Sunday, 14 September 2014

MAKUBWA::UKATILI..!! MWANAMKE AFUNGIWA BAFUNI MIAKA MITATU BAADA YA KUZAA MTOTO WA KIKE


MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 25, RAIA WA INDIA AMEOKOLEWA NA POLISI BAADA YA KUFUNGIWA BAFUNI NA MUMEWE KWA MUDA WA MIAKA MITATU AKITESWA KWA SABABU TU ALIJIFUNGUA MTOTO WA KIKE!

PAMOJA NA MATESO YA KUNYIMWA CHAKULA MARA KADHAA, MWANAMKE HUYO ALIZUIWA KUMUONA MWANAE HUYO KWA KIPINDI CHOTE CHA MIAKA MITATU.

KWA MUJIBU WA GAZETI LA INTERNATIONAL BUSINESS TIMES, AFISA WA POLISI ALIYETAJWA KWA JINA LA SEEMA KUMAR AMEELEZA KUWA MWANAMKE HUYO ALIKUTWA AKIWA AMEDHOOFU NA BAADA YA KUTOLEWA NJE HAKUWA NA UWEZO WA KUFUNGUA MACHO VIZURI KATIKA SEHEMU YA MWANGA KUTOKANA NA GIZA ALILOLIZOEA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU BAFUNI.

SEEMA AMESEMA MWANAMKE HUYO ALIWAELEZA POLISI KUWA HATA WAKWE ZAKE (WAZAZI WA MUMEWE) WALIMCHUKIA NA HII ILICHOCHEWA ZAIDI NA KIASI KIDOGO CHA MAHARI ALIYOTOA ILI KUFUNGA NDOA YA MUMEWE HUYO NA KWAMBA SIKU ZOTE WALIKUWA WAKIMTAKA AONGEZE KIASI HICHO.

KWA UTARATIBU WA BAADHI YA MAKABILA YA KIHINDI MWANAMKE NDIYE ANAELIPA MAHARI.

UCHUNGUZI WA POLISI UMEBAINI KUWA TANGU MWANAMKE HUYO AFUNGE NDOA NA PRABHAT KUMAR SINGH MWAKA 2010 AMEKUWA AKITESWA MARA KWA MARA NA MUMEWE HUYO HUKU WAKWE ZAKE WAKIMTAKA KUONGEZA MAHARI NA KUMSAKAMA KWA KUJIFUNGUA MTOTO WA KIKE

No comments:

Post a Comment