Msanii nyota wa filamu nchini, Jack wa Chuz (kushoto) akimtunza msanii mwenzake, Rose Ndauka (kulia)
Sherehe hiyo ya Rose, ambaye alizaliwa siku moja na Rais Jakaya
Mrisho Kikwete, ilishuhudia mastaa wengi wa kike walioalikwa, licha ya
kunywa na kula kwa kadiri walivyojisikia, lakini pia wakiwa wamevalia
vivazi vilivyoonyesha sehemu kubwa ya miili yao.
Msanii wa filamu nchini, Mayasa (kushoto) akitoa sapoti ya kufungua shampeni katika sherehe hiyo ya bethidei ya Rose Ndauka.
Katika pati hiyo kulikuwa na vinywaji vyenye kilevi na visivyo na
kilevi, huku pia vyakula vya aina mbalimbali vikipatikana, kiasi kwamba
hadi gazeti hili linaondoka, pombe na vyakula bado vilikuwepo.Lakini kivutio zaidi kwenye shughuli hiyo iliyoshuhudia pia Mussa Issa ‘Cloud’ anayekaimu uongozi wa Bongo Movie Unity akiutangaza upya umoja wao, alikuwa ni shoga mkubwa wa Rose, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’ambaye alionekana ‘akimkogesha’ fedha rafikiye wakati wa kutoa zawadi ulipowadia.
Akiwa kwenye sherehe hiyo, Rose alionekana kuwa mwenye furaha tofauti na siku chache zilizopita baada ya kukosana na mchumba wake huyo. Katika zoezi la vinywaji, baadhi ya waalikwa walikunywa hadi kulewa chakari na hivyo kuleta burudani nyingine.
Kwa upande wake, Rose alisema: “Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema na leo naanza kurejesha furaha yangu na kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu, kwani siku chache zilizopita nilikuwa siko poa, ila leo nafurahi na ndugu na marafiki zangu kwenye siku yangu muhimu, najua pati hii imekuwa safi na hakuna aliyeboreka maana mambo yote yako vyema kabisa.”
No comments:
Post a Comment