014 waliwavamia msafara wa watu waliokuwa wakitoka harusini eneo la Mji wa Paghman, karibu na Kabul na kuwatoa wananwake wanne kisha kuwabaka na kuwaibia kwa mabavu.
Hukumu hiyo ya kifo ilitolewa kwa kosa la wizi wa mabavu huku hukumu ya miaka kumi na tano ikisimamia ubakaji.
Rais Hamid Karzai aliunga mkono wito wa watu hao kunyongwa hadharani iwapo watapatikana na makosa.
HABARI: BBC

No comments:

Post a Comment