Friday 12 September 2014

JITAMBUE:::SOMA SABABU TANO ZINAZOKUFANYA USIFANIKIWE KATIKA KAZI ZAKO


Leo katika JITAMBUE KWANZAtumeangazia katika sababu maalum zinazowakwamisha watu wengi wasifikie vilele vya mafanikio yao, sababu hizo ni;

(i)  KUKOSA MOTISHA.
      Mafanikio huja kwa kupenda kile unachofanya.Je, kazi unayofanya inakupa mateso? Kama umeshawahi kuwachunguza watu wenyemafanikio, basi utaona angalau wanakitu kimoja muhimu wanachokipenda na kukithamini katika kazi zao: wanapenda wanachokifanya na wanafanya wanachokipenda.Je, hili ni tatizo kwako? Kama jibu ni hapana, unaweza kuanza leo kutambua mateso uyapatayo kutokana na kazi yako. Hii takuwa ni njia sahihi ya kupata motisha wa mafanikio katika kazi yako.

(ii)  UKOSEFU WA IMANI.
        Imani ni uimara wa kujiamini mwenyewe, Mungu na wengine unaoweza kuwaamini. Jenga maono imara kwa kila jambo unalotaka kulikamilisha.Kufanya hivyo itakupa moyo wa kufanya kazi bila kurudishwa nyuma na mtu yeyote, kwani binadamu tupo wakati mwingine ili kurudishana nyuma kwa kuona wivu na chuki katika mafanikio ya wenzetu.

(iii)  HOFU YA KUSHINDWA.
         Hofu ya kushindwa haipo, wala hofu ya mafanikio haina nafasi.Hofu husimama kama shahidi wa uongo, ukionekana kama ukweli. Hofu ni udanganyifu unaojitokeza unapotaka kufanya jambo fulani, kweli nivigumu kupambana na hofu.Lakini njia sahihi ya kuikabili hofu ni kuwasoma watu waliokwisha jambo fulani linaloendana na jambo unalohitaji kulifanya. Binadamu tumeumbwa sawa, ukiamini kuwa unauwezo hakika utaweza.

(iv)  KUTOKUWA NA MIKAKATI.
        Unapotaka kufanya biashara yenyekuleta mafanikio makubwa, ni lazima uwe na washauri wazuri.Huhitaji kupoteza muda, pesa na nguvu zako, washauri ni watu watakao kupatia mikakati madhubuti itakayokupatia moyo katika kuanzisha biashara yako.Chagua mtu yeyote anayekuvutia katika biashara, jaribu kuchunguza anafanyavipi kazi, alianzeje, hakika utafika katika biashara yako.

(v)  VIKWAZO VYA KIIMANI.
       Mara nyingi tumekuwa na vikwazo vya kiimani kuhusu kile tunachohitaji kukipata.Kwa mfano utakuwa unahitaji kufikia malengo yako lakini lakini kitu kinakwambia "hapana, siikwaajili yako, huwezi kufanya hivi" haya mawazo huchafua malengo yetu na maisha yetu.Njia pekee ya kushinda hali hii ni kusema neno "HAPANA!" mara hali hii inapotokea. Weka akilini kuwa wewe ni mtu kama watu wengine wanaofanikiwa maishani, na tambua kabisha kuwa kusudi la Mungu kukuweka wewe hai ni makusudi makuwa ya kukufanya ujiamini na umuombe kwa kila jambo.

Hivyo ni baadhi ya vitu muhimu ambavyo watu wengi wanasahau kuzingatia katika shughuli zao za kila siku.Hakika ukifuata vitu hivyo, utafanikiwa kwani wewe ni mtu muhimu sana katika jamii inayokuzunguka.

No comments:

Post a Comment