jumbe
wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vyama vya Siasa
vinavyounda TCD, Mhe. John Cheyo.
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
MJUMBE
wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD Mhe. John
Cheyo amewataka Watanzania kutodanganywa kuhusiana na mchakato mzima wa
kusaka Katiba Mpya.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mhe. Cheyo wakati alipokuwa akifanya mahojiano
katika kipindi cha asubuhi cha Jambo kinachorushwa na Televisheni ya
Shirika la Habari Tanzania (TBC).
Mhe.
Cheyo amesema kuwa ni vema viongozi kuacha kusema uwogo na kuwa
waungwana katika mchakato wa kutafuta Katiba Mpya kwani si vema kuitakia
Tanzania mabaya bali ni kutaka mchakato huo wa Katiba uendelee kwa
amani.
Ameongeza
kuwa Taifa la Tanzania linahitaji kuwa Taifa lenye nguvu kwani amani
haiwezu kuwekewa thamani kwa vurugu, hivyo ametaka amani iliyopo nchini
ilindwe na kuepuka kudanganywa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema
na nchi.
Mhe.
Cheyo ameshangazwa kwa kitendo cha viongozi wa UKAWA kutoweka ajenda ya
kurudi ndani ya Bunge hilo wala kuzungumzia kuhusu suala hilo la kurudi
ndani, bali wamekuwa wakitaka wajumbe wengine walioko ndani watoke kwa
kusema kuwa bunge hilo sio halali.
“Nawashangaa
UKAWA kwa kutoweka ajenda ya kurudi ndani ya Bunge hili Maalum la
Katiba na badala yake wao wanaweka ajenda ya kutoka ndani ya bunge hili
tena kwa nguvu”, alisema Mhe. Cheyo.
Aidha,
Mhe. Cheyo amewataka vijana nchini wawe na mshikamano na kuepuka
kudanganywa na viongozi kwa kuambiwa mambo yenye uwongo huku akisisitiza
kuwa Rais aliyeko sasa hivi ana nia njema ya kuipatia nchi Katiba iliyo
bora na yenye kumfaa kila Mtanzania.
“Vijana
achene kuvunjika miguu yenu bure, achene kukimbia kimbia barabarani
huku mkilishwa maneno yenye uongo kuhusiana na mchakato huu wa Katiba,
vunjikeni miguu kwa kufanya kazi kwa bidiii na sio kusikiliza uwongo”,
alisema Mhe. Cheyo.
Akizungumzia
kuhusu TCD, Mhe. Cheyo amefafanua kuwa TCD ni Jukwaa la majadiliano kwa
ajili ya maridhiano na mapatano pale panapokuwa na tofauti kati ya
vyama vya siasa.
“TCD
ni Jukwaa kwa ajili ya kufanya majadiliano na si vinginevyo, hii ni
meza ya maridhiano na nawaambia kuwa huko mnapokwenda ni kuchepuka,
rudini ndani kwenye njia kuu”, alisisitiza Mhe. Cheyo.
Naye
mjumbe wa Kamati namba Sita ya Bunge Malaam la Katiba Mhe. Steven
Wasira amewaasa Watanzania kwa kusema kuwa, watu wanaosema kuwa Bunge
limenyofoa baadhi ya mambo muhimu yanayohusu wananchi ni waongo na wenye
nia ya kupotosha Umma wa Tanzania.
“Kuna
watu wanasema kuwa Bunge Maalum la Katiba limenyofoa baadhi ya mambo
muhimu yanayohusu wananchi huo ni uwongo, ni mambo gani hayo
yaliyonyofolewa? kwasababu kuna mambo mengi yameongezwa na kuboreshwa
katika mapendekezo kwa ajili ya makundi mbalimbali ndani ya hiyo
Rasimu”, alisema Mhe. Wasira.
Mhe.
Wasira ameongeza kuwa katika Bunge hilo kuna Ibara ya Rasimu ya Katiba
na sio ibara za CCM, amewataka Watanzania nchini wafanya uchunguzi na
kusikiliza kwa kuchambua ili kupata ukweli wa hayo.
“Sisi
tuko tayari kuvaana na viopngozi wowote kwani tunataka Watanzania wote
waamini shughuli zifanywazo ndani ya bunge hili na waepuke kudanganywa”,
alisema Mhe. Wasira.
-MWISHO-
No comments:
Post a Comment