Neema inazidi kumuangia Diamond Platinumz na leo amepata habari njema
baada ya kutajwa kuwania tuzo ya MTV EMAs huku akipokea tuzo kutoka
nchini Australia.
Diamond amewapa mashabiki wake habari njema za ushindi wa tuzo ya AAMA
ya Australia kupitia tiketi ya collabo ya aliyopewa na Desert Eagle,
wimbo unaoitwa ‘Everyday’.
“Ningependa
niwajulishe kuwa kijana wenu nimepata tunzo nyingine toka Australia ya
Collabo bora ya Mwaka toka kwenye tunzo za #AAMMA_Awards kupitia nyimbo
niliyoshirikishwa na Desert Eagle iitwayo #EVERYDAY..... (jus wanted to
inform you that, your favourite artist @Diamondplatnunz won another
award from Australia on #AAMMA_Awards as best Collaboration song of the
Year..).” Ameandika.
Wakati huo huo, mtoto wa Tandale ametajwa kuwa moja kati ya wasanii
wanaowania MTV Europe Music Awards mwaka huu huku akichuana na wakali
wengine kutoka Afrika akiwemo Davido, Toofan (Togo) na Goldfish (Afrika
Kusini).
Msanii mwingine wa tano akisubiria kutajwa baada ya mashabiki kumpekeza
kutoka kwenye kundi la wasanii sita ambao ni Anselmo Ralph, Gangs of
Ballet, Mafikizolo, Sarkodie, Sauti Sol na Tiwa Savage.
Aidha, majina yote ya wasanii wanaowania tuzo hizo yatatajwa September 16 ambapo upigaji kura utaanza rasmi.
Hongera Diamond Platinumz, Tanzania inazidi kutajwa kwenye majukwaa ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment